Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Kwa muda mrefu sasa, wakopaji wengi wa mitandaoni wamekuwa wakilalamika kuhusu kitendo cha baadhi ya apps za mikopo ku-access list ya mawasiliano ya wateja na kisha kuwatumia message baadhi ya contacts iwapo mteja ameshindwa kulipa.
Soma pia: Serikali ipitie upya Sheria ya 'Mikopo ya Mtandaoni (Online)'
Tabia hiyo ilifika hatua mbaya zaidi kiasi cha baadhi ya kampuni kuanzisha magroup ya Whatsap na kuadd baadhi ya contacts unaowaheshimu na kuweka picha za wadeni wao ili kuwapa presha za kulipa madeni wanayodaiwa.
Siku ya jana BOT walitoa muongozo rasmi kujibu vilio vya wananchi ambapo katika muongozo huo, BOT umeweka miongozo ifuatayo (Nime-summarize)
Ningependa kuwapongeza BOT kwa kusikiliza kilio cha watanzania wengi.
Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia website ya BOT
Nawasilisha

- Hairuhusiwi kwa kampuni moja kumiliki apps mbili au zaidi za mikopo
- Kampuni za mikopo haziruhusiwi kushare taarifa za mteja kwa watu au makampuni za nje ya nchi
- Hairuhusiwi kwa kampuni za mikopo mitandaoni kukusanya namba za simu, meseji, picha, email au taarifa nyingine zozote kwenye simu yako
- Mdhamini wa mteja ni lazima afahamishwe kuwa amechaguliwa kuwa mdhamini na akubali
- Watu wa huduma kwa wateja hawaruhusiwi kutumia lugha chafu na kejeli kwa wateja
- Ni marufuku kuchapisha taarifa za mteja mtandaoni iwapo atafeli kulipa deni
- Ni marufuku kwa kampuni kumtaka mteja kulipa riba au pesa yote anayodaiwa kabla ya tarehe ya makubaliano
- Ni marufuku kutuma meseji kwa contacts za mteja ili kumuonesha kuwa anadaiwa