Bunge la Katiba Haliko Kwa Ajili ya Kuboresha Rasimu ya Kina Warioba!

...what has been discussed in this thread has been largely responded to by Judge Warioba himself in today's Mwananchi paper (when responding to comments made by Werema).....haswa kuhusu tofauti za bunge hili letu la katiba na mabunge mengine ya katiba....Msomeni vizuri Warioba hapa...Warioba ampa somo Werema - Kitaifa - mwananchi.co.tz


...Pamoja na makosa yote yanayotajwa kwenye mchakato huu wa katiba....na kwa kutafakari stage mchakato ulipofikia...i would rather go with Warioba's draft...than going for massive omissions as proposed by majority CCM and pro CCM members......just my opinion though....
 

Na kiuhalisia, wabunge wa Bunge la Kawaida hawawezi kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba automatically. Wajumbe wa Bunge la Katiba walipaswa kuchaguliwa na wananchi. Hivyo, Bunge la Katiba linalokaa Dodoma ni feki na hili linafanya mchakato mzima kutokuwa halali.
 
Mkuu rasimu ikitoka bungeni, lazima ipitishwe na kura za wananchi!
Wananchi wakiikataa, rasimu inarudi bungeni kwa mara ya pili, na hapo ikikataliwa tena na wananchi, TUNATUMIA KATIBA HII HII TUNAYOTUMIA SASA!

Kura zipi? Si huwa zinaibiwa? Unaimani kweli na upigaji kura katika nchi hii?
 
Habari wanajamvi

Kwanza kuiita hii rasimu ya "Kina warioba" ni dharau kwa watanzania ambao ndiyo waliotoa maoni yaliyoifanya rasimu iliyopo.

Lakini pia kutafsiri sheria kiasi cha kuona kuwa bunge la katiba halina muunganiko na tume ya katiba ni ufinyu wa makusudi wa mtazamo wa mchakato wa kuandaa katiba. Kama watu wataendelea kufikiri na kuenenda jinsi hii kwa sababu tu ya kutazama maslahi yao. All this will be a waste of time.

Walakini mawazo hayo finyu si mwisho wa tumaini jema kuhusu katiba. Tunaamini wabunge wa katiba watakuwa makini wasiweze kuchukuliwa na upepo wa fikra kama hizi ambazi hazijali gharama za taifa wala kuheshimu michango ya wananchi. Tutazidi kumwomba Mungu si kwa ajili ya kulinda maudhui ya rasimu iliyopo. Bali kwa ajili ya hekima itaayoongoza wajumbe wa bunge la katiba. Hata tupate katiba itakayojibu mahitaji ya watanzania.

Mungu ibariki Tanzania
 
Kelele za nini si msubiri kupiga kura

Unadhani wataheshimu kura zetu? Kilichobaki wananchi tujipange, tuchukue hatua (Informal Regulation). Hawa wapumbavu wataendelea kujiona kuwa wana haki ya kufikiri kwa niaba ya wananchi. F..k Bunge la Katiba, tuchukue hatua sasa.
 
Lakini yanafanywa haya kwa maslahi ya nani na kwa nini ? dah hadi najiona boya kuwa mtanzania.
 
Kikwete kachagua asiliamia kubwa ya wajumbe kutoka katika chama chake kwa makusudi ni mpango wa CCM kukataa serikali tatu na pia nia ni kuvuruga mchakato mzima wa katiba mpya wanajaribu kupindisha mamlaka yaani bunge liwe na uwezo wa kubadili kitu chochote katika rasimu ili wakifika katika mambo ambayo wao CCM hawayataki basi wao CCM kupitia wajumbe wao ktk bunge la katiba ambao ni wengi waweze kuweka mambo wanayo yapenda wao sababu tuna ambiwa kura itatumika hivyo wao CCM watashinda tu wapo wengi,yaani kwa ujumla tusitarajie kupata katiba iliyo nzuri ambayo imetokana na maoni ya wananchi.
 
Mtafanya nini? Hamuwezi kwa lolote lile kwani CCM sasa ni taasisi ya watu wa kifamilia na si ya wananchi kwa maana ya wafanyakazi na wakulima!
 
Lakini yanafanywa haya kwa maslahi ya nani na kwa nini ? dah hadi najiona boya kuwa mtanzania.

