Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin

Hizi ndio historia watoto wetu wanapaswa kuzijua, na ikiwezekana zichapishwe kwenye vitabu vya shule itapendeza, acha zile historia za kutengenezwa na western na mipicha yao ya kuchora eti mtu amefungwa minyororo na waarabu kisha anateswa. Akili zingine bwana, unabakia kucheka tu 🤣🤣🤣🤣

Hapa akili naona zimeanza kujirudi. Mzungu sio mtu ila wachache tu wenye kujitambua.
 

Some of the information because of the time that has lapsed, should be subjected to diclassified information and be allowed for sharing.

Our young generation wont understand some of these things that our fathers attained by sweat and blood.

Waisrel na wengine wote wanafanya hivyo. Tusije kusahau kuwa Taifa letu liko safarini tena njiani na lina mengi ya kujifunza
 
Sio hizi za wababaishaji wa leo wanatuchanganya tu🤣🤣🤣🤣
 
..tunapotofautina mimi na wewe ni kuhusu kubadilishana majukumu kati ya Tumainieli Kiwelu na David Musuguri.
Kwenye mahojiano na Raia Mwema, Kiwelu anaweka wazi, alifanya survey ya kuvuka, akaongoza kuvuka na hata kutoa operation order. Baada ya hapo aliripoti kwa amir Jeshi mkuu kwamba kazi ya kwanza imekwisha.

Halafu anasema, akamkabidhi Musuguri kuendesha kazi ya kuingia Uganda yeye akirudi makao makuu kwa ajili ya kutafuta nguvu ikiwemo vifaa kutoka kwa nchi marafiki, kazitaja.

Hadi hapo Kiwelu anatueleza vita ilikuwa na hatua mbili. Demarcation inaweza isionekane kirahisi kwani pande zote mbili zilikuwa vitani tena mpakani. Hata hivyo, mipango ya vita kwa mujibu wa Kiwelu inaeleza wazi uwepo wa awamu mbili, kukomboa mipaka na kuingia Uganda.

Katika vitabu vya vita ya Kagera na kama ukimsikiliza Kiwelu, kazi kubwa ilikuwa kuvuka daraja.
Ukubwa wa kazi ile unatokana na aliyosema Kiwelu, kwamba, kuna askari ambao hawakuwahi kupigana vita.
Kwahiyo ile ilikuwa 'firsthand experience'

Pili, hakukuwepo matarajio ya kuvunjwa kwa daraja
Tatu, hawakuelewa ukubwa na kujizatiti kwa jeshi la adui
Nne, kipigo cha kwanza walichopata kiliondoa morali

Ukimsoma Kiwelu katika mahojiano na Raia mwema, kuna sehemu anasema '' nikarudi makao makuu Dar es salaam kuendelea na CoS''. Kwa mantiki alikuwa 'siyo' na Mwakalindile alikuwa Acting.

Hata hivyo, kuna mkanganyiko kidogo. Kwamba, alikataa kumpa habari Sokoine inaonyesha ni katika capacity ya CoS akijua aliye juu yake ni CDF. Pili, alidhibiti habari na kueleza kuwa ikibidi habari ziende atapeleka mwenye Ikulu inaeleza ukuu wake na hasa CoS. Lakini pia yeye ndiye aliyetangaza 'operation order'' usiku ule. Kwa maana hiyo ni CoS, CDF na Amir Jeshi mkuu waliojua mpango.

Kwa mtazamo wangu hapa palihitajika maelezo mengine na ndiyo maana tunashauri kuwatumia washiriki kama Meja jenerali Msuya ambaye ni mmoja wa watu walio hai na walioshiriki kwa ukaribu sana.
 

Unapokataa kuongea na waziri wa ulinzi na waziri mkuu, unawezaje kuendelea kukaa mstari wa mbele? I think alirudishwa kwenye madawati ili asifanye mambo ya kiutawala kuwa magumu
 
Unapokataa kuongea na waziri wa ulinzi na waziri mkuu, unawezaje kuendelea kukaa mstari wa mbele? I think alirudishwa kwenye madawati ili asifanye mambo ya kiutawala kuwa magumu

..alirudi ktk jukumu lake la Chief of Staff wa jeshi.

..Na CoS ndiyo engine ya jeshi, kwa maana anashughulikia masuala ya utayari, nidhamu, na maadili, ktk jeshi.

..Wasikilize hapa askari mbalimbali waliopata kuhudumu kama CoS.

 


We jamaa nnimekusoma kwenye nyuzi 2 tofauti kuhusu vita y kagera, nimegundua Ni mbishi tu na unalazimisha watu waelewe kile unachoamini. Sometimes unaharibu radha ya uzi kwa ubishi wako wa kimaandazi
 
Brig Gen Kabunda yupo, ni mstaafu.
 
