GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 4,291
- 5,786
Nilichojifunza kuhusu BRELA ni kuwa: Watumishi wengi hawajawa na ujuzi wa kutoa huduma kupitia mtandao. Kipindi cha JPM ndio walikuwa wanapewa "Tuition" wakiwa kazini, hata hivyo hadi leo wachache wanaojua kidogo huishia kutoa huduma kwa malipo ya pembeni.
Mfumo wenyewe wa OBRS haufanyiwi "Update" hata kama una computer yako, ukituma maombi mfumo unajibu kupokea lakini hutapata mrejesho. Kwenye malipo ndio kabisa, pesa ukilipa hata kwa makosa hairudi hiyo, ukienda kudai wanakwambia ujaze fomu ya marejesho.
Kifupi tu ni kuwa BRELA ni tatizo zaidi kuliko kuwa suruhisho la urahisi wa kufanya biashara. Kwa usumbufu uliopo kwenye taasisi hiyo niliamua kuachana nao kabisa kwa miaka mitatu hadi juzi nilipowafuata kwenye maonyesho yao Mlimani City. Wengine wanaofuata mtindo usioeleweka kama BRELA ni mamlaka ya leseni. Huko nako hali ni hiyo hiyo ya kurubuni watu watoe rushwa.