Wanajamiiforums ,tumekita kambi tangu alfajri maeneo ya bunge hapa Dodoma hapa mambo ni mengi kila mtu yuko bize wewe mwana jf utapata kila kitu hapa hapa na kama unaswali uliza pia .
UTANGULIZI
Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 65 (1,2) inampa nguvu rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ya kulivunja bunge kwa kulihutubia ambapo inatarajiwa muda mfupi ujao leo 16/6/2020 mh rais John Pombe Joseph Magufuli atalivunja bunge la kumi na moja ,itakubukwa kuwa mnamo tarehe 20/11/2015 rais John Pombe Magufuli alilizindua bunge hili la 11 hapa Dodoma kwa mara ya kwanza kama ibara ya 91 (1) ilivyomtaka na hii itakuwa mara yake ya pili kulihutubia na kulivunja pia,hii inamaanisha muda wa bunge la kumi na moja utakuwa umeisha kama ibara ya 65 (2)inavyotamka na kutoa wasaa wa nchi yetu kuelekea katika uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani .
MASPIKA
Job Ndugai anakuwa spika wa sita mzalendo baada ya ukoloni wengine ni
1.Chief Adam Sap Mkwawa 1964-1973
2.Erasto A.M.many'ingu 19731975
3.pius msekwa 1975-2005
4.Samweli sita 2005-2010
5.Anna Makinda 2010-2015
6.Job Ndugai 2015-2020 ambaye ubunge wake unakoma leo na ameshatangaza kuondoka
MAMBO MUHIMU KWA BUNGE LA KUMI NA MOJA
Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limekuwa chombo kikuu cha kikuungano kinacho jumuisha wabunge 393 ,watanzania bara wakiwa 322 na wanzibari wakiwa 71 .wabunge wanawake kwa ujumla wakiwa 145 na wanaume 248 kwa wabunge wote waliomo katika bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania.
C.C.Mimekuwa na wabunge 287, chadema 63, C.U.F 32 ,ACT WAZALENDO1 na NCCR MAGEUZI 1 ukiachilia hamahama ya wabunge.wabunge wa majimbo walikuwa 264.viti maalum 113 .wabunge wawakilisha wa Zanzibar 5.wabunge wa rais 10 na mwamasheria mkuu wa serkali 1.
Aidha mbunge aliyeuliza maswali mengi ni George Malima lugereje wa jimbo la mpwapwa mawasli 103 na michango 59 huku wizara iliyopokea maswali mengi ni wizara ya TAMISEMI na waziri wake Suleiman Jafo kuwa waziri aliyejibu maswali mengi zaidi,mbunge Dk mary Nagu ndio mbunge alihudumu bungeni muda mrefu kwa vipindi vinne mtawalia huku mbunge George mkuchika akiwa ndio mbunge mwenye umri mkubwa zaidiwa miaka 72 ,mbunge Halima Bulembo yeye ndio mbunge mwenye umri mdogo wa miaka 28 kwali aliingia bungeni akiwa na miaka 23 tu.
Bunge hili la kumi na moja limekamilisha kuchambua na kupitisha bajeti tano za serkali na miswada 82 ya sheria na hasa zile za hati za dharula zilizoletwa na serkali
Kama sehemu ya ya majukumu ya kikatiba ya bunge hili.
BAADHI YA PANDA SHUKA ZA BUNGE LA 11
Kumekuwa na panda shuka za msuguano wa bunge hili na taasisi nyingine katika masuala mbalimbali
1.tarehe 7/sept/2017lilitoke tukio la mbunge Tundu lisu kushambuliwa na risasi ambapo wabunge wengi hasa wa upinzani walizua sintofahamu kuhusu usalama wao na familia zako na kutaka majibu ya kina ya serkali na kuzua mkwaruzano
2.Poul Makonda( RC. Dar es salaam) kuwatuhumu wabunge kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya ambapo wabunge walionesha hasira na kutaka serkali imwonye
3.Poul Makonda (RC.Dar es salaamu) kuwatuhumu wabunge kuwa wanasinzia tu bungeni na ikapelekea kuitwa mbele ya kamati ya bunge kuhojiwa
4.wabunge wa upinzania kuwekwa vizuizini kwa miezi kadha na kuzua hofu ya uonevu mfano Godless lema,Freeman mbowe,lijualikali,Halima mdee ,Joseph Mbilinyi na nk.
