Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100.
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-
19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.
b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.
d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.
e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.
g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge
Sent using
Jamii Forums mobile app