Bunda: Auawa na mkewe kwa kuchomwa kisu, kung'atwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo sehemu za siri pamoja na ulimi

Kei ina nguvu sana, vijana acheni kushindana na mlipotoka. Ukiona umeoa JIKE SHUPA na uwezo wako wa kumdhibiti mdogo muache aende, hakunaga tuzo ya uvumilivu ni kifo tu utaambulia..!!!
 
Umeongea kwa hisia sana.
 
YAKOBO 4:1,2, INASEMA; 1 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? 2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! 3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

Mungu amesupply kwetu kila remedy ya maisha yetu ya kila siku. Tungalimpa Yesu Maisha yetu na kujazwa Roho Mtakatifu atakayekuwa anatuongoza, hakika hapangekuwa na mapigano wala mauaji wala magomvi, wala wivu wala chochote. haya yote yanatokana na kwamba wakati mwingine tunakuwa mbali na uso wa Mungu, hivyo tunampa adui shetani nafasi, na anaweza kukufanya chochote. kama hamjui, hao hata sio wa kuwacheka kama wewe haujaokoka, kama hujaokoka shetani anaweza kukugeuza na kukufanya chochote apendavyo kwasababu hauna uwezo wa kushinda dhambi.

kabla sijaokoka, nilikuwa nagombana mno na mke wangu, nilishampiga sana pia, nilikuwa na hasira sana, nilikuwa katili sana, nilipookoka, kila kitu kilibadilika, ninaishi nikiwa a living testimony kwamba ukiokoka Mungu huwa anakubadilisha kabisa.

enyi waume, nanyi wake, mkitaka ndoa yenu iwe salama, pambaneni ninyi kwa ninyi mmpe Yesu Maisha, kama mwenzako bado, omba na msaidie aokoke, mkiokoka nyote mtakuwa mmeziba mlango wa shetani pakubwa sana. ama la, shetani atakua anaingia na kutoka kwenu, anaweza kuleta magonjwa apendavyo kupitia mwenza wako, kwasababu mmemkataa Yesu na mmempa yeye shetani nafasi. mwenye masikio na asikie, usisubiri hadi shetani akuteketeze katika dakika za mwisho ndio umtafute Mungu, wahi mapema kabla hajakusambaratisheni.
 
na kwa wasio wanasheria, nikiwadokeza tu, hii kesi hawezi kunyongwa, ni manslaughter kwasababu kifo kimetokea wakati wa ugomvi, malice aforethought inaweza kuwa ya kutafuta. soon dada atakuwa mtaani, na ataolewa tena. ila mwenzake ndo kafa, na siajabu kafa katika dhambi. ndo maana tunasema okokeni, shetani yupo ili kuangamiza maisha ya wanadamu kabla hawajarudi kwa Mungu. shetani hua anagombanisha wanadoa,wanapigana, wanachinjana yeye kakaa pembeni, ikiwezekana wote wauane ili wote waende motoni. kuweni makini, kuishi nje ya Mungu hakuna mwisho mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…