Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Dah 🙆🏿‍♂️
Hata Watoto huwa wanapitia nyakati ngumu pia nakumbuka nilipokuwa na miaka 11 kuna mtoto mwenzetu alichukua uamuzi kama huo. Alichukua zile kamba za nailon za kufungia marobota ya mitumba akafunga kwenye mbao iliyokuwa inashikiria roof ya velandar bahati nzuri alipojiachia tu ile mbao ikavunjika maana ilikuwa imeshaliwa na dumuzi ilikuwa imebaki na muonekano mzuri lakinj ndani ilikuwa imebaki unga tu.

Sababu kubwa ilikuwa ni manyayaso ya Mama yake mzazi alikuwa anamtumikisha sana na maneno ya kumtukana yaani hakuna jambo alilolitenda lilikuwa jema mbele ya Mama yake.
 
November 20,leo ni International Day of the child.
Kwa maana hiyo heading ingeweza kuwa,
Leo ikiwa ni siku kimataifa ya mtoto,mtoto ajinyonga Buguruni
That is the stars for you;
Kwanza jengo linaporomoka siku Rais Samia anapopanda ndege kwenda Rio.
Halafu mtoto wa miaka kumi anajinyonga on International Day of the child.
 
November 20,leo ni International Day of the child.
Kwa maana hiyo heading ingeweza kuwa,
Leo ikiwa ni siku kimataifa ya mtoto,mtoto ajinyonga Buguruni
That is the stars for you;
Kwanza jengo linaporomoka siku Rais Samia anapopanda ndege kwenda Rio.
Halafu mtoto wa miaka kumi anajinyonga on International Day of the child.
Sikujua mkuu kama leo ni siku ya mtoto.
Ni jambo linafikirisha sana kwakweli
 
Watoto nao wanapata sonona,

Nakumbuka niliwahi shuhudia mtoto wa miaka 13 alidakwa akijaribu kujinyonga

Alikuwa kiranja wa bweni, akidaka wenzake wanaingia na chakula bwenini anawasemea kwa walimu.

Wenzake wakawa wanamtenga, hawaongei nae kabisa.

Ndo akafikia huko....
13 at least tutasema keshaingi kwenye teen age. Anaweza kupata depression
Lkn 10 ni mdogo maskin
Na kwa nini arudi shule na kufanya shughuli zake kama kawaida! Then ndio achukue maamuzi ya kujinyonga?
Sidhani kama ana akili ya kufanya yote hayo. Huyo inawezekana sn kanyongwa then kawekwa tu ionekame ka commit suicide
Rip mtt mzuri
 
13 at least tutasema keshaingi kwenye teen age. Anaweza kupata depression
Lkn 10 ni mdogo maskin
Na kwa nini arudi shule na kufanya shughuli zake kama kawaida! Then ndio achukue maamuzi ya kujinyonga?
Sidhani kama ana akili ya kufanya yote hayo. Huyo inawezekana sn kanyongwa then kawekwa tu ionekame ka commit suicide
Rip mtt mzuri
Mama mtoto analia sana, anasema mtoto mwenyewe amempata Kwa kufanyiwa Upasuaji.
Isitoshe kwenye mwezi wa 6 alifiwa na mtoto wake mwingine pia
 
November 20,leo ni International Day of the child.
Kwa maana hiyo heading ingeweza kuwa,
Leo ikiwa ni siku kimataifa ya mtoto,mtoto ajinyonga Buguruni
That is the stars for you;
Kwanza jengo linaporomoka siku Rais Samia anapopanda ndege kwenda Rio.
Halafu mtoto wa miaka kumi anajinyonga on International Day of the child.
Very bad Omen.
 
Wataalamu wetu tunao wadharau ila kesi kama hizi hawajawahi niangusha btw kwa crime scene kama hio clue ni nyingi kuanzia lock imefungiwa wapi ndani au nje
macho
Airway obs na kadhalika
Tuwe makini na maudhui ya filamu wanazoona watoto wetu
 
Hapa ndipo umuhimu wa forensic unapoonekana
kabla ya askari kufika watu kibao wamesha jazana ndani pale.
Si unajua mazingira ya uswahilini na elimu kwenye haya mambo ni kama hatuna.
Walichukua kisu wakakata ile kamba aliyojinyongea marehemu (nimesikia wanasema hili ni kosa lilifanyika)
Kwamba ilitakiwa askari ndiyo waje wamtoe pale kwenye kitanzi.
 
Zipo za chini chini
Wengine wameshaingiza imani za kishirikina maana hawa wazazi ni Wakinga kwahiyo kwamba huenda ni kafara wazazi wametoa 🤔 Kwamba itakuwaje mtoto wa miaka 10 ajinyonge?
Au kauliwa halafu kawekwa pale kwenye kitanzi kama geresha.

Bila shaka polisi watakuja na majibu ya yenye kueleweka
Waafrika utafikiri bila fikra za uchawi tungeishi milele. Mtoto anaweza kukerwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia na mwalimu wake na kutishwa akisema atauawa akaachoka akaamua kujinyonga.
Sasa maamuzi ya polisi kuweka lock up watoa msaada unafanya sisi tunaosikia hayo kukataa kutoa msaada maana unatoa msaada halafu unawekwa ndani.
 
Dada wa kazi na Fundi wahojiwe vizuri, ila sitashangaa pia watu wengine kuwa wamehusika ila kwa ujanja wakawa mbali na nyumbani wakati wa tukio.
Mida ya tukio aliyekuwepo nyumbani ni dada wa kazi na kaka Wa marehemu ambaye Kamaliza darasa la saba nadhani mwaka huu au mwaka jana.
Ila kama unavyosema huenda kuna wengine labda wamehusika ila hawajaonekana.
 
Dah Huyo dogo apumzike kwa amani,

Ila makende ya bwana fundi leo shughuli ipo
Fundi kazi anayo, tumeshinda wote leo tunapiga stori akaja kuchukuliwa mida ya jioni kwamba kuna mlango umefungwa kwa ndani aende akafungue.
Kwenda kuvunja ndiyo kakutana na huo msala.
Ni jamaa hivi ana masikio mazito (kama hasikii vizuri hivi) kazi anayo.
Ila namtakia kila la heri liwe upande wake
 
Habari za usiku wakuu! Kuna mtoto wa miaka 10 amekutwa amejinyonga chumbani kwake hapa Buguruni.

Maelezo ya kina hayajapatikana ila kwa maelezo ya awali ni kwamba mtoto katoka shule mida ya saa tisa jioni na baada ya kufika nyumbani amefanya shughuli ndogo ndogo na baada ya muda umeingia chumbani na kujifungia humo.

Dada wa kazi baada ya kuona huyu mtoto kajifungia ndani kwa muda mrefu akaanza kupiga hodi ili mtoto afungue mlango.

Amepiga hodi sana baada ya kuona kimya na tayari hapo ni jioni kama saa 11 ikabidi atafutwe fundi avunje kitasa waingie ndani.
Baada ya kuingia ndani ndipo wakamkuta mtoto amejinyonya kwa kufunga kamba kwenye dirisha.

Polisi wamekuja wameuchukua mwili wa mtoto, dada wa kazi, kaka wa marehemu na fundi aliyevunja kitasa cha mlango.
Maelezo zaidi watakuwa nayo polisi baada ya kufanya uchunguzi wao
Mambo ni mengi , tuwaombee watoto wetu huenda kuna chagamoto imemchosha ukizingatia ukatili umekua mwingi especially ulawiti ubakaji nk.
 
Back
Top Bottom