Bunge la Ulaya laitaka Tume kufuta Ufadhili wa Mwaka 2026 kwa Tanzania

Bunge la Ulaya laitaka Tume kufuta Ufadhili wa Mwaka 2026 kwa Tanzania

Hiyo ndo inaitwa Husda. Yaani Hasidi anaumia sana kuona mwenzio anafaidi japo yeye anaambulia kidogo. So yupo tayari apoteze hata kidogo hicho provided aliyenacho naye atapoteza
Lini Msigwa atatoa ufafanuzi siku ile alisema bado kuna hatua hazijaisha.
 
Nawaza tu,ingawa chadema watafurahi kiasi cha hata kunywa bia baridi, lakini nimetafakari sana,je?
*Tukipandisha bei ya unity ya umeme wa majumbani,
*Tukapandisha bundle za internet
*Tukapunguza safari za nje kwa watumishi
*Tukapunguza vikao na posho mbalimbali,
*Magari mengi /yote ya umma yakawa ya nishati ya umeme
*Tukaweka kodi ya kichwa,ya 10000 kwa mwaka,
*Ruzuku zikaondolewa kwa vyama vya siasa
HAPO VIPI?
Kama haya yatafanyika ni furaha zaidi kwa hao chadema unaowahofia maana yataongeza ugumu wa maisha maradufu jambo ambalo litawarahisishia chadema kuwaunganisha wananchi kuishambulia serikali hata kwa maandamano yenye ufanisi wa haraka.
 
Hizi sasa ndo akili?
Mpk sasa hujui kuwa mishahara na posho za Samia na genge lake kupitia kodi yako itaendelea kama kawaida lkn kijijini kwenu watateseka?
elewa kwamba wananchi kuwa na hali ngumu ni reflection ya kipi kinaendelea ndani ya serikali..

kodi za wananchi zinachangia pakubwa sana katika uendeshaji wa serikali...

ndani ya serikali kutakuwa na hali ngumu vilevile, zile posho za kila wakati zitakoma, na hapo ndipo uchawa utakoma... Hali hio ikiendelea sote tunajua nini kitatokea...
 
Hawa jamaa wanaotuongoza ni muda wa kujitathmini sasa.

Huku serikali za maghaibi zinatulima barua za maonyo,kisha vikwazo,

Raia kupiga kelele kuhusu mifumo ya usalama inavyowakandamiza,

Gen Z wanawasha moto Kila kukicha. Sasa hivi Dar imekuwa kama Sudan Kila barabara na roundabout askari wamejaa Huku wamejikoki na silaha nzito na mabomu ya machozi vifuani,

Bandari road wamewatoa bodaboda wote kwenye vijiwe vyao walivyokuwa wanajitafutia riziki. Wenye Private cars wanaoishi kigamboni wanapitakwa ugumu hadi wakuscan utadhani tupo mpakani wa mexico na U.S. kumbe tupo Tz. Hatukuwahi kuona hii hali.

Ni kama jamaa wapo katika panic mode.

Kila kukicha viongozi wanapiga mikwara kuhusu wanaotukana viongozi wa serikali,

Msigwa kila kukicha yeye ni kuwatisha waandishi wa habari kuwa siyo wazalendo na wanaovujisga siri za serikali "wataokotwa"

Kafa Mbunge bwege Kila mmoja ametoa pole hakuna matusi Wala kashfa ila akifa kiongozi wa sisiem hata awe mjumbe wa nyumba kumi,taarifa ikifika mtandaoni sisiem wote wanaoga matusi ya nguoni hukunwatu wakishukuru Mungu kwa "kidogo" huku wanaombea wafe viongozi wazito kule juu

Ila ajabu wanasema Hawa ni watu wachache wanaopiga kelele wakiwa nje ya nchi.

Sijui lini waamtaacha kujidanganya na kuamua kubadilisha mwelekeo wa hii nchi!

Au mpaka vikwazo vituchakaze? Ile kenge hasikii hadi atoke damu kwa msikio?
Hatutaki kujifunza na kukataa mabaya tuliyofanya, mtu anayekataa kutubu na kuleta ubabe usio na maana matokeo yake ndio hayo
 
elewa kwamba wananchi kuwa na hali ngumu ni reflection ya kipi kinaendelea ndani ya serikali..

kodi za wananchi zinachangia pakubwa sana katika uendeshaji wa serikali...

ndani ya serikali kutakuwa na hali ngumu vilevile, zile posho za kila wakati zitakoma, na hapo ndipo uchawa utakoma... Hali hio ikiendelea sote tunajua nini kitatokea...
Kweli, pesa za kuwalipa machawa hazitakuwepo na wote tutarudi kuongea lugha moja
 
Tumieni wataalamu wenu kuunda mifumo yenu.
Si mnapeleka watoto vyuoni wakasome kozi za sayansi, kwanni hamuwatumii au hamuwaamini?
Tungekuwa na uwezo huo tungeshaunda mengi, mbaya zaidi tuwagemea watupe hiyo elimu huku tunawatukana.
 
Back
Top Bottom