BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!

Wakuu,

Kwa muda mrefu sasa, wakopaji wengi wa mitandaoni wamekuwa wakilalamika kuhusu kitendo cha baadhi ya apps za mikopo ku-access list ya mawasiliano ya wateja na kisha kuwatumia message baadhi ya contacts iwapo mteja ameshindwa kulipa.

Soma pia: Serikali ipitie upya Sheria ya 'Mikopo ya Mtandaoni (Online)'

Tabia hiyo ilifika hatua mbaya zaidi kiasi cha baadhi ya kampuni kuanzisha magroup ya Whatsap na kuadd baadhi ya contacts unaowaheshimu na kuweka picha za wadeni wao ili kuwapa presha za kulipa madeni wanayodaiwa.

Siku ya jana BOT walitoa muongozo rasmi kujibu vilio vya wananchi ambapo katika muongozo huo, BOT umeweka miongozo ifuatayo (Nime-summarize)
  • Hairuhusiwi kwa kampuni moja kumiliki apps mbili au zaidi za mikopo
  • Kampuni za mikopo haziruhusiwi kushare taarifa za mteja kwa watu au makampuni za nje ya nchi
  • Hairuhusiwi kwa kampuni za mikopo mitandaoni kukusanya namba za simu, meseji, picha, email au taarifa nyingine zozote kwenye simu yako
  • Mdhamini wa mteja ni lazima afahamishwe kuwa amechaguliwa kuwa mdhamini na akubali
  • Watu wa huduma kwa wateja hawaruhusiwi kutumia lugha chafu na kejeli kwa wateja
  • Ni marufuku kuchapisha taarifa za mteja mtandaoni iwapo atafeli kulipa deni
  • Ni marufuku kwa kampuni kumtaka mteja kulipa riba au pesa yote anayodaiwa kabla ya tarehe ya makubaliano
  • Ni marufuku kutuma meseji kwa contacts za mteja ili kumuonesha kuwa anadaiwa
Hayo ni machache tu wakuu.

Ningependa kuwapongeza BOT kwa kusikiliza kilio cha watanzania wengi.

Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia website ya BOT

Nawasilisha
Serikali ilitakiwa iwafungie hawa.
Si walisema watawafungia kabisa!??
Mbona wamebadilika!?
 
Serikali ilitakiwa iwafungie hawa.
Si walisema watawafungia kabisa!??
Mbona wamebadilika!?
Principle ya BOT ni "monitoring and inovation". Kufungia kabisa ni kuua ubunifu katika sector mpya ya digital lending. BOT wamefanya vzr kujikita ktk kuregulate, na siyo kufungia. Biashara ya digital lending lazima iendelee.
 
Hapo hamna jipya. Watu wataendelea kukopeshwa kwa siku 4 mpaka 6 tofauti na vibali vyao
Udhalilishaji upo palepale.
Riba mpaka 80% iko palepale.
Nawajua vizuri hawa wakopeshaji kuliko BOT ambao wametoa vibali.
Kwani ni BOT waliowapa kibali cha kutukana watu zamani?
Kwani ni BOT waliowapa mamlaka ya kutoa mkopo wa siku 3?
Kwani ni BOT waliowapa mamlaka ya kutoa riba ya mpaka 80% kwenye mikopo ya siku 5?
Hawa jamaa hawaiogopi serikali. Na wataendelea kufanya hivyo.
 
Kwa riba zenu za kitapeli mtapigwa sana, we unamkopesha mtu elfu 50 kisha unamkabidhi elfu 45 halafu unataka akurudishie elfu 90 kweli? Mtumiege akili sazingine. Huna ofisi kusema labda utalipa pango ila unataka riba kubwa kuliko hata benki. Shenzi type!!!
Hakika,yaani hadi mtu unaona umeumizwa kabisa hata kama ulikuwa na shida
 
Hiyo riba ni zaidi ya 80%
BOT wasicheze na akili za Watanzania.
Inakuwaje deni la wiki moja lizae riba ya 40-90%?
Maana app nyingi mkopo ni wa wiki ambapo siku ya 4 tu wanadai pesa yao
Hawa waondoshwe nchini.
Wamekiuka Sheria miaka mingi
BOT ndio waliokubali watanzania tuumizwe,inakuaje yeye kama msimamizi anasikia malalamiko yote haya na hachukui hatua madhubuti
 
Hiyo riba ni zaidi ya 80%
BOT wasicheze na akili za Watanzania.
Inakuwaje deni la wiki moja lizae riba ya 40-90%?
Maana app nyingi mkopo ni wa wiki ambapo siku ya 4 tu wanadai pesa yao
Hawa waondoshwe nchini.
Wamekiuka Sheria miaka mingi
BOT sijui wana regulate nini sasa maana hapo intelijensia ilitumika kung'amua kuwa watu wanasumbuliwa hata wasiohusika ilitakiwa ing'amue pia kwamba riba sio radiki ndo maana watu wanakimbia.
 
