Bunge laazimia Serikali inunue ndege nyingine kwa ajili ya kuhudumia viongozi

Bunge laazimia Serikali inunue ndege nyingine kwa ajili ya kuhudumia viongozi

Shame on you who call themselves wabunge! Kura mliiba, pesa mnaiba, port mmeuza, baada ya kuhongwa na DP; mbuga mmeuza!

Nchi ina matatizo kibao; watoto hawana bima ya afya; umeme hamna; kila kitu bei juu watu wanalia! And all you can think about ni kujinunulia ndege! Shame!
 
Ningetegemea waazimie umeme, maji, usafiri wa umma upatikane kwa uhakika kuanzia kesho.
 
Bunge la Tanzania limeazimia kuwa Serikali iangalie umuhimu wa kununua ndege nyingine mpya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi wakuu wa kitaifa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Joseph Mhagama, ambaye ameeleza kuwa nia ya azimio hilo inatokana na Wakala wa Ndege za Serikali kushindwa kuwahudumia kwa wakati viongozi wakuu pale zinapotokea safari kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Mhagama kamati yake imebaini kuwa kwa sasa kuna ndege tatu zinazowahudumia viongozi wa Serikali. Ndege moja inamhudumia Rais wa Tanzania, ndege nyingine mbili zinawahudumia Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Kwanza na Wa Pili wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa kitaifa.

“Hali hii husababisha Wakala [wa Ndege za Serikali] kutekeleza jukumu la kuwahudumia viongozi kwa kuchelewa pindi zinapotokea safari za viongozi wote kwa wakati mmoja,” Mhagama anasema.

“Kwa hiyo basi Bunge linaazimia kwamba Serikali ione umuhimu wa kufanya ununuzi wa ndege nyingine ili kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga kwa viongozi wakuu wa kitaifa".

Source: The Chanzo

Nini maoni yako kuhusu azimio hili?
Naunga mkono hoja. Kila kiongozi awe na ndege yake ya kumhudumia.
 
Waafrika tuna matatizo lakini Watanzania tuna matatizo makubwa sana

Nchi zinazotuletea misaada husikii mambo ya kipuuzi namna hii.
Katika nchi hizo, Waziri anapewa 'credit card' ya kampuni kutumia kwa ticket na accommodation

Majuzi viongozi wa Bunge hili wamepitisha sheria ya kulipa 'watu wanaopendana' kwa kisingizio cha Wenza.
Kwamba hata wakiacha utumishi 'Wenza ' wanaendelea kulipwa. Wakifariki tayari wana 'insurance' ya familia zao

Wakati hayo yakiendelea kuna Walimu, Wauguzi, madktari, wahasibu, Wahandisi wastaafu hawajapata hata kikotoo cha kuanzia maisha. Kuna Polisi anasema miaka 30 ya utumishi amepewa milioni 18 yaani mshahara wa mwezi mmoja wa hao Wabunge wanaotunga sheria.

Tunaomba Bunge lipitishe haya
Bunge la JMT lipiisha sheria ya kuhakikisha kila mzazi anapewa kitanda na godoro kabla ya kujifungua
Bunge Lipitishe sheria ya kununua magari yatakayopeleka mishahara kwa Walimu vijijini
Bunge linunue 'Coaster' za kuharakisha mabwana shamba kufika mashambani haraka
Bunge lipitishe sheria Wahasibu wote wapewe magari maalumu kwa kusafirisha pesa na 'cheki'
Bunge lihakikishe kila Mwalimu ana Noah ili kuwahi darasani.
Bunge lipitishe sheria ya kila jimbo kuwa na Helicopter ya Wagonjwa

Mwisho, Wananchi wajilaumu kwasababu Katiba hii ndiyo inawapa uwezo wa kufanya upuuzi tunaouona

Kama wewe ni mwananchi na unasema siasa haikuhusu, Katiba mpya haikuhusu ni vema lakini gharama za hizo ndege zinakuhusu 100%

Afrika ina umasikini wa Viongozi si rasilimali.

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Hapa inabidi tuwapongeze wawakilishi wetu,tabu waliokuwa wanapata Viongozi wetu kwa kuwa na ndege chache siyo jambo zuri.Zinunuliwe hata tatu za Kuanzia alafu zingine mwakani ili Viongozi waweze kutuhudimia vizuri.
 
..Spika, Naibu Spika, Jaji Mkuu, na Naibu Waziri Mkuu, nao wanahitaji kuwa na ndege.
 
Serikali ina ndege tatu za viongozi kama tulivyoarifiwa; ndege ya Rais na ndege zingine mbili kwa ajili ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Katika hali mbaya ya kiuchumi ambayo tunakabiliana nayo ikiwemo madeni ya Taifa, maisha magumu kwa wananchi, ukosefu wa ajira kwa vijana, uhaba wa vyakula kama sukari na mafuta ya kupikia, nauli kupanda kwa sababu ya ughali wa mafuta, ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, madawa na vifaa tiba hospitali za umma, pembejeo za kilimo kwa wakulima nk inakuwaje Bunge kuazimia kununua ndege mpya kwa viongozi?

Si wabunge hawa hawa kila siku wanalalamikia uduni wa huduma za jamii kwa wananchi wao? Si wabunge hawa hawa wanalilia serikali itoe fedha za maafa ya mafuriko, barabara mbovu, upungufu wa chakula na maradhi yanayowakumba wananchi.

Ina maana shida zote hizi wabunge wamezisahau mara hii?

Inashangaza Bunge kupitisha azimio la kununua ndege ya viongozi wakihesabiwa Rais wa Zanzibar na Makamu wake wawili, ina maana Serikali ya Zanzibar haiwezi kununua ndege kwa ajili ya viongozi wake? Ina maana hata magari ya viongozi wa Zanzibar yananunuliwa na Serikali ya Tanganyika? Mapato ya serikali ya Zanzibar ni kwa ajili ya nini kama hayawezi kuhudumia viongozi wake.

Napata wasiwasi huenda hata mishahara ya viongozi wa Zanzibar inalipwa na Serikali ya Tanganyika. Huu ni unyonyaji hauwezi kuvumilika hata kidogo! Yaani kwa Wazanzibari chao ni chao lakini chetu Watanganyika ni chao pia Wazanzibari! Huu si uungwana hata kidogo.

Hakika serikali tatu ni muhimu hivyo katiba mpya ni sasa!
 
Kwanini wasitumie hiyo hela kununua Majenereta makubwa ya Back Up kwa kipindi cha Kiangazi na Ukame ili angalao Gridi ikizidiwa yanawashwa ili mateso yapungue.

Ndege ya Viongozi ya kazi gani? Ile Ndege ya "kula nyasi"iko wapi?

Ifufueni Air Kula Nyasi iwapeleke mnakotaka.
 
Serikali ina ndege tatu za viongozi kama tulivyoarifiwa; ndege ya Rais na ndege zingine mbili kwa ajili ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Katika hali mbaya ya kiuchumi ambayo tunakabiliana nayo ikiwemo madeni ya Taifa, maisha magumu kwa wananchi, ukosefu wa ajira kwa vijana, uhaba wa vyakula kama sukari na mafuta ya kupikia, nauli kupanda kwa sababu ya ughali wa mafuta, ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, madawa na vifaa tiba hospitali za umma, pembejeo za kilimo kwa wakulima nk inakuwaje Bunge kuazimia kununua ndege mpya kwa viongozi?

Si wabunge hawa hawa kila siku wanalalamikia uduni wa huduma za jamii kwa wananchi wao? Si wabunge hawa hawa wanalilia serikali itoe fedha za maafa ya mafuriko, barabara mbovu, upungufu wa chakula na maradhi yanayowakumba wananchi.

Ina maana shida zote hizi wabunge wamezisahau mara hii?

Inashangaza Bunge kupitisha azimio la kununua ndege ya viongozi wakihesabiwa Rais wa Zanzibar na Makamu wake wawili, ina maana Serikali ya Zanzibar haiwezi kununua ndege kwa ajili ya viongozi wake? Ina maana hata magari ya viongozi wa Zanzibar yananunuliwa na Serikali ya Tanganyika? Mapato ya serikali ya Zanzibar ni kwa ajili ya nini kama hayawezi kuhudumia viongozi wake.

Napata wasiwasi huenda hata mishahara ya viongozi wa Zanzibar inalipwa na Serikali ya Tanganyika. Huu ni unyonyaji hauwezi kuvumilika hata kidogo! Yaani kwa Wazanzibari chao ni chao lakini chetu Watanganyika ni chao pia Wazanzibari! Huu si uungwana hata kidogo.

Hakika serikali tatu ni muhimu hivyo katiba mpya ni sasa!
Kwa bunge hili hakuna anayepinga kila kinacholetwa na serikali.

Kila mbunge anajihami Mwakani asikose Kuteuliwa kugombea.

Wamejifunza yale ya 2020 kwamba Rais ndio kila kitu Wajumbe ni Mbwa koko tu hawaweza kuchagua mgombea tena.
 
Kwanini wastumie hiyo hela kununua Majenreta makubwa ya Back Up kwa kipindi cha Kiangazi na Ukame ili angalao Gridi ikizidiwa yanawashwa ili mateso yapungue.

Ndege ya Viongozi ya kazi gani? Ile Ndege ya "kula nyasi"iko wapi?
Ndugu we acha tu.

Wananunua mandege wakati BBT ya Waziri imefeli instead wangeipa support ikatukomboa na mfumuko wa bei ya Chakula.
 
Itakuwa anapanga hoteli zaidi ya moja kwa hiyo analala kwa kuhama hama!
Achunge Juisi za kuagiziwa au Soda unaletewa imefunguliwa asome kitabu cha Fidel Castro.
 
Back
Top Bottom