Bunge la Ulaya: Hii ni bahati mbaya au ni malengo maalum?


Mkuu hapa umenena ....

Ngoja tumsubiri mkuu Mkuu wa chuo aje atoe ufafanuzi!
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli unachokisema maana hata kwa sasa hiyo roho ya mpinga kristo ipo na inatenda kazi, lakini kufunuliwa kwake ni bado kwani baadhi ya mambo hayatokea bado, kama tunavyoona katika Danieli 9:27 agano bado hajaweka...

1 Yohana 2:18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
 

Sasa hapa mkuu naona kuna concept mpya.

Wewe na Mkuu wa chuo mnaamini hivi
● Daniel 9:26 kwamba huyo mkuu hajaja bado na atakuja baadae

Ila kuna jambo Mkuu wa chuo alisema limetimia kwamba Kuharibiwa kwa mahali Patakatifu pameshatimia mwaka 70AD....

Sasa kama hao watu wa mkuu atakayekuja walishafanya hayo inakuwaje tena Kuna watu wewe unawazungumza hapa kwamba wanatayarisha kumkaribisha huyo mpinga kristo
 
Wajinga ndio waliwao.

Hizo picha zinafanana? au hujuwi maana ya kufanana?

Na huyo ndio mnyama mwenye mapembe kumi?

e
Upunguani mwingine ni wa hali ya juu.
kwa mara ya kwanza nimekuunga mkono,hizo pembe kumi sizioni wala hayo majengo hayafanani,pale nairobi kuna jengo laduara pia basi nalo tusemeje
 


Basi Aliyefanya Ya kwenye Daniel 9:26 ni Mpinga Kristo mwingine ambaye si huyu anayekuja mwishoni

Na kama Unakataa kwamba 70AD haikulenga hilo utakuwa Tofauti kimtazamo na Mkuu wa chuo. . Na Daniel 9:26 haijatimia yote kabisa
 
kwa mara ya kwanza nimekuunga mkono,hizo pembe kumi sizioni wala hayo majengo hayafanani,pale nairobi kuna jengo laduara pia basi nalo tusemeje

Ndo maana hatujaconclude kabisa.. Tatizo tunajiuliza kwanini zina Biblical View.. ? Na kwanini wajenge jambo ambalo linaonekana limetabiriwa kwenye Biblia. .

Hata kama pembe hizo hazipo ila kuna Mnyama mwenye pembe mbili na yupo Mwanamke anayembeba mnyama mwingine mwenye pembe kumi
 
nimependa mjadara.imenibidi nijikusanye kwanza kabla sijatoa maoni yangu maana nimejifunza humu kutoa maoni bila evidence ni sawa na upotoshaji
 
uyo atakuwa allah subhaanau tu mpinga kristo unaonaje jembe

Ok Tatizo ni Evidence na sifa za Mpinga Kristo ziendane na hayo unayonena..

Mpinga Kristo hata Wewe unaweza ukawa ila Tatizo unazo kwa asilimia 100%

Mfano Mpinga kristo ni yule anayemkana Mwana Wa Mungu kwahiyo kama Hiyo ipo Basi Huyo ni Mpinga Kristo. ...
 
Mi nadhani hapa hujapaelewa vizuri.. inakuwaje watu wanakuja kuangamiza mji bila kuwa na Kiongozi wao.. ?

Mfano

Jeshi haliwezi kuvamia sehemu bila kuwa na amri kutoka kwa Raisi. Na Raisi ndo anayezungumziwa hapo kwamba ndiye mkuu
Mtawala wa kipindi hicho wakati Warumi wanauangamiza mji alikuwa ni Tito, Lakini pia kama umeenda kule chini ukaangalia ule uchambuzi kuhusiana na yale majuma 70, ina maana na hayo yaliyokuwa yakifanyika ila ni baada ya majuma 69 na juma la 70 lilikuwa bado halijaingia, ndio maana nasema kuna gap kati ya juma la 69 na 70, kwa sababu kama ukisema ni Tito hajaweza kutimiza kuhusiana na lile fungu la 27 la Daniel, na hilo ndio juma moja la kwa Daniel lililobakia na Ufunuo ile ina base kwenye hiyo miaka 7 ya Daniel iliyobaki...

Fungu la 27 linahusiana na mpinga kristo...


