Bunge la Senate lapongeza zuio la Paul Makonda kuingia Marekani. Lasema huo ni mwanzo wa kuwawajibisha walioua demokrasia ya Tanzania

Bunge la Senate lapongeza zuio la Paul Makonda kuingia Marekani. Lasema huo ni mwanzo wa kuwawajibisha walioua demokrasia ya Tanzania

Fanya kazi wewe tafuta hela acha ujinga. Unayemtetea yeye pamoja na familia, ndugu zake na marafiki wanakula kiyoyozi maisha matamu na walinzi kila kona.
Mabeberu wanamuogopa jemedari wetu JPM amezuia mianya yao ya upigaji kupitia miradi yao ya hovyo huku na vibaraka wao..JPM anawanyoosha mabeberu sasa wameanza chokochoko..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania hawana chuki za bila sababu kwa viongozi wao, ukiona kiongozi anachukiwa na watanzania wengi hivi basi ujue ana matatizo makubwa sana dhidi ya watanzania hao, kikwete hakuchukiwa kiasi hiki, hivi mnafkiri hakuwa na madhaifu? Wallahi mtu akipata nafasi ya kuwa kiongozi basi ajitahidi sana kuwa muadilifu na asimamie HAKI kisawasawa.
 
Mabeberu wanamuogopa jemedari wetu JPM amezuia mianya yao ya upigaji kupitia miradi yao ya hovyo huku na vibaraka wao..JPM anawanyoosha mabeberu sasa wameanza chokochoko..
Kumbuka kwa Jana hao unaowaita mabeberu wametupa msaada wa kijeshi na bado unawapigia magoti wakupe USD 500ml ya elimu. Bila wao hata Dawa hupati hospitalini. Kenge sana wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na akae akielewa, kuwa Mheshimiwa rais yeye anankinga ya kutoshtakiwa. Ila rais huyu akiondoka madarakani Makonda atatumia muda mwingi wa maisha yake mahakamani kama siyo jela sababu ametengeneza mwenyewe maadui wengi nje na ndani ya nchi na wanachofanya ninkumkusanyia ushahidi tu. Yaani huyu anayembeba na kumtetea akiondoka ataumizwa sana. Ndiyo maana wanalilia kila siku Mkuu aongezewe muda zaidi, wanajua kitakachotokea.
Makonda bado ni kijana mdogo ana familia inakua changa nadhani yeye mwenyewe ataangalia haya yanakuaje kwasababu inavyoonekana hawa wanaoitwa mabeberu wamemkalia vibaya..
Ni vizuri tukipata nafasi za uongozi tujue kuna kesho na tuna watoto wanakua..hili ni jambo zito sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yetu macho tumeandika sana hapa mzee mtoe makonda akawa anatupiga vijembe yeye apangiwi kazi [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] wameyakologa wayanywe sasa

makonda hajazuiwa kwa sababu amefanya kosa, sababu kubwa amepinga ushoga
japo simkubali mkoromije ila katika hili msishabikie


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Bro fisi akitaka kula baadhi ya watoto wake kwanza anaanza kuwashutumu kuwa wananukia kama mbuzi ili ahalalishe ulaji wake. Hii ya Makonda kuzuia ni starter kuna kitu wanatafuta. Bahati mbaya wanaopaswa kusema ukweli wanaimba nyimbo za sifa na utukufu sababu wamekula na kushiba.
Na wenyewe wamechoka, wanampiga ban Makonda kwenda Marekani ataenda kufanya nini huko kwao. Ni sawa na mimi kunipiga ban kuwa rubani wa ndege wakati hata abc kuhusu hizo ndege sizijui

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti wameua demokrasia. Demokrasia gani ya kushiba fisadi peke yao na wezi wa mfuko wa umma. Demokrasia gani ya kutoa uhuru wenye hela kuuza na kununua haki. Demokrasia gani kurusu rushwa kutawala na wananchi kua watazamaji tu kwenye uchumi ukimilikiwa na wageni. Demokradia gani wananchi wao kubakia manamba tu. Hiyo ndio demokrasia ya kiliberali huku kwetu inatoa mwanya wa nchi kugeuzwa shamba la bibi...haitufai
 
makonda hajazuiwa kwa sababu amefanya kosa, sababu kubwa amepinga ushoga
japo simkubali mkoromije ila katika hili msishabikie


Sent from my iPhone using JamiiForums
Usitufanye watoto hivi ujinga aliokuwa anaufanya ulikuwa huoni anza sakata la vyeti, njoo uvamizi wa clouds, na ujinga mwingine nyuma ya pazia ulikuwa ni ushoga eti
 
Mungu ni mwema kila wakati na atatutendea Taifa letu yaliyo mema tu. Naamini Magufuli amechokwa na kila mtu mpaka na wale waliomsaidia kuiba kura akina Lubuva, Kipilimba, Nape na Kinana. Na lazima Mkutano Mkuu umtose kama mgombea wa CCM hapo August 2020. Kama washauri wake aliamua wawe ni akina Makonda, Bashiru Ally na Pole pole badala ya wazee wetu wastaafu wenye busara na upeo basi anawajibika kwa haya yanayotokea.

