Bukoba: Ndege ndogo yapitiliza na kuingia ziwa Victoria

Bukoba: Ndege ndogo yapitiliza na kuingia ziwa Victoria

Vip Yale Mazoezi Ya Utayari Hayakufua Dafu Wakati Huu Wa Hali Halisi
 
Poleni kwa waliokua ndani ya ndege hiyo, hopes wote wametoka salama, ndugu zangu watanzania tuache upumbavu huu, hilo ni eneo la ajali sio picnic site, umati wote huo haukutakiwa uwepo hapo,je hiyo ndege ikilipuka hapo hamfikirii maafa yatakayokupata?

Hakuna kuchukua self au video kwenye eneo la ajali,ni vema vikosi vya uokoaji vikafanya kampeni ya kuwaelimisha wapumbavu hawa,stay away from accident/crime scenes for your own safe
Wabongo utawaweza?? Hawana shughuli ya kufanya all day long. Wakipata tukio ndo hivo sasa. Kila mtu ni mwandishi wa habari, anahusika na usimwulize eti inakuhusu nini?? Atakufyatukia kama javelin ya Ukraine.
 
Hii ndio JWTZ wameizamisha majini mzeeee. 😬😬😬😬 Kumbeeee Tz tupo wa Moto sanaaa
Inaweza kuwa ni mojawapo ya Topic (Mada)katika mafunzo namna ya kuepusha maafa kwa raia na mali zao. Nakumbuka tukio lile la Uwanja wa Taifa Chang'ombe enzi hizo baada ya vita ya Uganda, jamaa aliielekeza ndege nje ya uwanja na JWTZ waliokuwa kwenye hilo gwaride ndani ya Uwanja na hivyo wakasalimika.
Rubani alipewa heshima ya Ushujaa.
 
Kwa mujibu wa vyanzo vya mtaani kuna uwepo wa ndege ndogo imepitiliza na kuingia ziwa Victoria

---
Ndege yenye namba za usajili 9127 mali ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imepata ajali na kuanguka maeneo ya uwanja wa ndege manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Akizungumzia juu ya kutokea kwa ajali ya ndege hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Kagera ACP Blasius Chatanda amesema kuwa, tukio hilo limetokea hii leo tarehe 20 Julai mwaka 2023 mnamo majira ya saa 3:30 asubuhi.

Kamanda Chatanda amefafanua kuwa ndege hiyo ilikuwa katika mafunzo yanayoendelea ambapo ndani yake walikuwemo marubani wawili ambao ni Meja Renadi Revokatus Mkundwa Muha mwenye umri wa miaka (45) pamoja naye Luteni Alex Venance Moshi Mchaga umri miaka 30.

Amesema kuwa watu hao wawili wamepelekwa hosptalini na kufanyiwa uchunguzi kiafya hivyo wamebainika kuwa salama na kuruhusiwa.

Hata hivyo ameongeza kuwa chanzo cha ajali ya ndege hiyo hakikufahamika mara moja na uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajari hiyo.

Mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima amewashukuru jeshi la zima Moto na uokoaji pamoja na wadau wengine waliojitokeza na kuwahi kufika eneo la tukio mapema hatimaye kusaidia kuwaokoa marubani hao.


=====
Zoezi la uokoaji likiendelea huko Bukoba asubuhi ya leo 20, 07, 2023 baada ya Ndege aina ya Jet Fighter kudondoka ndani ya Ziwa Victoria.
Wapi majaliwa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom