Acha kujifanya hujui, ficha ujinga wako hapa JF.
Wewe fahamu tu, CHADEMA waliomba kukutana na Rais Samia takribani miezi kumi iliyopita, mpango huo ukaharibiwa na wale 'mafisi' wa CCM waliomzunguka Samia na mwisho wakamlisha Samia matango pori ya kuruhusu kesi ya michongo ya ugaidi kufunguliwa.
Baada ya kesi kuwa ngumu kwa serikali, mama Samia kupoteza uungwaji mkono ndani na nje ya nchi, imebidi sasa Samia abadilishe mkondo wa siasa zake. Mambo mawili yameshafanyika ndani ya masaa 48.
1. Kasitisha mwendelezo wa kuleta mashahidi wa jamhuri kwenye kesi ya ugaidi.
2. Kakutana na Lissu nchini Ubelgiji.