Bunge la Tanzania umekuwa muhimili mbovu na usio na tija wala faida kwa Taifa

Bunge la Tanzania umekuwa muhimili mbovu na usio na tija wala faida kwa Taifa

Tukiamua kama nchi wote tunakomaa tunakwenda pale tunaongea nao mpk waelewe na unaitishwa uchaguz mkuu kwa ajili ya kuchagua wabunge upya sio wanaokaa kuangalia nembo za taifa. Katb ya warioba ndio ilikuw mhogo mchungu kwao lakn wakaescape kiaina lakn xxa hv wabunge wengi wasingeweza kaliza miaka yao mitano kwny jimbo.
 
Bunge ni chombo ambacho kama kingekuwa kinafanya kazi yake ipasavyo hakika Tanzania ingekuwa mbali sana kwa sasa. Lakin Bunge la Tanzania ni miongoni mwa mabunge ya hovyo na hasara kwa Taifa, halina msaada wala mchango wowote ule kwa taifa hili.

Bunge linatia hasara Serikali kila mwaka. Bunge linakula posho bila michango chanya kwa taifa zaidi ya mipasho na malumbano ya kijinga. Kwa Tanzania bunge ni chombo cha kula posho tu na kupiga meza hakuna ambacho bunge linaweza kufanya chenye tija kwa taifa hili.

Bunge linaamuliwa mambo ya kufanya, Bunge haliwezi kujisimamia katika maamuzi yake lenyewe. Bunge halieleweki lina simamia nini, lipo kama ishara ya Bunge katika taifa. Maamuzi ya Bunge yanaweza kupindishwa hata na Mkuu wa Wilaya au Mkoa na ikiwezekana hata Mwenyekiti wa chama wilaya anaweza kulitunishia misuli Bunge.

Bunge la hivi la nini wakati halina faida kwenye nchi hata kwa 10%? Bora livunjwe pesa za posho na marupurupu mengine ziende kupeleka huduma kwa wananchi maana halina faida na halijui majukumu ya Bunge.

Si spika wa Bunge wala mwenyekiti wa Bunge, si Naibu wala Katibu na wabunge wote wanaojua umuhimu wa Bunge kuwepo.

Nasema hawajui tena hawajui wapo pale kula posho maana bado matatizo katika jamii yapo kwa kiwango kile kile kila mwaka mf.

1. Njia ni za msimu wa kiangazi tu masika hazipitiki na ni tangu uhuru

2. Maji bado shida sehemu kubwa ya nchi tangu uhuru

3. Umeme bado ni shida kwa wiki mnautumia siku tatu au nne tena kwa masaa

4. Huduma za afya na dawa bado shida palepale tangu uhuru

5. Elimu ndio kabisa ipo mahututi

Bunge linasema hivi na kuamua hivi lakini Serikali inafanya hivi na kuamua vile. Bunge hili la nini na linatumia pesa nyingi kujiendesha tena bila faida? Bunge lifutwe na lisiwepo kabisa, halina faida bunge hili.

Nawasilisha

Bunge letu lao(cccm) limekuwa halina tofauti na msikiti au kanisa, limekuwa ni sehemu ya kusikilisa mahubiri ya cccm, kupongeza, kusifia na kusifu...from parliament to church la mungu mtu.
 
nadhan swala la bunge kuonyeshwa live sio hoja hapa mkuu nadhan na wewe ni mbunge wa bunge la tanzania ndio maana unatoka nje ya mada maana nikawaida kwa wabunge hawa.
Tena atakuwa anatokea chama cha makenikia.
 
Kwa bunge hili bora lisiwepo linatumia fedha zetu bure na sioni faida yoyote. Wamefikia wanaongelea mambo ya wigi ktk nembo ya taifa! Kweli? akili nyingine bora kwenda kulima matembele.
 
