Bunge lapitisha Muswada unaotaka wake wa Marais na Maspika wastaafu kulipwa kiinua mgongo

Bunge lapitisha Muswada unaotaka wake wa Marais na Maspika wastaafu kulipwa kiinua mgongo

Watu wanalipa tozo mbalimbali, wanalipa kodi mbalimbali, hali ni ngumu, maisha yamewapiga Watanzania.

Badala ya Serikali kuleta muswada wa kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuwapa unafuu Watanzania, yenyewe inaleta muswada wa kuzigawa fedha za Watanzania kwa kikundi kidogo cha watu ambacho hata hivyo kimekuwa kikifaidi mema ya Nchi kwa muda mrefu kabisa.

Mungu mwenye enzi, nguvu na uweza wa ajabu aingilie kati suala hili. Tunaodhani wangekuwa msaada kwa Wananchi, hao ndo wanakuwa GENGE la majizi na mafisadi.

Wabunge nao wakiamua tu, wanajiongezea posho na marupurupu ya kila aina.

Allah Akbar.
Daah hii imenisikitisha sana yaaani
Basi na wenza wa wastaafu wote nao walipwe kwa mfano polisi,walimu, n.k iwe haki kwa wote
 
Nani atawapa kiinua mgongo wake za walimu, wanajeshi wetu JWTZ, polisi, madaktari na wauguzi, na watumishi chungu nzima?

Imagine Mke wa Rais awamu ya 4,Ana haja ya kiinua mgongo kweli? 😀😀, yeye analipwa mafao ya mke wa Rais na mafao ya mbunge? Naambiwa alikuwa mwalimu, je amefikiria kuhusu kiinua mgongo cha mke wa mwalimu?

CCM mbele kwa mbele 😀😀😀Karibuni mnisakame
Alafu wanapewa kila kitu hata baada ya kustaafu
Kama ulinzi,nyumba, na wanaedelea kutunzwa na serikali kwa kila kitu lakini still hawariziki na wakati kuna kundi la vijana mtaani hawana Ajira ..
Yaani hii nchi tumelaaniwa
 
Alafu wanapewa kila kitu hata baada ya kustaafu
Kama ulinzi,nyumba, na wanaedelea kutunzwa na serikali kwa kila kitu lakini still hawariziki na wakati kuna kundi la vijana mtaani hawana Ajira ..
Yaani hii nchi tumelaaniwa
JK alikuja na slogan MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA kumbe alimaanisha MAISHA BORA KWA VIGOGO WA CCM
 
Inasikitisha na inahudhunisha sana kwa mambo ya ajabu yanayoendelea hapa nchini. Sikuwahi kufikiria kuwa wabunge wanaojidai kuwawakilisha wananchi wangethubutu kupitisha muswada wa kipumbavu unaokomba mabilioni ya pesa za walipakodi na kuwalipa watu ambao hawajawahi kuwa na njaa.

Pia soma:
1698833080155.png
Spika wa bunge la CCM aliyesimamia upitishwaji wa muswada wa ajabu

Wakati ujinga huu ukiendelea, shuleni hakuna madarasa wala madawati ya kukalia wanafunzi, hospitalini hakuna vitanda vya wagonjwa, nchi ipo gizani kwa kukosa umeme, wananchi wanashare maji na mifugo (hawana huduma ya maji safi) na idadi kubwa ya wananchi hawana uhakika wa maisha. Inauma sana.
1698838554490.png

Akina mama wazazi wakiwa wamelala chini (hakuna vitanda wodini)

1698833892510.jpeg

Wanafunzi wamekiti chini wanasoma chini ya mti

Hivi kwanini fedha hizi zinazochezewa kiasi hiki sizitumike kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida wanaoishi kama watumwa katika nchi yao inayosemekana kuwa na uhuru wa bendera lakini haina uhuru wa maisha bora na ustawi wa jamii? Nchi hii imerogwa au ni nini hasa kimeisibu?
1698838845208.png
1698839143149.png