Kama mliwezwa kugeuzwa boya na nyerere kwa kuufuta utanganyika wenu basi si ubaya kugeuzwa boya kwa utanzania wenu,zanzibar kwanza.
 

Kama unatengeneza chipsi kwa kutumia viazi vilivyooza unategemea nini?

Hebu tuambie wewe katiba ya sasa inasemaje?

Tupe na specific provisions kabisa ili tuende step by step.
 
In my humble view, Warioba na Shivji, aidha wote wanatafsiriwa vibaya au hawakujieleza vya kutosha, if not both:

Ukweli unabakia kuwa - Bunge la katiba linatakiwa ku-base its discussions kutokana na rasimu ya katiba iliyoandaliwa na tume ya katiba na sio vinginevyo. Suala la bunge la katiba kuondoa yaliyopendekezwa ndani ya rasimu iliyowasilishwa na tume ya katiba ni suala ambalo sio black and white kama makada wa CCM na wengine of the same political persuasion wanapenda iwe. In order for the constituent assembly kuondoa au kufuta kipengele au vipengele vyovyote ndani ya rasimu iliyowasilishwa na tume ya katiba, inatakiwa zipatikane two thirds ya kura za wajumbe wa bunge la katiba, vinginevyo yaliyowasilishwa na tume ya warioba yanatakiwa kubakia kama yalivyo au kuboreshwa zaidi. Hali hii ndio inatoa uhalali, haja na umuhimu wa tume ya katiba na bunge la katiba.Kumezuka mjadala mkubwa sana juu ya umuhimu wa tume ya katiba vis a vis bunge la katiba huku wengi wakihoji iwapo kulikuwa na maana ya kuwa na tume ya katiba in the first place na wengine wakihoji iwapo basi kulikuwa na maana ya bunge la katiba kuketi baada ya kazi ya tume ya katiba. Nadhani ufafanuzi huo hapo juu utasaidi to shed some light katika sula hili unfolding before us;

Kwa kuongezea, kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, confusion iliyojitokeza ni kwamba baina ya jaji warioba na shivji is a matter of practice versus theory and principle, lakini vyovyote vile, nilichojadili hapo juu kinasimama kama kilivyo.

* Wote wawili, yani Jaji warioba na Professor Shivji hawajafafanua the fact above - kwamba discussions zote za bunge hili ni lazima zitokane na rasimu iliyopo mbele ya wajumbe wa bunge la katiba na kazi yao ikiwa ni kujadili kwa nia ya kuboresha yaliyomo kwenye rasimu na baadae to draft and enact the constitution. Lakini iwapo kutatokea maamuzi ya KUFUTA au KUBADILI kitu chochote, basi ni lazima maamuzi hayo yatokane na "TWO THIRDS" ya kura za wajumbe wa bunge hili. Kura hizi zisipotimia, basi yaliyomo kwenye rasimu ya katiba yanabaki kama yalivyo; both warioba and shivji fell short of explaining this fact.

*Hoja ya Jaji Warioba inaondeshwa zaidi na practice kuliko theory kwani Jaji wariona amejikita zaidi on "practice" za siasa za CCM katika hoja yake, hasa ikizingatiwa kwamba tayari tume yake ilishapata mashambulizi makali kutoka kwa makada wa CCM. Kwa jaji warioba na wengine wenye mtazamo kama wake wanajua fika kwamba CCM itatumia "theory and principle" behind bunge la katiba "to practice" siasa za chama katika upatikanaji wa katiba itakayoendana na matakwa ya CCM.

*Professor Shivji as a constitutional lawyer, yeye hoja zake (tofauti na jaji warioba) zinaendeshwa zaidi na maelezo juu ya majukumu ya bunge la katiba in "theory" kuliko in "practice"; Lakini tukumbuke kwamba practice behind mabunge ya katiba hazifanani world wide, kwa maana nyingine, "one size doesn't fit all". Isitoshe, professor shivji kwa muda mrefu sana alikuwa akipingana na hali ya taifa kukosa katiba inayotokana na wananchi ambapo hakuwa akiitambua katiba ya 1977 kisheria kuliko alivyotambua mkataba wa muungano (1964); pili, professor shivji amekuwa akielezea sana jinsi gani mchakato wa katiba unavyofanya isivyo; ni kwa mantiki hii, ingawa anapingana na mtazamo wa jaji warioba in principle, in practice anakubaliana nae kwamba katiba mpya haitatokana na matakwa ya wananchi;