Sasa kama spika wa Bunge ajui kwamba Bunge ni muhimili unajitegemea unategemea nini nikutokujitambua tu kwa watanzania Spika wa Bunge ajui kwamba Bunge linabidi lisimamie serikali yeye kutwa kucha najipendekeza kwa serikali sasa hivi serikali ndo inasimamia Bunge
 
Bunge mahakama siku hizi mihimili ikijitambua kwamba ni mihimili iliyokamilika aitakiwi kupelekeshwa na mtu au watu flani basi Tanzania tutakua tumejikomboa
 
Hiki chombo ni mhimili muhum sana katika serikali.

Tukianza na Serikali haina shida
Mahakama haina tatizo

Shida ipo bunge

1. Chombo kinachotumia pesa nyingi bila tija.
2. Wahuni hujikusanya pale na kutudanganya.
3. Sekta nyingi muhimu zinahitaji pesa jeshi la kisasa, kukuza uchumi na elimu na kiteknolojia.
4. Hawa darasa la saba wanatuchezea akili zetu kwa kulipwa mishahara na kutembelea magari ya gharama.
5. Bunge liwe na wawakilishi waliopo katika ofisi ya DC na RC na madiwani na wenye viti wa vitongoji na vijiji.
RC na DC wawe wanagombea na si uteuzi. Kamati za bunge zitokane na timu ya kuanzia mwalimu hadi ngazi ya RC representative's.
Bunge pamekuwa sehemu ya kupata fedha zenye dhulma.

  1. Utalipajwe 10mil+?
  2. Who are you?
  3. Je Dr hana thamani?
  4. Mwl hana thamani?
Why
  • Bunge ni sehem ya kujitwalia pesa za burebure
  • Bunge pamekuwa na kupotezea wkt na hoja kichovu.

NB watakaokuwa wawakilishi wabunge wawe na elimu ya chuo na sio la saba.

Naomba kutoa hoja.
 
Hiki chombo ni mhimili muhum sana katika serikali.

Tukianza na Serikali haina shida
Mahakama haina tatizo

Shida ipo bunge

1. Chombo kinachotumia pesa nyingi bila tija.
2. Wahuni hujikusanya pale na kutudanganya.
3. Sekta nyingi muhimu zinahitaji pesa jeshi la kisasa, kukuza uchumi na elimu na kiteknolojia.
4. Hawa darasa la saba wanatuchezea akili zetu kwa kulipwa mishahara na kutembelea magari ya gharama.
5. Bunge liwe na wawakilishi waliopo katika ofisi ya DC na RC na madiwani na wenye viti wa vitongoji na vijiji.
RC na DC wawe wanagombea na si uteuzi. Kamati za bunge zitokane na timu ya kuanzia mwalimu hadi ngazi ya RC representative's.


Why
Bunge ni sehem ya kujitwalia pesa za burebure

Bunge pamekuwa na kupotezea wkt na hoja kichovu.

NB watakaokuwa wawakilishi wabunge wawe na elimu ya chuo na sio la saba.

Naomba kutoa hoja.
Humo bungeni la saba wapo wangapi!?
Mawaziri karibu wote wana masters na phd ukitoa nape 4m4 failure.
Waziri wa fedha na phd yake amefanya nini!?
Mtikila alisema tunawasomi wapumbavu(foolish)
 
Uwakilishi haihitaji elimu kubwa Kwa sababu jamii Kuna ambao hawana elimu ni wengi.pia kujua changamoto za kwenye jamii Yako hakuhitaji elimu ya PhD.Lakini Kwa aina ya bunge letu lilivyo hata likifutwa hakuna tatizo kabisa Kwa sababu
1.Bunge letu halina watu jasiri wakuhoji na kusimamia mapungufu ya serikali.bunge letu kibogoyo limekuwa la ndiyooooo.chochote kinacholetwa na serikali wao wanakubali hata kama Cha kipuuzi.Bunge limeshiriki kuuzwa Kwa bandari zetu,gesi ya mtwara,wamasai wamefukuzwa,wamepitisha tozo za simu Huku wao wakidai waongezwe mshahara kufikia milioni18 Kwa mwezi.Bunge la tz lifutwe.
 
Rekebisha heading hio,,nikajua bunge lifanyiwe partition
 
Back
Top Bottom