Bunge la Ulaya laitaka Tume kufuta Ufadhili wa Mwaka 2026 kwa Tanzania

Bunge la Ulaya laitaka Tume kufuta Ufadhili wa Mwaka 2026 kwa Tanzania

Haya mambo ya kumsikiliza Kabudi na Kombo yataleta shida...

Hivi Serikali haijui kwamba haya makelele huko Ulaya yanapunguza kuaminika kwa Serikali...

Inapunguza investment za watu wa Ulaya kuja Tanzania

Tunaonekana hatuna ustaarabu kama binadamu..

Kuna Doctor mmoja yupo Ocean Road..kaniambia alienda ubalozi wa EU akiwa na hofu ili wasisitishe misaada ya dawa za cancer..bahati nzuri akajibiwa hizo dawa zitaletwa kama kawaida maana zinahusisha jamii

Dawa za cancer ni bei mbaya..EU wanatoa dawa na vifaa tiba kwa mwaka inazidi billion 50... Na sisi tunajidai kukimbilia Urusi...

Hawa EU wanataka tuheshimu haki za binadamu....sisi tunajibu eti ni utamaduni wetu ..mara wasituingilie...
Sasa kwanini tunawaomba Hela kama hatutaki wasituingilie?
 
Machawa ya Mbogamboga hayajui haya
 
Hizi sasa ndo akili?
Mpk sasa hujui kuwa mishahara na posho za Samia na genge lake kupitia kodi yako itaendelea kama kawaida lkn kijijini kwenu watateseka?
Maisha yatakua Magumu mpaka kwa kwenye vyombo vya Ulinzi na utakuja kusiku Askari kaacha kazi serikalini kaenda Kuwa Mlinzi Namibia au South Africa, Na Wananchi wakizdi kuteseka ndiyo mwanzo wa CCM kuanguka
 
Kwahiyo wewe tahira kukosa misaada ambayo miaka kwa miaka tuliipokea lakini haijatusaidia unaona ni tatizo?
Tanzania itasimama imara zaidi ya jana. Tuna basement tatu duniani.
Basement moja ikigoma mbili zitakuwa upande wetu.
Mbona waziri wa wizara husika juzi kawachana uwazi hao wazungu.
Sisi sio koloni la Taifa lolote, tuna rasilimali nyingi zinapendwa na mataifa mengi. Watakuja kama wafanyabiashara na tutadeal nao kama wafanyabiashara
Ona huyu, unasema tulikuwa tunapokea misaada na haijatusaidia kwahiyo ukiikosa ndio utaendelea.
 
Hawa jamaa wanaotuongoza ni muda wa kujitathmini sasa.

Huku serikali za maghaibi zinatulima barua za maonyo,kisha vikwazo,

Raia kupiga kelele kuhusu mifumo ya usalama inavyowakandamiza,

Gen Z wanawasha moto Kila kukicha. Sasa hivi Dar imekuwa kama Sudan Kila barabara na roundabout askari wamejaa Huku wamejikoki na silaha nzito na mabomu ya machozi vifuani,

Bandari road wamewatoa bodaboda wote kwenye vijiwe vyao walivyokuwa wanajitafutia riziki. Wenye Private cars wanaoishi kigamboni wanapitakwa ugumu hadi wakuscan utadhani tupo mpakani wa mexico na U.S. kumbe tupo Tz. Hatukuwahi kuona hii hali.

Ni kama jamaa wapo katika panic mode.

Kila kukicha viongozi wanapiga mikwara kuhusu wanaotukana viongozi wa serikali,

Msigwa kila kukicha yeye ni kuwatisha waandishi wa habari kuwa siyo wazalendo na wanaovujisga siri za serikali "wataokotwa"

Kafa Mbunge bwege Kila mmoja ametoa pole hakuna matusi Wala kashfa ila akifa kiongozi wa sisiem hata awe mjumbe wa nyumba kumi,taarifa ikifika mtandaoni sisiem wote wanaoga matusi ya nguoni hukunwatu wakishukuru Mungu kwa "kidogo" huku wanaombea wafe viongozi wazito kule juu

Ila ajabu wanasema Hawa ni watu wachache wanaopiga kelele wakiwa nje ya nchi.

Sijui lini waamtaacha kujidanganya na kuamua kubadilisha mwelekeo wa hii nchi!

Au mpaka vikwazo vituchakaze? Ile kenge hasikii hadi atoke damu kwa msikio?
Yule bi mkubwa akidondoka au jk watu watafurahi sana. Sijui wanawezaje kuishi huku wakichukiwa kiasi hiki.
 
Hizi sasa ndo akili?
Mpk sasa hujui kuwa mishahara na posho za Samia na genge lake kupitia kodi yako itaendelea kama kawaida lkn kijijini kwenu watateseka?
Hujui kitu, wewe unaangalia mshahara wa Samia tu hufikirii mishahara ya wanajeshi, polisi, watumishi wa umma, miradi, poor and narrow thinking.
 
Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.

Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.

Soma, Pia

View attachment 3610467View attachment 3610466
Chande alisema waliouawa ni 500+
Hawa wazungu mnaowaamini wanasema watu 400. Na hakuna lofa yoyote anayelalamikia idadi ndogo.
Waafrika ni wassengee
 
Hujui kitu, wewe unaangalia mshahara wa Samia tu hufikirii mishahara ya wanajeshi, polisi, watumishi wa umma, miradi, poor and narrow thinking.
Wewe ndo hujitambui. Kama kuathirika basi kwanza ni miradi na kuzorota kwa huduma za kijamii wakati Samia na genge lake wataendelea kulamba kodi yako mpk wao waathirike basi kijijini kwenu hakutokuwa na barabara wala maji
 
Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.

Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.

Soma, Pia

View attachment 3610467View attachment 3610466
Ukisikia kupigwa mbele na nyuma ndio huku
 
Maisha yatakua Magumu mpaka kwa kwenye vyombo vya Ulinzi na utakuja kusiku Askari kaacha kazi serikalini kaenda Kuwa Mlinzi Namibia au South Africa, Na Wananchi wakizdi kuteseka ndiyo mwanzo wa CCM kuanguka
Ni kweli kabisa. Mpk ifikie Samia na genge lake kuumia basi huko vijijini kutakuwa taabani kiasi tutahitaji miaka 50 kukaa sawa. Hapo Samia na genge lake hawatokuwepo tena duniani kwa umri wao. So msoto utakuwa kwa gen Z wanaoshabikia leo
 
Huo muarobaini wote tutaunywa hautachagua CCM au wapinzani.
Hiyo ndo inaitwa Husda. Yaani Hasidi anaumia sana kuona mwenzio anafaidi japo yeye anaambulia kidogo. So yupo tayari apoteze hata kidogo hicho provided aliyenacho naye atapoteza
 
Back
Top Bottom