Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia, amekutana na kufanya Mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu.
Ni baada ya Lissu kuomba kuonana naye.
Walizungumzia mambo mbalimbali kuhusu ustawi wa Tanzania.
Pia, soma
1). Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi
2). Tundu Lissu afutiwa kesi zote za uchochezi
3). Summary ya Maongezi ya Rais Samia na Tundu Lissu
Picha: Rais Samia alipokutana na Tundu Lissu nchini Ubelgiji
UPDATES: LISSU AELEZA MAMBO SABA (7) ALIYOZUNGUMZA NA RAIS SAMIA1. Ajenda ilikuwa "hali ya siasa ya nchi yetu." mazungumzo yamechukua takribasi saa moja, na mojawapo ya mambo niliyozungumza nae ni juu ya mwenendo wa kesi ya Mbowe
2. Ajenda ya pili ni suala na la vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa sheria.
3. Jambo la tatu ni suala la Katiba Mpya na nimemwambia Mh. Rais ana nafasi ya kuhakikisha tunapata Katiba Mpya na anatengeneza mfumo wa kidemokrasia.
4. Ajenda ya nne, ni inayonihusi mimi na wenzangu tuliolazimika kuikimbia nchi yetu sababu ya vitisho. Nimemwambia Rais kwa mamlaka yake, nina haki ya kupatiwa matibabu kwa mujibu wa sheria, na mazingira yanayohusu kuondolewa kwangu Tundu A. Lissu bungeni na kutokulipwa mafao yangu.
5. Nimemwambia Mh. Rais kuwa mimi Tundu A. Lissu ninahitaji kurudi nyumbani na ninahitaji atoe kauli ya kunikaribisha nyumbani na nitakuwa salama, nimehakikishiwa nitapata hati ya kusafiria, kwa kuwa yangu iliibiwa Ujerumi. Nimewaongelea pia wenzangu Wenje Ezekiah na Godbless Lema
6. Nimemweleza mh. Rais sisi Chadema hatuna wabunge Bungeni kwa kuwa wale wabunge tumewafukuza uanachama. Nimemwomba Mh. Alishughulikie hilo.
7. Ajenda ya mwisho nimemwomba Mh. Rais atuongoze katika kuliponya Taifa kutokana na majeraha tuliyonayo, kwa kutekeleza ahadi yake ya kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani.
Pia soma: Summary ya Maongezi ya Rais Samia na Tundu Lissu yaliyofanyika Ubelgiji
Ni baada ya Lissu kuomba kuonana naye.
Walizungumzia mambo mbalimbali kuhusu ustawi wa Tanzania.
Pia, soma
1). Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi
2). Tundu Lissu afutiwa kesi zote za uchochezi
3). Summary ya Maongezi ya Rais Samia na Tundu Lissu
Picha: Rais Samia alipokutana na Tundu Lissu nchini Ubelgiji
UPDATES: LISSU AELEZA MAMBO SABA (7) ALIYOZUNGUMZA NA RAIS SAMIA