Wananchi wakiteka maji dimbwini kwa ajili ya kunywa

Ndugu zangu watanzania mkae mkijua kuwa serikali ya CCM haina mpango wowote wa kuboresha maisha yenu. Wewe fikiria kule bungeni kuna wabunge wa CCM zaidi ya 360 lakini wanagonga madawati kupitisha muswada wa ovyo kama huu! Sisi walipakodi hatuna la kufanya zaidi ya kuendelea kutazama pesa zetu zinakwapuliwa na serikali na mafisadi na kuiacha hazina ikiwa tupu kama changudoa wa Buguruni kwa Kimboka anayewinda wateja usiku kucha bila mafanikio. Kila siku tunakamuliwa kodi lakini inawanufaisha vigogo wachache huku walipakodi wakiwa hawanufaiki ipasavyo. Inauma sana.
1698840611427.png

Kodi kila kona lakini hazina manufaa kwa walipa kodi

Hivi serikali hii iko madarakani kwa manufaa ya nani ikiwa inaweza kudiriki kuwakamua watanzania kodi kila siku halafu pesa hizo zinatumika kufanyia anasa? Serikali ni kama mtu mzima anayemtumia mtoto mdogo kama ngazi ya kufikia mafanikio yake bila aibu wala soni.
1698839766891.png

Wananchi ni ngazi ya mafanikio ya vigogo

Wabunge waliopitisha muswada huu wa kishetani hawana tofauti na mtu mzima aliyekabidhiwa kumnywesha mtoto maziwa akuwe badala yake yeye mwenyewe anajinufaisha kwa maziwa hayo. Hii ni aibu kubwa sana.
1698839945267.png

Vigogo wanawadhulumu sana wananchi keki ya taifa

Ni nani hasa atakayewanasua wananchi kutoka tope la umasikini walilonasa kwa zaidi ya miaka 60 sasa? Ndugu zangu watanzania tuamke kumekucha. Sishangai Rais Kenyatta aliwahi kumuambia mwalimu Nyerere kuwa yeye (Nyerere) hatumii nguvu nyingi kuongoza kwa kuwa anaongoza maiti (watanzania). Ni maiti pekee anayeweza kukubali mambo haya ya kipumbavu yanayofanywa na serikali ya CCM bila aibu.

Nawasilisha

 

Attachments

  • 1698839649465.png
    1698839649465.png
    199.2 KB · Views: 1
Watalipwa ikiwa hao waume au wake zao watakufa wakiwa kwenye uongozi. Mfano mwigulu afe leo na sheria ishapitishwa basi mkewe atapata mgao ila akimaliza kipindi chake ndipo afe basi hakuna mgao.
Soma vizuri hansard za bunge mkuu. Sheria inasema wataanza kulipwa immediately sheria hii ya kipuuzi itakaposainiwa na Rais. Na Rais naye mume wake ataanza kulipwa haraka iwezekanavyo. Nchi ya kijinga sana hii.
 
Soma vizuri hansard za bunge mkuu. Sheria inasema wataanza kulipwa immediately sheria hii ya kipuuzi itakaposainiwa na Rais. Na Rais naye mume wake ataanza kulipwa haraka iwezekanavyo. Nchi ya kijinga sana hii.
Hebu iweke hapa tuisome maana mimi kwa maelezo na uelewa ni pale wanapokufa hao viongozi wakiwa kazini. Iweke tuijadili hapa kwa pamoja tuweze ielewa wote
 
Kwa wanaoamini Mungu tumuombe atupe watu,
MUNGU ATUPE "WATU"🤲🙏
MUNGU ATUPE "BINADAMU"🤲🙏
Wawahurumie wenzao.......
 
Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.

Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.

Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.

#MillardAyoBUNGENI
Hii nchi ni ya kipumbavu sana aisee! muswada gani wa kipuuzi huu? Sijawahi kuona miswada ya kipumbavu kama huu tangu nizaliwe hapa duniani.
 
Vyovyote iwavyo, huo ni uhuni mtupu
  1. Watumishi wa umma hawalipwi stahiki zao na wanafanya kazi katika mazingira ya hovyo ati fedha hakuna
  2. Huduma za jamii (shule, afya, maji nk) ni duni kisingizio fedha hakuna
  3. Barabara za mitaa mbovu kupita maelezo wanasema fedha hakuna
  4. Waliotoa huduma serikalini wanadai fedha nyingi hawalipwi
Ajabu matumizi ya kufuru ndiyo hayo
  1. Wabunge posho juu
  2. Mashangingi ya anasa yanabamizwa na kubadilishwa kila uchao
  3. Wastaafu wanajengewa mahekalu na kulelewa na kodi zetu huku wameshajilimbikizia mali
  4. Fedha zinafujwa kila kona hakuna anayejali wala kuchukua hatua
 
Back
Top Bottom