Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa

Bora livunjwe warudi majimboni angalau na sisi raia tupate hizo rushwa ndogo ndogo kama pilau, pesa za ugoro,kofia na mengineyo maana tumezi 'miss' kwa muda mrefu.[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nishajiandaa na kadi za vyama nijilie rushwa ndogo ndogi
 
Kwenye list ya maspika umekosea sequence kidogo.

(1) Abulkarim Karimjee -Mpaka 1962
(2) Adam Sapi Mkwawa- 1962- 1973
(3) Erasto Mang'enya- 1973- 1975 (Sikumbuki ni nini kilichomfanya Mkwawa aache gap hili)
(4) Adam Sapi Mkwawa - 1975- 1994
(5) Pius Msekwa - 1994- 2005
(6) Samwel Sita - 2005-2010
(7) Anna Makinda- 2010-2015
(8) Job Ndungai - 2015-2020
 
Kama mojawapo ya kazi ya wabunge ni kuishauri na kuikosoa serikali pale panapo hitajika kufanya hivyo, sasa imegeuka kinyume na sasa baadhi ya wabunge hasa wana ccm ni kuitetea serikali
Bunge la hovyo sana kuwai kutokea hapa Tz. Sioni umuhimu wa kuwepo Bunge hapa kwenye nchi ya Yesu.
 
Cdm ni chama makini sana hawapo tayari kutumiwa kama rubber stamp kupitisha sheria mbovu, ambazo zitakuja kuwaumiza watanzania.
Chadema watatoka bungeni,halafu wataa canteen,kumsikiliza Rais
 
Bunge la Ndugaye limeshindwa kuisimamia serikali na badala yake limekuwa ni mtetezi wa serikali
Bunge linapaswa kutafakari kama limeisimia serikali ambao ndo wajibu wake mkuu au limekuwa sehemu ya serikali katika kipindi cha miaka hii mitano
 
Spika wa pili ni Erasto Mang'wenya. Mtoa Uzi fanya ku-edit hapo ili kuweka kumbukumbu sawa.
Mang'enya (siyo Mang'wenya labda ni typo tu) alikuwa spika kwa muda mfupi sana kama nilivyoonyesha hapo juu, utumishi wake mwingi ulikuwa serikalini. Asingekuwa Spika wa kwanza kwa vile wakati Bunge letu la kwanza linaaza yeye alikuwa mwakilishi kudumu kwenye Umoja wa mataifa
 
Msafara wa spika umekweisha ingia ,spika job ndugai anaingia kwenye eneo la bunge kama mwenyeji kumsubilia mgeni rasmi Jonh pombe magufuli
 
Kwahiyo likiwa na wapinzani wachache Ndiyo uchumi wa Tanzania utapanda kwa asilimia angalau 8%?
Thread yako inatoa kumbukumbu nzuri ya matukio.

Hili litakuwa ni bunge la mwisho lenye wabunge wengi wa upinzani.

Hali halisi inaonyesha bunge lijalo litakuwa na wabunge wachache sana wa upinzani huku likiongozwa na KUB mpya!
 
Umesahau kabisa kuwa mficha maradhi siku zote kifo ndio umuumbua, endeleeni kuchezeshwa ngoma ya madogori
 
Kwakweli kama kuna mbunge wa chadema atarudi bungeni ntaamini wizi wa kura upo
 
Ukiambiwa nyinyi ni zaidi ya wana futuhi mnarusha ngumi hewani.

Mlipo kuwa mnaruhusu mfumo wa multi party system mlilazimishwa? Au hamkujua kuwa huo mfumo alimaanisha kuwa kutakuwa na vyama vya upinzani?
Wingi wao haujasaidia chochote bora tuwe na Wabunge wa chama kimoja tu chama tawala
 
Vipi wadada wa Udom, CBE nk wametapakaa mtaani kupata pensheni za mwisho mwisho?
 
Kwa akili za watawala wanadhani upinzani ni Mbowe na Lissu au zile kombati zao
uzuri ni kwamba upinzani unafutwa kibabe (sio kidemokrasia) hivyo upinzani halisi bado upo sana!.
watawala wanajidanyanya/mnawadanganya na kweli wamedanganyika!.
 
Ikiwezekana asiishie tu kwenye kulivunja hilo bunge! Alibomoe kabisa na hilo jengo lake maana ndani ya awamu hii ya tano, hilo bunge limeinufaisha zaidi ccm na viongozi wake kuliko sisi wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…