Fungu la 27 linaelezea kweli yamkini huyo mtu atatokana na Rumi, au pia Rumi inaweza ikawakilisha mataifa, Jaribu kusoma Mathayo 24, Yesu pia alitabiri hicho kitu cha kuharibiwa mji lakini baadae alikuja kuelezea chukizo la uharibifu

Pia unaweza ukaangalia Luka 21:20 na kuendelea...
Kama unakumbuka ulisema kuwa Antious alikamilisha kusimamisha Sanamu zake mule ndani ya hekalu na ukasema kuwa

Ila hapa Tena naona nachanganyikiwa kwa weww tena kusema kuwa Mpinga Kristo anakuja na bado hayajatimia

Antiochus Epiphanes alifanya hivyo ila hakubomoa hekalu alifanya hiyo Chukizo la Uharibifu katika enzi zile za kina Makabayo, Lakini huyu jamaa atakayekuja ataweka agano tena halafu chukizo la uharibifu litasimama...
Hayo ni mambo yaliyokuwa yanaelezewa baada ya yale majuma 69 ya Daniel kutimia, ila lile juma la 70 bado halijatimia hadi sasa, hadi mwaka 90 AD hayo ya Daniel 9:27 hayakutokea, ndio maana kunakuwa na ile miaka saba ya dhiki ndio ile miaka ya juma la 70 la kwa Daniel...
 
Ngojea nikuwekee Kiswahili cha kisasa upate concept, halafu pale nitakapopigia mstari ndio utaelewa

Daniel 9:26 Baada ya majuma hayo sitini na mawili, yule aliyepakwa mafuta atakatiliwa mbali hatabaki na kitu. [SUP]m [/SUP]Mji na mahali patakatifu kabisa vitaharibiwa na jeshi la mtawala atakayekuja kushambulia. Mwisho wake utafika kama mafuriko, kukiwa na vita na maangamizi kama yalivyopangwa na Mungu.

Zingatia hapo nilipopiga mstari...
 
Muhammad and Allah are both Anti Christ. According to the Qur'an, the Bible contains prophecies about Muhammad (see Qur'an 7:157; 61:6). Yet, when we open the Bible, we find that Muhammad is condemned as an antichrist (1 John 2:22-23)! Muslims try to ignore this by claiming that the Bible has been corrupted. But if the Bible has been corrupted, why did Muhammad say that we should go to it to find prophecies about him? If the Bible has been corrupted, why does Allah say that no one can change his words (6:115; 18:27)? If the Bible has been corrupted, why does Allah command Jews and Christians to judge by the Torah and the Gospel (5:43-47)?
 

Quran 7-157
َ

Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.

Quran 61-6
ٌ

Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!

Haya tuoneshe wapi amempinga Yesu...
 

hapo ninaweza nikakujibu roho ya mpinga kristo inatenda kazi, kwa hiyo Automatically wale walioharibu waliongozwa na hiyo roho, kwa hiyo wanaweza wakawa wanaitwa watu wa mkuu kwa muktadha huo...

Na kama unavyojuwa joka ambaye ni shetani atampa mamlaka mnyama, kwa hiyo hao watu pia waliongozwa na hiyo roho ndio waka tenda hivyo ni kama vile Shetani alivyoweza kumuingia Yuda Iskariote

kama kule chini kwenye jukwaa la dini umeweza kuyasoma yale majuma 69 kwenye ule uzi moja kwa moja, utaweza kupata concept...
 

Sasa Mkuu wa chuo huoni hilo tukio la kuharibiwa ni baada ya Yesu kukataliwa ndo linatokea?

Na wewe tayari ushasema lilitimia au umebadili mawazo sa hivi...
 
Last edited by a moderator:

Hili nafikiri tayari nimekwisha lijibu hapo juu, nimekwambia kwamba kuna gap yaani kama kuna pause fulani, matukio ambayo yalihaidiwa katika majuma 69 yamekwisha timizwa baada ya kukamilika hayo majuma 69 baada ya muda ndio ikaja kule kuharibiwa kwa mji mwaka 70 AD ambayo hapo juma la 70 lilikuwa bado halijaanza, na juma la 70 hadi kwa sasa halijatimia maana hatujaona mpinga kristo akiweka agano kama inavyoelezewa na fungu la Daniel 9:27

Cha kujiuliza ni kwanini waliitwa watu wa mkuu!? hapo juu nimekupa concept na Daniel 9:27 inalezea habari za mpinga kristo

Na katika Yohana 5:43, Yesu anawaambia Wayahudi yeye alikuja kwa jina la Baba yake wakamkataa ila kuna ambae atakuja kwa jina lake mwenyewe watamkubali huyo, kwa hiyo Mpinga kristo kwa lugha nyingine anatambulika kama Masihi wa uongo ambaye atakapokuja Wayahudi watamkubali, ndio atafanya agano nao kwa muda wa juma moja yaani miaka 7, na katikati ya juma atavunja agano ndipo chukizo la uharibifu litakaposimama, ndio hilo fungu la Daniel 9:27 linaeleza hivyo, kwa hiyo bado hilo fungu la 27 halijatimizwa yaani lile juma la 70 bado, angalia hiyo Yohana 5:43

Yohana 5:43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
 

Okay sawa mkuu, itabidi pia nizame kwenye hiyo concept ila nimeshaipitia kwa juu juu itabidi nije nizame zaidi...

Ni kweli Elimu Haina mwisho...

Shukrani sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…