5.Hama hama ya wabunge wa upinzani kihistoria bunge la kumi na moja ndio limetia fora wa wabunge wengi kuhama vyama vyao vya awali na kujiunga na ccm
6.Hoja ya CAG ,baada ya CAG mstafu kutoa hoja yake wakati akihojiwa na redio ya umoja wa mataifa kuwa bunge ni dhaifu kuisimamia serkali uongozi wa bunge na baadhi ya wabunge walikuja juu kutaka aitwe na ahojiwe na hili lilifanyika ba baadae akaoneshwa mlango wa kutokea
7.kufukunzwa kwa wabunge kutumika umma kwa sababu za utoro bunge hili linalomaliza muda wake lilifukuza wabunge wawali kazi mbunge Joshua Nasari na Tindu lisu kwa kile kilichotajwa kuwa ni utoro
8.Spika kuugua kwa muda mrefu na kuzua taharuki ,baada ya spika wa bunge la kimi na moja kulazwa nchini India na kudaiwa kutumia pesa nyingi hapa nchini na hasa bungeni kulikuwa na hofu.
9.Itakumbukwa wakati wa bunge hili kuanza siku ya kwanza ya hotuba ya rais wabunge wa upinzani waliondoka bungeni kwa madai ya kutoridhika na matokeo ya urais Zanzibar chini ya mwavuli wa ukawa hivyo kususia hotuba ya rais
10.Madai ya kuumizwa kwa kiongozi ya kambi rasmi ya upinzani bungeni ambapo pande mbili bado zinarushiana maneno kama ni kweli alishambuliwa na wengine wakisema ameanguka kwa kuzidiwa na pombe
11.ishu ya mbunge Cecil mwambe aliyekiacha chama chake cha chadema na kuendela kuhudumu ambapo jamii ya watanzania ilishangaa kwani katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 71 (1,2,) inatamka kuwa ubunge wake utakuwa umekoma baada ya kuhama chama.
12.Kutokuoneshwa bunge live ,hili lilizua kizaazaa bungeni na mitaani watu wakitaka bunge lioneshwa life.
13. Ishu ya corona ambapo wabunge wa upinzani waliamua kuondoka kwa madai serkali haikuchukua hatua za kuzuia
14.ishu ya escrow ambapo mwanasheria mkuu wa serkali aliondoka bungeni kwa aibu
15.mwenyekiti wa chama cha wananchi C.U.F professor lipumba kuwafuta ubunge wabunge 8 kwa wakati mmoja na kuwafanya wakose sifa za kuwa wabunge
MAFANIKIO YA BUNGE LA KUMI NA MOJA.
Hata hivyo kumekuwa na mazuri ya bunge hili la kumi na moja
1.ujenzi wa shule ya wasichana kwa kutumia michango ya wabunge na wahisani ambapo shule hii imepewa jina la bunge
2.kushirikiana kwa karibu ya serkali kwa ukaribu na kufanikisha kusimamia miradi ya kimkakati ya serkali
3.kusomamia malipo ya wabunge watoro wa vikao ,bunge hili la kumi na moja limeonesha umakini wa kusimamia malipo hewa ya pesa za walipakodi
4.kupunguza urasimu wa habari na kupitisha miswada haraka ili kwenda na kasi ye serkali
5.Kulinda hadhi ya bunge ,bunge hili la kumi na moja halikubali kuyumbishwa kwani limekuwa likiwaita na kuwahoji wote walolionekana kupingana na mwenendo wa kanuni na sheria za kibunge.
6.kutetea wabuge walioonekana kuonewa na vyama vyao mfano cecil mwambe na lijualokali
7.kuunda mfumo bora wa kidijitali ilikuwawezesha wabunge kupata taarifa za kinachoendelea bungeni hata kama hawapo bungeni
8.kuihoji serkali juu ya matumizi ya pesa za umma hasa zile za kwenye miradi ya kimkakati
9.kuishauri serkali juu ya hoja zilizowekwa mezani
10.kuungana wakati wa matatizo kama vifo vya wabunge wenzao na waiopata matatizo ya kuugua na kilazwa
WAGENI WAALIKWA
Wageni mbalimbali wamewasili hapa mjini dodoma tangu majuzi na wengine wanaendea kufika ,wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama tayari wamekwisha kufika ,mawaziri wakuu wastafu na mabalozi wa nchi marafiki bila kuwa sahau mabalozi wa mashirika mbalimbali ya kimataifa au waaakilishi wao viogozi ni wengi.
Wa kuu mikoa wenyeviti wa vyama vya siasa viogozi wa dini madhehebu mbalimbali
Ulinzi umeimarishwa mara dufu gari za dolia usiku mzima na alfajiri hii askari kila sehemu hasa maeneo ya bunge na ikulu ,usafi pia umefanyika kwa kiwango cha kuridhisha tofauti na siku nyingine za kawaida
Television karibu zote zita kuwa hewani nawaona wawakilishi/wanahabari wao mapema sana kuna vyombo vya nje kama CRI .DW .BBC na ndani ya nchi TBC1,channel ten,ITV.star Tv.clouds tv.EATV watu wa online tv ,blogs ,magazeti na n.k
Nipo hapa bungeni unaweza ukaweka swali hapa
Karibuni
USSR