Naamini kama CCM wasipomtosa 2020 tutarajie machafuko makubwa nchini kwa kuwa Magufuli hawezi akapata hata 20% ya kura za kupigwa kwa sanduku la kura. Badala yake atafanya vituko zaidi kuliko uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019. Na wananchi hawatavumilia.

Atambue tu kuwa toka Uhuru wa Tanzania mwaka 1961 Taifa letu halijawahi kuwa na mstakabali mbovu wa kisiasa na kidiplomasia ya Dunia kama kipindi hiki. Kitendo cha Paul Makonda kuzuiwa kwenda Marekani ni ujumbe tu kuwa kuna mengi yanafuata. Mojawapo ni hili hapa;

qz.com

The Trump administration has confirmed visa bans on four African countries, including Nigeria
"The administration’s expanded travel ban now affects close to a quarter of the population of the African continent."
qz.com
qz.com

Magufuli asijidanganye kuwa kwa vile huwa hasafiri nje ya Tanzania basi hayamhusu. Hapana, jina lake na la Kabudi, Mambosasa lipo tu kwa watu ambao hawatakiwi kwenda US, muda tu wa kutaja haujafika

Wamarekani wanazo details za udhaifu wa Serikali ya Magufuli ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu, ukosefu wa utawala wa sheria, utekaji wa wakosoaji, kubambikia watu kesi, mauaji na ukandamizaji wa demokrasia ya vyama vya upinzani.

Magufuli asijidanganye kuwa anaweza kufanya Tanzania anavyoyaka kama anavyofanya kwenye familia yake, hapana!! Utulivu wa Tanzania una masilahi makubwa kwa nchi za Magharibi hasa US, UK na Germany. Tanzania ikitulia maana yake eneo zima la maziwa makuu limetulia. Waganda walipochafuana miaka ya 1970s walikimbilia Tanzania, Warundi na Wanyarwanda walipochafuana miaka ya 1960s nao walikuja Tanzania. Kuanzia 1960 mpaka 1990s Tanzania ilikuwa Makao makuu ya vyama vya ukombozi vya Afrika kama SWAPO, MPLA, ANC, PAC na ZANU.
Hata Wakenya mwaka 2008 walipouana ni Tanzania iliyohusika kuwapatanisha.

Nchi za Magharibi haziwezi kukubali Magufuli na Makonda waharibu amani ya nchi hii. CCM hamujachelewa mtupeni huyu Magufuli kwenye bahrii kama Yona alivyotupwa alipokataa kwenda NINAWI ili chombo kiendelea na safari. Mkishindwa ataondolewa kwa nguvu na CCM itakuwa imekwisha kama iliyokwisha UNIP ya Kaunda au KANU ya Kenyatta. Uchaguzi ni wenu na muda munao, na uwezo munao pia.
 
Makonda aka Bashite hajawahi kufanya jambo bila kuacha alama...Haya ni machache tu ila yapo mengi sana aliyofanya ambayo yanakandamiza haki za binadamu na uhuru wa kuishi....Bashite anafanya hayo akikingiwa kifua na Baba Yake Meko na Mjomba wao Hi Now.

1.Bashite anahusika 100% kwa kuawawa kwa Ben Saanane.
2.Bashite anahusika 100% kwa shambulio la Lissu.
Mh! Itakuwa ishue ya kuyakamata mashoga, hivi kwani makonda ana nyumba marekani? Akae tu hapa akichoka dar anaenda mwanza kula satto
 
Hapana, hapo ni wale watuhumiwa wa ugaidi wengi wao kutoka mkiru, hakuna aliyepelekwa mahakamani, uwe na hatia au la ukikamatwa hauridi.
Duh! Hadi nasisimka, kuna watu kazi zao ni ngumu sana duniani, kazi ya kuuwa binadamu?
 
Sisi ni matajiri hata wasipoleta pesa za elimu alizozuia Zitto hatuna shida tunanunua ndege kwa cash, tunajenga SGR na Stigula goji kwa pesa zetu za ndani. Tumenunua korosho zote. Timezuia makinikia. Sisi ni dona kantri bwana tutembee vifua mberee
Mabeberu wanamuogopa jemedari wetu JPM amezuia mianya yao ya upigaji kupitia miradi yao ya hovyo huku na vibaraka wao..JPM anawanyoosha mabeberu sasa wameanza chokochoko..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaza tu! Hivi marehem Mwangosi na kuuwawa kinyama vile, angeua awamu hii ingekuwaje?
 
Back
Top Bottom