Juzi kuna kampuni inaitwa flexi walinitumia meseji na kunipigia simu wanataka nikope kwao.
Binafsi natumiaga branch hawana riba kubwa na marejesho ni siku 30.

Sasa jana nikasema ngoja niwajaribu, aisee riba ni 37 kwa wiki.
Flex wasumbufu sana. Namba yako ikiingia kwenye mfumo wao tu watakupigia kila siku ili ukope. Mimi nimewablock
 
Wakuu,

Kwa muda mrefu sasa, wakopaji wengi wa mitandaoni wamekuwa wakilalamika kuhusu kitendo cha baadhi ya apps za mikopo ku-access list ya mawasiliano ya wateja na kisha kuwatumia message baadhi ya contacts iwapo mteja ameshindwa kulipa.

Soma pia: Serikali ipitie upya Sheria ya 'Mikopo ya Mtandaoni (Online)'

Tabia hiyo ilifika hatua mbaya zaidi kiasi cha baadhi ya kampuni kuanzisha magroup ya Whatsap na kuadd baadhi ya contacts unaowaheshimu na kuweka picha za wadeni wao ili kuwapa presha za kulipa madeni wanayodaiwa.

Siku ya jana BOT walitoa muongozo rasmi kujibu vilio vya wananchi ambapo katika muongozo huo, BOT umeweka miongozo ifuatayo (Nime-summarize)
  • Hairuhusiwi kwa kampuni moja kumiliki apps mbili au zaidi za mikopo
  • Kampuni za mikopo haziruhusiwi kushare taarifa za mteja kwa watu au makampuni za nje ya nchi
  • Hairuhusiwi kwa kampuni za mikopo mitandaoni kukusanya namba za simu, meseji, picha, email au taarifa nyingine zozote kwenye simu yako
  • Mdhamini wa mteja ni lazima afahamishwe kuwa amechaguliwa kuwa mdhamini na akubali
  • Watu wa huduma kwa wateja hawaruhusiwi kutumia lugha chafu na kejeli kwa wateja
  • Ni marufuku kuchapisha taarifa za mteja mtandaoni iwapo atafeli kulipa deni
  • Ni marufuku kwa kampuni kumtaka mteja kulipa riba au pesa yote anayodaiwa kabla ya tarehe ya makubaliano
  • Ni marufuku kutuma meseji kwa contacts za mteja ili kumuonesha kuwa anadaiwa
Hayo ni machache tu wakuu.

Ningependa kuwapongeza BOT kwa kusikiliza kilio cha watanzania wengi.

Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia website ya BOT

Nawasilisha
Good move
 
BOT fungieni hawa watu hakuna manufaa yoyote kwa mtanzania kwa sababu madhara ni makubwa kuliko faida.Sisi waathitika tunashauri muwafungie hii biashara.Sisi watanzania wenye nchi tunasema fungieni hii biashara ambayo inafanywa na wachina pamoja na wakenya wakishirikiana na watanzania wachache.Tumeona madhara yake ikiwemo kuwa na madeni lukuki hivo inabidi uendelee kukopa kwenye app zao mbalimbali ili ukamilishe madeni ya APP zingine wakati huo riba ni kubwa sana na siku ni chache (5-6)hivo unabaki kuwa mtumwa wa madeni ambayo hayalipiki na hakuna faida unayopata zaidi ya kugombana na ndugu zako, marafiki,wafanyakazi wenzio kwa sababu ili uweze ku maintain pressure za hawa wachina na wakenya wa APP za mikopo inakubidi ukope na kwa watu wako wa karibu hivo husababisha ugomvi na chuki miongoni mwa jamii wakati huo huo aliekopa akiendelea kuwa na madeni kwa sababu inafikia wakati hayo madeni hayalipik tena.kUMBUKA kuwa utapigiwa simu kuanzai saa kumi na moja alfajir hadi usiku wa manake ukipokea vitisho na maneno ya kejeli muda wote unakuwa huna amani badala ya mkopo inakuwa SHARI sasa.Hebu fikiria saa saba usiku mkeo anapigiwa simu eti anaambiwa tunajua uko na jamaa hapo mwambie alipe ! Saa saba usiku wakati umelala na mkeo ! Hii ni zaidi ya ushenzi !
Nawashauri BOT wafanye reseach katika jamii juu ya suala hili ili waujue ukweli na research yenyewe iwe direct one to one na wale walioathirika watapata A to Z ya tatizo hili kubwa.
Narudia tena BOT funga hii biashara ya mikopo ya APP mitanadaoni.
CCM waelekezeni BOT wafunge hii biashara tafadhali.
Na pia wakati BOT wakivuta miguu kufunga biashara hii TRA fuatilieni hizi APP , pesa nyingi sana mapato ya serikali zinaenda kwa wajanja wachache bila kulipa kodi wakati hawana ofisi ya kuwa trace wala kuwa hold responsible.
Huu ni UHUJUMU UCHUMI

Narudia tena BOT na serikali ya sikivu ya CCM fungia hawa watu !
 
Mkuu nakuunga mkono.kwa asilimia Mia kwa mia
 
Back
Top Bottom