Bunge la Ulaya laitaka Tume kufuta Ufadhili wa Mwaka 2026 kwa Tanzania

Tungekuwa na uwezo huo tungeshaunda mengi, mbaya zaidi tuwagemea watupe hiyo elimu huku tunawatukana.
Kwa hiyo unakiri kwamba vijana walipo vyuoni kama pale DIT au COET , Udsm hawana msaada wowote kwa jamii ya kitanzania?
 
Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.

Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.

Soma, Pia

View attachment 3610467View attachment 3610466
ERoni hilo ni jambo la kawaida sana na haliwezi kuibabisha Tanzania kwa namna yoyote ile.

Msaada ni wa kwao, na wana hiyari ya kuifadhili nchi yoyote duniani kadiri wanavyoona inafaa.

Kama taifa,
tupo vizuri sana na tumejipanga mbaya sana kisiasa, kijamii na kiuchumi, na hakuna taifa au jumuiya yoyote duniani inaweza kueilekeza au kuishinikiza Tanzania jinsi ya kuendesha mambo yake ya ndani na namna ya kuwatumikia wananchi wote wa Tanzania, eti kwasababu wanatoa msaada. That's useless..

Ni vizuri misaada na ufadhili wao, ikapelekwa kuwasadia watu maskikini na waliotengwa Ulaya, kuliko kujitia kimbelembele kusaidia Tanzania hali ya kua kuna nia ovu nyuma ya misaada hiyo.

Tanzania is becoming more powerful, united and more stronger than before economically, politically and socially 🐒
 
Hawa jamaa wanaotuongoza ni muda wa kujitathmini sasa.

Huku serikali za maghaibi zinatulima barua za maonyo,kisha vikwazo,

Raia kupiga kelele kuhusu mifumo ya usalama inavyowakandamiza,

Gen Z wanawasha moto Kila kukicha. Sasa hivi Dar imekuwa kama Sudan Kila barabara na roundabout askari wamejaa Huku wamejikoki na silaha nzito na mabomu ya machozi vifuani,

Bandari road wamewatoa bodaboda wote kwenye vijiwe vyao walivyokuwa wanajitafutia riziki. Wenye Private cars wanaoishi kigamboni wanapitakwa ugumu hadi wakuscan utadhani tupo mpakani wa mexico na U.S. kumbe tupo Tz. Hatukuwahi kuona hii hali.

Ni kama jamaa wapo katika panic mode.

Kila kukicha viongozi wanapiga mikwara kuhusu wanaotukana viongozi wa serikali,

Msigwa kila kukicha yeye ni kuwatisha waandishi wa habari kuwa siyo wazalendo na wanaovujisga siri za serikali "wataokotwa"

Kafa Mbunge bwege Kila mmoja ametoa pole hakuna matusi Wala kashfa ila akifa kiongozi wa sisiem hata awe mjumbe wa nyumba kumi,taarifa ikifika mtandaoni sisiem wote wanaoga matusi ya nguoni hukunwatu wakishukuru Mungu kwa "kidogo" huku wanaombea wafe viongozi wazito kule juu

Ila ajabu wanasema Hawa ni watu wachache wanaopiga kelele wakiwa nje ya nchi.

Sijui lini waamtaacha kujidanganya na kuamua kubadilisha mwelekeo wa hii nchi!

Au mpaka vikwazo vituchakaze? Ile kenge hasikii hadi atoke damu kwa msikio?
acha porojo na upotoshaji useless namna hiyo gentleman 🐒
 
Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.

Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.

Soma, Pia

View attachment 3610467View attachment 3610466
Unakuaje Rais hata kiti chenyewe hukifurahii
 
Hiyo ndo inaitwa Husda. Yaani Hasidi anaumia sana kuona mwenzio anafaidi japo yeye anaambulia kidogo. So yupo tayari apoteze hata kidogo hicho provided aliyenacho naye atapoteza
Akili yako ndogo unafikiria tumbo lako tu sisi tunafikiria kuikomboa nchi toka midomoni mwa familia zisizozidi 20 against Watanganyika zaidi ya 65milioni wewe unashabikia kakikundi ambacho wewe huna hata sehemu unabaki kuwa mpenzi mtazamaji, think big !!!
 
Mjifunze kujitegemea.
Mmezoea kupokea misaada hadi inafika kipindi mnahisi ni haki zenu kikatiba.
Wa kujifunza kujitegemea ni serikali za kipuuzi zinazoongoza hizi nchi za kimaskini ambazo toka raisi mpaka mwananchi wa kawaida hawajui kwanini wapo duniani.
 
Sasa kama wanaopata shida ni serikali.
Iweje watu wa kawaida wanaitaka serikali iige misingi ya demokrasi ili wazungu walete misaqda ?
 
Atakaeumia ni bibi yako na babu yako huko kijijini wewe mpuuzi unaeshabikia, bi Wanu, Mr Abdul wanaendelea kula kuku kwa mrija
Bibi na babu hawumii kwa vikwazo kwa sababu wao wanategemea mashamba yaliyo upenuni mwa nyumba zao. Wanaoumia ni hao wanaojenga hoja kwamba hajatokea Rais aliyefanya maendeleo nchi hii kama Samia.
 
Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.

Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.

Soma, Pia

View attachment 3610467View attachment 3610466
 
Attachments

  • downloadfile(41).jpg
    downloadfile(41).jpg
    61.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom