Bunge lakanusha Kauli ya Mbowe kuwa Mshahara wa Wabunge umepanda kutoka Tsh Milioni 13 hadi 18

Bunge lakanusha Kauli ya Mbowe kuwa Mshahara wa Wabunge umepanda kutoka Tsh Milioni 13 hadi 18

Mbowe alikuwa anaongea kama sehemu ya kujifurahisha tu .maana wakati ni mbunge hakuwahi kusema popote pale kuwa alikuwa anapokea millioni 13. Lakini ukitaka kufahamu ya kuwa CHADEMA ni waropokaji ropokaji rejea kauli ya John Heche ambaye naye alitamka kuwa wabunge wanapokea kwa sasa millioni 16. Kwa hiyo mpaka hapo unaweza kuona kuwa wanafanya upotoshaji na kutafuta sifa za kijinga jinga tu.ndio maana wanafanya kazi ya kuropoka ropoka tu wakiwa majukwaani.
 
Hivi hawa CHADEMA huwa wanaletaga uthibitisho wowote pale wanapotoa madai na shutuma zao?

Au hii ndio Kiki tu?

Tuone.
 
Maneno ya kukana hoja Hizo yametolewa na Kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa Bungeni..

Jana Ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara na kisha Video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amedai kwamba mishahara ya Waheshimiwa Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=)
hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)

View attachment 2942304

Mshahara wa mbunge ni zaidi ya shilingi za ki-Tanzania bilioni moja akitumikia kipindi cha miaka mitano (miezi 12 x miaka 5 ) ktk kikokotoo:

Mchanganuo wa mshahara wa miaka mitano wa mbunge ni Bilioni 1 na milioni themanini :

Shilingi 18,000,000 x miezi 12 = 216,000,000

Shilingi 216,000,000 × miaka 5 =1,080,000,000

  • Bado hapo pia anapokea allowance za vikao vya bajeti
  • Ziara za mafunzo Dubai, India n.k
  • Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge PAC, LAAC, Mambo ya Nje na ulinzi usalama n.k
  • Marupurupu ya mkopo wa gari n.k
  • Bima ya Afya kwa mbunge hospitali VIP Class n.k
  • Pensheni ya mkupuo akimaliza ubunge miaka
 
Mshahara wa mbunge wa zaidi ya bilioni moja kila mwaka (miezi 12) ktk kikokotoo:

Mchanganuo wa mshahara wa miaka mitano wa mbunge ni Bilioni 1 na milioni themanini :

Shilingi 18,000,000 x miezi 12 = 216,000,000

Shilingi 216,000,000 × miaka 5 =1,080,000,000

  • Bado hapo pia anapokea allowance za vikao vya bajeti
  • Ziara za mafunzo Dubai, India n.k
  • Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge PAC, LAAC, Mambo ya Nje na ulinzi usalama n.k
  • Marupurupu ya mkopo wa gari n.k
  • Bima ya Afya kwa mbunge hospitali VIP Class n.k
  • Pensheni ya mkupuo akimaliza ubunge miaka
Sasa hiyo ni kwa mbunge mmoja zidisha mara 393 (Idadi ya wabunge wote)
 
Waongo hao. Si waweke wazi ni kiasi gani wabunge wanalipwa badala ya kukanusha tu. Na kama waliaita akina Paskali Mayalla kwenye Kamati ya Bunge kwa mambo mdago kwa nini wasimuite Mbowe kwa hili.... Hapo ndipo nitaamini.

Chadema wana Mbunge wao mmoja bungeni. Amuombe atoe payslip yake hadharani.
Acha upoyoyo,mzee Mbowe aweke nyaraka za kuthibitisha alichoropoka ,vinginevyo anakaribia kuingia kwenye kundi la lema na mdude
 
Sasa hiyo ni kwa mbunge mmoja zidisha mara 393 (Idadi ya wabunge wote)

Hawa wabunge kwa kweli wanajioendelea wao kupita kiasi.

Waajiri kama madaktari, waalimu na pia sisi walipa kodi tuangalie kikokotoo cha wabunge kuvuna mshahara wa jumla ya billion moja ktk miaka mitano.

Na hapo bado marupurupu bima za afya hatujatia katika hiya billion moja.
 
Kwani Bonge Lingesemaje?
Wenye Akili Wanajua, Watanzani Siyo Wajinga Sasa Hivi
 
Habari ya wabunge kujiongezea mshahara si ya leo wala jana. Hii ni taarifa ya siku nyingi sasa kwa nini imechukua muda mrefu kukanusha?

Hatudanganyiki kwa kuwa Bunge na Serikali hii wamekuwa waongo kupita maelezo!
 
Walijiongeza kutoka 12 mpaka 13..
Ila sasa Wamejiongeza kutoka 13 mpaka 18
 
Wanachi mnataka tukale wapi sisi wawakilishi wenu.😃😃
Pwaaaapwaaa pwaaa,napenda kuchukia nafasi hii Adimu kumshukuru ........,Mama Dkt.......Mhe....S......
Mke wangu,Watoto wangu na familia yangu wapo pale juu.....

Pwaaaaaaaa pwaaaaaaa...Ndugu Wabunge wenzangu,Ndugu yetu Mbowe anaona hayuko Bungeni anaropoka ropoka tu huku mtaani.......

Bunge linashangilia kwa makofi na kicheko...😀😀😀😀😀

Anadakia Spika kwa sauti yake ..

Eee ndugu zangu wabunge,wewe kama haupo humu inakuhusu nini eee..eti Msukuma.
 
Nitamshangaa atakaye amini kauli ya Bunge kuhusu kujiongezea posho. Ila mke wa kikwete anafaidi, huku anapokea milioni 18 za ubunge kule anapokea pesa za mafao ya mke wa rais.
 
Acha upoyoyo,mzee Mbowe aweke nyaraka za kuthibitisha alichoropoka ,vinginevyo anakaribia kuingia kwenye kundi la lema na mdude
Sasa hao wanakanusha mbona hawasemi Wanalipwa Tshs ngapi. Wajinga endeleeni kuamini.
 
Pamoja na kukana je wanavyojiona wana sifa gani special ya kuwafanya wao kupokea mshahara Tsh 13,000,000/= pamoja na marupurupu chungu mbovu na bima za maisha za uhakika?
Ndo hapo SASA.au kwa sababu wanapitisha wao mapato na matumizi?
 
Back
Top Bottom