Bunge la Marekani lapitisha Muswada wa Sheria ya kuifungia TikTok

Hoja dhaifu
 
Sio kutojiamini, wapo makini na nchi yao. Hawa jamaa huwa wanaona mbali sana, kuna namna tu hiyo kampuni ina vitu fulani, hawabahatishi hawa.

Kupuuzia puuzia mambo ni kitu hawafanyi hawa.
Walimpuuzaga mohamed atta akawafanya vibaya,
 
EU wanataka watu wanunue bidhaa zinazozalishwa Eu na hii toka muda sana ndio maana ukinunua kitu online cha kutoka China au USA kodi inakuwa kubwa mno tofauti na ukinunua bidhaa kutoka ndani.
 
Ngoja china nao walipize kufungia mitandao ya wamarekani wao watapoteza idadi kubwa ya watumiaji.
Kunya anye kuku, akinya bata kaarisha.

Kwani china wamefungia app ngapi za kutoka huko Marekani.

Kwahiyo ikifanyiwa Marekani hamna shida, ikifanyiwa China ni nongwa
 
Kivipi tiktok yaweza kuingilia uchaguzi msaada mwenye uelewa
Kwanza ni maswala ya data za watumiaji.

Ni rahisi kujua wangapi wanasupport Mgombea A na wangapi mgombea B.

Pili, wanaweza kutumia app, kusambaza taarifa za uongo kuhusu mgombea fulani.

Au wakaminya taarifa za mgombea fulani.

Hii ni kwa ufupi tuu.
 
Kivipi tiktok yaweza kuingilia uchaguzi msaada mwenye uelewa
Wanakusoma vipendeleo vyako na kukushawishi(campaign) baada ya kusoma psychology yako, ilifanyika trump aliposhinda,Ila nyuma ya pazia ni woga tu wa marekani kwa china,kwamba ushawishi wa kiteknolojia wa china unakua,kuanzia Huawei na minara ya 5g,mpaka TikTok
 
Marekani anataka yeye ndiye atawale inapohusu teknolojia (technology hegemony) hasa ushindani unapokuwa mkali

Miaka ya 1980 walishawahi kuifanyia hivyo hivyo Japan pale walipohakikisha teknolojia ya Japan haiteki soko la dunia.

Moja ya makampuni ya Japan yaliyopigwa ban ni TOSHIBA



Miaka hiyohiyo pia Marekani walipiga ban magari kutoka Japan


Wanachofanyiwa TikTok ni mwendelezo wa sera zilezile za ukandamizi za Marekani alizofanyiwa Japan

Wakiwa kwenye media wanasiasa wa Marekani wanahubiri free trade. Wakizidiwa wanapiga ban
 
Kivipi tiktok yaweza kuingilia uchaguzi msaada mwenye uelewa
.............. kwa kusambaza uwongo na kupotoisha habari za uchaguzi.

Uhuru mkubwa walio nao raia wa marekani wa kuongea lolote lile (freedom of speech) ndio unawatafuna sasa hivi kwani hata uwongo na upotoshaji vinalindwa kisheria chini ya freedom of speech. lakini ndivyo vinavyoweza kutumika kupotosha wapiga kura wasipige kura zao sawasawa.
 
Mitandao yote ya kijamii ya Marekani imezidiwa AI Algorithm na e-commerce tech na TikTok

Ndio maana Marekani wanasema ikiwa wanataka TikTok iendelee Marekani basi OS source code iwe chini ya control ya Marekani

Huu mchezo Marekani waliifanyia TOSHIBA miaka ya 1980 mwisho wa siku Marekani wakaiba teknolojia ya kutengeneza semiconductor wakaipeleka kwa kampuni ya Marekani ya Intel

China wameshaushtukia. Ninachopendea China huwa hanaga kusanda kama Japan.
 
Hiyo ya Intel siyo kweli! Ukitaka fungua thread ya processor chipsu pate ukweli wenyewe kuliko hizi hisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…