*Pia niseme kwamba Mzee Mwanakijiji (pia Nguruvi3 na wengineo) - katika suala husika wao wanajikita zaidi katika kuelezea jinsi gani practice had gone wrong from the beginning kutokana na interference ya CCM na pengine weakness kwa upande wa upinzani (hasa chadema). However, Mzee Mwanakijiji unatuchanganya kidogo pale unapotumia practical failures to justify theory and principle katika suala husika, je should practice justify theory and principle au theory/principle should justify practice in our context?

Cc Mag3, EMT, JokaKuu, Bongolander, Pasco, Zakumi, MTAZAMO, zumbemkuu, Jasusi, Candid Scope, gfsonwin, Zinedine


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Heading yako ni ya utata. Hakuna Rasimu ya Wakina Warioba. Rasimu ni ya ni maoni ya Watanzania. Ikawekwa sawa kisheria na TUME YA MABADILIKO YA KATIBA.
 

Katiba ya mwaka 1977 haikuwashirikisha wananchi kama ilivyo hii rasimu ya sasa kitu kilicholalamikiwa mara kadhaa. Pamoja na kasoro kadhaa zilizotokea katika hatua mbalimbali za rasimu hii, dhahiri ushirikishwaji wa wananchi umekuwa mkubwa kwa kiwango ambacho hakuna raia ambaye hajui inachoendelea kuhusu rasimu ya Katiba hii ya sasa.

Kwamba bunge lije na kile ambacho kiko nje ya rasimu iliyoandaliwa na kamati yake ambayo imezunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wamamchi na taasisi mbalimbali, licha ya kukubalika kwa theluthi mbili kama itakavyotakiwa kuondoa kile ambacho wabunge wasingependa kuwamo ndani ya rasimu hii ya katiba, basi dhana ya ushirikishwaji wa umma katika maandalia ya Katiba hii haiakuwa na maana iliyokusudiwa, vinginevyo kazi lingeachiwa bunge lifanye kama ilivyotokea tuliyo nayo ya mwaka 1977. Kwa maneno mengine kazi ya bunge ni kujadili rasimu hii iliyopo na si vinginevyo na kinachotakiwa kuiboresha zaidi rasimu si kuja na kitu kipya ambacho hakijatoka au kuwahusisha wananchi.

Jambo la msingi lieleweke hii si rasimu ya Warioba bali ni ya watanzania kwa kuwa wameshirikishwa kikamilifu katika kuiandaa kwa mazingira yanayowaruhusu ushiriki wao, pale inapotokea kwenda kinyume cha rasimu iliyopo ambayo ni maoni ya watanzania itakuwa ni wanasiasa kuiteka katiba na hivyo kuwavika kilemba cha ukoka wananchi walioshirikishwa tangu awali.

Hawa wasomi wa mambo ya katika kama akina Shivji wakati mwingine wanaonekana kuchanganya katika kuelimisha na ueleweshaji wa kawaida kuliko inavyotegemewa.

CC:
Mchambuzi,
JokaKuu, Bongolander, Pasco, Zakumi, MTAZAMO, zumbemkuu, Jasusi
 
Wapi constitutional review act imesema kuwa kazi ya tume ni kuboresha rasimu?
 
Nadhani hatujielewi kabisa ikiwa bunge maalum limepewa malaka ya kujadili na kupitisha rasimu je, swali kama bunge likikataa kupitisha rasimu je, hayo siyo mamlaka?
 
Kwa hiyo MM unaposema hili sio tatizo maana yake ni kwamba unapenda na unafurahia kabisa uchakachuaji wa maoni ya wananchi na unajua wazi kua watanzania hawana ujasiri na hawawezi kamwe kupiga kura ya hapana.....daah inauma sana.

Oh no! mimi nimekaa na popcorn tu naangalia picha kwa sababu hakuna chochote kinachotokea sasa au kitakachotokea baadaye ambacho hatujakisema na kikawa! Kwa hiyo hata sioni furaha wala uchungu niko kama kwenye movie theater tu naangalia watu ambao waliamshwa wakakataa kwa vile walikuwa wanapenda usingizi sasa wanaamka wanashangaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…