Bunge la Ulaya: Hii ni bahati mbaya au ni malengo maalum?


Rumi ipo kwa maana hizo Falme kulingana na wale Wanyama au tukirudi katika ile mfuatano wa ile sanamu ina maana zilikuwa zikienda kwa kupokezana na historia inaonyesha baada ya Ugiriki ilifuatia Rumi, na kipindi cha Yesu Rumi ndio iliyokuwa ikitawala... kwa hiyo sifa kubwa ilikuwa ni ile trend ya mfuatano wa zile Falme ndio maana huwezi iweka Ottoman hapo au Falme nyingine...
 
Mkuu mbona una madini hivi halafu kule kwenye ule uzi chini sikuoni sana!?
 

Mkuu,si zamani sana,ni miaka ya 90's tu sikuwahi kufikiri kuwa kuna siku kanisa litasimika askofu shoga,leo hii vipi?sikuwahi kufikiri kuna siku nitasikia nchi ya kiafrika ikiwekewa vikwazo kwa kukataa ushoga.Leo hii vipi?Sikuwahi kufikiri,kuna siku nitakuwa na mijadala mingi kumshawishi mtu aamini uwepo wa Mungu kama humu jf.Leo hii vipi?Sikuwahi kufikiri kuna siku ntashuhudia haya nishuhudiayo middle east,africa,n.k mauaji,vita,njaa,magonjwa.Sikuwahi kufikiri wala kuamini kuwa ipo siku ntashuhudia mmomonyoko wa maadili kwenye jamii kama leo hii.Mwaka jana nilikuwa na project fulani iliyonikutanisha na vijana wengi teenagers from 14 to 19.Mkuu,hali inatisha.sijui hawa wakifika umri wetu kuiendesha hii dunia hali itakuwaje.Juzi tu nilialikwa semina fulani ya wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali,mada mojawapo ni kuwafundisha kuvumiliana na kuheshimu watu wote,including gays.Na umeipata kashfa iliyotokea kwa makasisi wakatoliki ulaya na Marekani.Maana yake jamii imeoza to the core,wala hatapata shida huyo atakayeamua kuyaweka rasmi hadharani haya maovu.Kizazi nikionacho huku chini,ni kizazi cha mpinga kristo,nazungumza hili kwa ujasiri kabisa tena hapa hadharani mkuu.Hata hivyo,ukitazama ule Ufunuo wa 666,kwamba hakuna kununua wala kuuza,do you really think itakuwa mazingira ya usiri kweli?!
 

Mkuu,haya mambo nashindwa kuyaelewa kwa kiasi ambacho nyie mnayaelewa

Ni kwanini Danieli aliona wanyama wawili tu ambao waliwakilisha falme mbili tu kama Rumi ilikuwa na umuhimu ambao tunauona hapa?

Kitu kingine ambacho kinanishangaza ni kuwa,Danieli aliona falme ambazo zilikuja kutawala na aliambiwa kuwa hayo ni ya wakati wa mwisho [Danieli 8] kweli kabisa mkuu iliwezekanaje kushindwa kuona mnyama aliyeiwakilisha Rumi hapo kwenye Danieli 8?

Mkuu sijui ni kwanini hili linanisumbua sana kichwani,lakini huenda kuna sababu ...!!
 

Umeongea mambo ya maana sana na nikiyakataa nitakuwa sina maana......

Pamoja na hayo kama ni hivyo wewe unadhani itachukua muda gani hadi tufikie kwenye kilele kabisa?
 
Umeongea mambo ya maana sana na nikiyakataa nitakuwa sina maana......

Pamoja na hayo kama ni hivyo wewe unadhani itachukua muda gani hadi tufikie kwenye kilele kabisa?

