Karungikana
JF-Expert Member
- Jan 8, 2017
- 913
- 844
Naunga mkono hoja. Kila kiongozi awe na ndege yake ya kumhudumia.
Bunge la Tanzania limeazimia kuwa Serikali iangalie umuhimu wa kununua ndege nyingine mpya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi wakuu wa kitaifa.
Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Joseph Mhagama, ambaye ameeleza kuwa nia ya azimio hilo inatokana na Wakala wa Ndege za Serikali kushindwa kuwahudumia kwa wakati viongozi wakuu pale zinapotokea safari kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa Mhagama kamati yake imebaini kuwa kwa sasa kuna ndege tatu zinazowahudumia viongozi wa Serikali. Ndege moja inamhudumia Rais wa Tanzania, ndege nyingine mbili zinawahudumia Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Kwanza na Wa Pili wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa kitaifa.
“Hali hii husababisha Wakala [wa Ndege za Serikali] kutekeleza jukumu la kuwahudumia viongozi kwa kuchelewa pindi zinapotokea safari za viongozi wote kwa wakati mmoja,” Mhagama anasema.
“Kwa hiyo basi Bunge linaazimia kwamba Serikali ione umuhimu wa kufanya ununuzi wa ndege nyingine ili kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga kwa viongozi wakuu wa kitaifa".
Source: The Chanzo
Nini maoni yako kuhusu azimio hili?
Hapa inabidi tuwapongeze wawakilishi wetu,tabu waliokuwa wanapata Viongozi wetu kwa kuwa na ndege chache siyo jambo zuri.Zinunuliwe hata tatu za Kuanzia alafu zingine mwakani ili Viongozi waweze kutuhudimia vizuri.
Kwa bunge hili hakuna anayepinga kila kinacholetwa na serikali.Serikali ina ndege tatu za viongozi kama tulivyoarifiwa; ndege ya Rais na ndege zingine mbili kwa ajili ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Katika hali mbaya ya kiuchumi ambayo tunakabiliana nayo ikiwemo madeni ya Taifa, maisha magumu kwa wananchi, ukosefu wa ajira kwa vijana, uhaba wa vyakula kama sukari na mafuta ya kupikia, nauli kupanda kwa sababu ya ughali wa mafuta, ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, madawa na vifaa tiba hospitali za umma, pembejeo za kilimo kwa wakulima nk inakuwaje Bunge kuazimia kununua ndege mpya kwa viongozi?
Si wabunge hawa hawa kila siku wanalalamikia uduni wa huduma za jamii kwa wananchi wao? Si wabunge hawa hawa wanalilia serikali itoe fedha za maafa ya mafuriko, barabara mbovu, upungufu wa chakula na maradhi yanayowakumba wananchi.
Ina maana shida zote hizi wabunge wamezisahau mara hii?
Inashangaza Bunge kupitisha azimio la kununua ndege ya viongozi wakihesabiwa Rais wa Zanzibar na Makamu wake wawili, ina maana Serikali ya Zanzibar haiwezi kununua ndege kwa ajili ya viongozi wake? Ina maana hata magari ya viongozi wa Zanzibar yananunuliwa na Serikali ya Tanganyika? Mapato ya serikali ya Zanzibar ni kwa ajili ya nini kama hayawezi kuhudumia viongozi wake.
Napata wasiwasi huenda hata mishahara ya viongozi wa Zanzibar inalipwa na Serikali ya Tanganyika. Huu ni unyonyaji hauwezi kuvumilika hata kidogo! Yaani kwa Wazanzibari chao ni chao lakini chetu Watanganyika ni chao pia Wazanzibari! Huu si uungwana hata kidogo.
Hakika serikali tatu ni muhimu hivyo katiba mpya ni sasa!
Ndugu we acha tu.Kwanini wastumie hiyo hela kununua Majenreta makubwa ya Back Up kwa kipindi cha Kiangazi na Ukame ili angalao Gridi ikizidiwa yanawashwa ili mateso yapungue.
Ndege ya Viongozi ya kazi gani? Ile Ndege ya "kula nyasi"iko wapi?
Hata Mpina sijamsikia akihoji!Kwa bunge hili hakuna anayepinga kila kinacholetwa na serikali.
Kila mbunge anajihami Mwakani asikose Kuteuliwa kugombea.
Wamejifunza yale ya 2020 kwamba Rais ndio kila kitu Wajumbe ni Mbwa koko tu hawaweza kuchagua mgombea tena.
Mpina hana amani vitisho na mikwala anafanyiwa kwenda mbele huenda hata kulogwa juu sijui kama usiku huwa analala vizuri.Hata Mpina sijamsikia akihoji!
Itakuwa anapanga hoteli zaidi ya moja kwa hiyo analala kwa kuhama hama!Mpina hana amani vitisho na mikwala anafanyiwa kwenda mbele huenda hata kulogwa juu sijui kama usiku huwa analala vizuri.
Achunge Juisi za kuagiziwa au Soda unaletewa imefunguliwa asome kitabu cha Fidel Castro.Itakuwa anapanga hoteli zaidi ya moja kwa hiyo analala kwa kuhama hama!
Hiyo haiwezi kafanikiwa kwa Bunge hili la waganga njaa dawa yao ni kuwapa makavu hata kama watapuuza!Wakati mwingine njia bora ya kumshawishi mtu kuwa amekosea ni kumruhusu afanye anavyotaka.
Anaogopa Mwakani UchaguziHata Mpina sijamsikia akihoji!
They don't careWakati mwingine njia bora ya kumshawishi mtu kuwa amekosea ni kumruhusu afanye anavyotaka.