We jamaa nnimekusoma kwenye nyuzi 2 tofauti kuhusu vita y kagera, nimegundua Ni mbishi tu na unalazimisha watu waelewe kile unachoamini. Sometimes unaharibu radha ya uzi kwa ubishi wako wa kimaandazi
Usiponielewa utaona kuwa ni mbishi; ukweli ni kuwa jukumu la kusimamia vita ile lilipewa CoS wa wakati huo, lakini yeye kusimamia vita haina maana kuwa ndiye aliyeingia vitani na wapiganaji. Makamanda wote walioingia vitani na vikosi vyao wanajulikana. Lakini makamanda hao wasingechukua vikosi na kuvipeleka vitani bila ridhaa ya uongozi wa juu wa jeshi ambao ulikuwa unatoka kwa CoS wakati huo, siyo kwa CDF. Hiyo ni tofauti na wanaoamini kuwa kwa vile CoS ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia vita ile basi yeye ndiye aliyepigana; hicho ndicho ninatofautiana nyie wote. Kwa level ya juu ni sawa kuwa ndiye aliyengoza vikosi vyote vya vita, lakini kwenye microlevel siyo sawa kabisa kwani yeye hakuingia kwenye thiata kabisa-ambayo ndiyo mimi naongelea; ukishahema kuwa yeye ndiye aliyepigana, basi unaweza kusema pia kuwa Nyerere ndiye aliyepigana kwa vile ndiye aliyekuwa amiri jeshi mkuu na ndiye aliyetangaza vita ile, jambo ambalo wapiganaji hawatakubaliana nawe.
 

..Martin Mwakalindile alikuwa kaimu CoS wakati Kiwelu ametumwa mstari wa mbele.

..Kiwelu alikwenda mstari wa mbele kama kamanda mkuu wa mapigano ya kuyaondoa majeshi ya Uganda toka ardhi ya Tz.

..baada ya majeshi ya Uganda kufukuzwa toka ardhi ya Tanzania, David Musuguri akateuliwa kuwa kamanda mkuu wa mapigano ndani ya Uganda.

..Kiwelu akarejea makao makuu na ktk majukumu yake kama CoS kama ilivyokuwa kabla ya vita kuanza.

..Mwakalindile akatoka kuwa acting CoS na kupewa jukumu la kuwa kamanda mkuu wa mafunzo ya askari wakati wa vita.

NB:

..Major General Abdalah Twalipo CDF alipiga kambi maeneo ya Bukoba wakati wa mapigano ya kuondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi yetu. Lakini haielezwi wakati wowote kwamba alipokuwa mstari wa mbele kulikuwa na acting CDF.

..Sasa kwanini wakati wa mapigano hayo kulikuwa na acting CoS? Maelezo sahihi ni kwamba CoS Brigadier Kiwelu alikabidhiwa majukumu mengine, alikuwa hatekelezi majukumu ya CoS wakati yuko mstari wa mbele.

cc Nguruvi3
 
Jibu simple ni kuwa kuna makamanda wanaopanga mezani na kuna makamanda wanaotekeleza mipango iliyopangwa mezani kwa vitendo.
 
Jibu simple ni kuwa kuna makamanda wanaopanga mezani na kuna makamanda wanaotekeleza mipango iliyopangwa mezani kwa vitendo.
Jibu simple ni kuwa kuna makamanda wanaopanga mezani na kuna makamanda wanaotekeleza mipango iliyopangwa mezani kwa vitendo.

Basi kwa jibu simple hilo ni kuwa kamanda aliyepanga vita yote mezani alikuwa kanali Kitete siyo Kiwelu; ukisoma mahojiano hayo anaeleza alivyokuwa akizunguka naye kuvinjari lile eneo la mto ambapo kanali kKitete ndiye aliyeweka mkakakati wa kuwazunguka askari wa Amini kutokea Magharibi. Wakati huo kanali Kitete ndiye aliyekuwa Chief Tactician wa Ngome kabla hajapandishwa cheo kuwa Brigedia na yeye pia kupewa brigedi ya kuongoza ndani ya uganda.
 
Kipi ambacho hujaelewa kwenye post yangu!?
 
Huyo imrani Kombe, ndio huyu aliekua mkuu wa TIS, alieuwawa Moshi?
 
Huyo imrani Kombe, ndio huyu aliekua mkuu wa TIS, alieuwawa Moshi?

..Yes.

..alikuwa mmoja wa makamanda ktk vita vya Uganda.

..baada ya vita akateuliwa kuwa Chief of Staff wa Jwtz.

..Na baada ya hapo akateuliwa mkurugenzi wa Tiss.
 
Hivi vitabu vinapatikana wapi?
Unaweza kutusaidia

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…