BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

Waliokuwa wanalisha familia zao kwa kuchangisha wananchi kwa ajili ya kesi ya Mbowe sijui Wana hali gani
 
Akiwemo mke wako analiwa na Martin kwa kutumia hela hiyona taarifa unapewa na ndcho kinachokuuma hicho.
Sasa tafuteni jinsi ya kuishi mjini, upepo umebadilika, mmekula Hela zetu wanachadema kwa muda, Sasa utapeli umefikia kikomo
 
Una akili fupi sana, sijui kama huwa ushirikisha kichwa Chako. Hapa ni chadema imemfuata Rais au Rais ameifuata chadema?. Habari mbaya ni kwenu mliodhani chadema itaipigia serikali magoti.
 
HONGERA kwa Mama Samia Suluhu Hassan Rais wetu, Hongera Tundu Antipas Lissu, Hongera Tanzania na Watanzania. Ni ishara na nuru kwa mwanzo mwingine kwa nchi yetu. Sijali na tusijali nani alianza kumtafuta mwingine, hawa wote ni wanasiasa, watanzania wetu ambao hawana rafiki wala adui wa kudumu. Naamini Lissu anarudi, Mbowe anaachiliwa nchi itulie na chuki dhidi ya mama ipungue na hatimaye kwisha. Iwe mwanzo mwingine wa siasa zenye tija.
 
Waliokuwa wanalisha familia zao kwa kuchangisha wananchi kwa ajili ya kesi ya Mbowe sijui Wana hali gani
Wamefurahi sana since jana baada ya mawakili wa serikali kushindwa kuleta mashahidi 11 akiwepo Boaz aliyeogopa kutapishwa damu kizimbani.
 
Hivi Mbowe ameshafungwa? Hivi Mwaka 2020 kabla ya October ni Nani alikuwa Rais wa Nchi? Unafahamu historia ya kesi ya Mbowe ilianza lini kusetiwa? Usimsingizie our beloved Madam President. Usimtie damu mikononi mwake. Sasa mtashangazwa na hatima ya Kesi ya Mbowe.
 
Viva our darling mama and our beloved President, her Excellency, the only Excellency with a heart full of flesh. Be blessed madam President. We love you. Uchama tuweke pembeni tujenge nchi.
Haswa mkuu.

Uchama tuweke pembeni tujenge nchi
 
Sijui itakuwaje kwa wale bavicha ambao hawatak maridhiano
 
Safi sana mh rais karibu nyumbani Tundu Lisu tunakupenda sana
 
Hili kundi la Maria na MMM na wenzao wa kwenye Maspace leo ndio unafiki wao umetamalaki. Kumbe ZZK kukutana na Rais siku ile ya kongamano la TCD iliwauma. Leo Lissu kakutana na Mhe. Rais tena kwa yeye Lissu kuomba wacha uone anavyosifiwa. Haya majamaa ni makanjanja sana. Yaani bure kabisa.
 
Sijui itakuwaje kwa wale bavicha ambao hawatak maridhiano
Wasage chupa wanywe. Tunataka Amani. Waliokimbia nchi warejee. Walioteswa wapate faraja. Ninatamani siku Moja Mh. Rais azitembelee na kuzipa faraja zile familia zote ambazo watu wao walipotelea kusikojukikana.

Japo wapewe hata kiasi cha fedha wajenge maisha Yao maana ndugu zao ndiyo walishapotezwa. Nikiwaza hii kama mtu mzima mwenye watoto na wajukuu najikuta mwanaume mzima ninalia. Rest in Peace Wherever you are Hero's😭😭😭
 

Na kwa akili yako finyu unadhani TL kajiamulia mwenyewe kukutana na SSH bila kuushirikisha uongozi wa juu wa CHADEMA?

Acha kupandikiza fitina. Mara ngapi Mbowe aliomba kukutana na SSH akapuuzwa?

Leo hii SSH mwenyewe ndio kaomba kukutana na kiongozi wa CHADEMA.

CHADEMA ni level ingine ndugu!
 
Tundu Lisu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema amekuwa gumzo kubwa duniani na ameonekana kukubalika " zaidi " na Rais Samia ukilinganisha na wapinzani wengine akiwemo Zitto Kabwe.

Awali mama Samia akiwa makamu wa Rais alimtembelea Tundu Lisu mjini Nairobi nchini Kenya alikokuwa akitibiwa.

Na sasa wamekutana tena makao makuu ya Jumuiya ya Ulaya Ubelgiji.

Mungu wa mbinguni mbariki Rais Samia.

Mungu wa mbinguni mbariki Tundu Lisu.

Maendeleo hayana vyama!
 

Mbowe kawekwa ndani chini ya Utawala wa Samia, kama angekuwa Jela kipindi cha Magu (RIP) jambo la kwanza ambalo Samia na Tundu Lisu wangefanya ni kumtoa Jela mara moja kama walivyofanya kwenye mambo mengine yalioanzishwa na Magufuli, Samia mpaka aliomba msamaha kwa foreign leader Uhuru Kenyata na kusema live kwamba tuliwafanyia Wakenya ukatili ije kuwa hilo la Mbowe ?

Kinachomponza Mbowe ni Uwenyekiti, huo unatakiwa hivyo aidha aukabidhi kwa Makamu or else yatamkuta.
 
Lissu hawezi kushirikisha viongozi wa CHADEMA vichaa waliobaki Tanzania, hii kaipiga mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…