Turudi kwenye imani yetu mie na wewe,wafuasi wa Bwana Yesu.Alituambiaje?kwa mtini jifunzeni...maana yake tutazame ishara ambazo unabii umetuachia.Ni kosa la jinai kutumia muda ili kujua unabii wa biblia unless bible yenyewe imetaka hivyo.Hivyo tuitazame dunia,tuwe wachunguzi tukioanisha mambo na unabii ili kuona kama ishara tulizoambiwa zinaonekana.Ndio maana ni muhimu kujua tafsiri sahihi ya Neno la Mungu.Kwa mfano eiyer,hivi chukizo la uharibifu ni kitu gani?mkuu wa chuo,unaelewaje hiyo kitu,abomination of desolation?
 

Mkuu chukizo la uharibifu hapo naona ni lile ambalo limenenwa na nabii Danieli

Kama ni hivyo basi,hapa hadi hekalu lijengwe tena ....
Mkuu wa chuo ...!!
 
Last edited by a moderator:

Unawajua Vizuri hao jamaa??
 
Labda nikuulize pia,Mwanamke ni nini katika unabii wa biblia?kwa nini alitumika mwanamke pale juu ya mnyama mwekundu?

Nadhani tafsiri ya Mwanamke aliitoa malaika mwenyewe kwamba ni MJI MKUU kwenye Ufunuo 17
 

Chukizo la uharibifu ni kile kitendo cha Mpinga kristo kukaa ndani ya Hekalu la Mungu na kufanya yale mambo yake...

2 Wathesalonike 2:4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
 
Mkuu mbona una madini hivi halafu kule kwenye ule uzi chini sikuoni sana!?

Mkuu,kile kichwa cha habari kinanipa shida.Halafu nimekumbuka swali kila siku nataka kuwauliza wakuu,hivi mpinga kristo ni nani,ni yule mnyama aliyebeba mwanamke,au mwanamke aliyebebwa?je,kuna connection kati ya mnyama yule no 666 anayewapiga chapa watu na huyu aliyebeba mwanamke pamoja na mwanamke mwenyewe?
 
Mkuu chukizo la uharibifu hapo naona ni lile ambalo limenenwa na nabii Danieli

Kama ni hivyo basi,hapa hadi hekalu lijengwe tena ....
Mkuu wa chuo ...!!
Halafu chukizo la uharibifu ni baada ya mpinga kristo kufanya agano na Wayahudi, kwa juma moja yaani ile miaka saba kati kati ya juma atavunja agano ndipo chukizo la uharibifu litakaposimama

Chukizo la uharibifu ni msemo wa Kiyahudi una maana ya kukufuru au kunajisi patakatifu pa hekalu...
 

Ok.niliuliza purposely kwa sababu hilo tukio ni one of the signs.nadhani wakuu iko haja kuweka mlolongo au timeline ya matukio makuu ambayo unabii umeyaeleza kama ishara ya kuelekea ule mwisho
 

Yeah ni Yule mnyama aliyebeba mwanamke ndio mpinga kristo mwenye vichwa saba na pembe kumi, kile kichwa cha habari kisikuogopeshe mkuu... Yeah connection ipo, yule mnyama anaye sababisha watu kupigwa namba 666 ni nabii wa uongo, ukienda Ufunuo 13 imeelezwa vizuri, Mwanamke yule ni Kahaba, kwenye paji la uso wake kuna BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA huyo mwanamke pia anaweza akawa anawakilisha system fulani hivi ya dini mfano wa Babeli, pia huyo mwanamke ni mji, nikikaa vyema ninaweza kuja kuichambua Ufunuo 17 kule chini...
 
Nipo makini kufatilia hatua kwa hatua
lakini kuna mdau kasema Mungu hana dini,hili linanipa wakati mgumu kuamini.
Binafs Kupitia maandiko matakatifu naona kabisa kupitia nabii Musa,kupitia Yesu kirsto na manabii wengine Mungu alijitambulisha vyema kwa mwanadamu,
Yesu kirsto alikuja kuingunisha mwanadamu aliyejitenga na MUNGU
NIPO TAYARI KUKOSOLEWA
ila naamini kabisa kuputia agano la kale na agano jipya,Mungu katuelekeza dini ya kufuata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…