BUNGENI: Peter Serukamba(CCM) atukana tusi kali, "F*** you"

BUNGENI: Peter Serukamba(CCM) atukana tusi kali, "F*** you"

SERUKAMBA kuwa mbunge hakumaanishi wewe unaweza lolote popote. Hata kama una kinga ya KIBUNGE kuongea lolote ndani ya BUNGE na usishtakiwe hiyo haikupi uhuru wa kuzungumza matusi bungeni. CCM mmelewa madaraka. Nauona mwisho wenu hivi karibuni mkifanya masihara mtabaki historia.
 
Bungeni kuna matusi mengi tu na mengine wanatoa hao ambao unawataka waratibu maandamano.

Wamalizane tu huko huko bungeni, wakumbuke tu kuwa wananchi wanataka maendeleo wakishamaliza kutukanana.

acha kufariji Chama Cha Matusi,nambie mpinzani alowahitoa tusi kubwa ivyo..nadhani ni mbunge wa kwanza toka chama cha wahuni mafisadi..ndo mmeendelea kujimaliza
 
Bado unasubiri? Ndo ishatoka hiyo....kama nilimwelewa, Makinda alisema mbunge akitukana anaita polisi na sio ataita!! I don't believe kama haya mambo yanatokea kutoka kwa watu wazima!!

Endelea kutokuamin...:rockon:
 
Matusi ya Serukamba yanazungumza mengi kuhusu kiburi cha wabunge wa CCM pamoja na chama chao. Bunge ni moja kati ya mihimili mitatu ya taifa letu. Na ni wajibu wa kila mbunge kuheshimu nafasi hiyo adimu wananchi waliompatia. Kitendo alichofanya Mpumbavu (siwezi kutumia neno Mheshimiwa kwa mtu kama huyu) Serukamba ni kitendo kinachomzalilisha yeye mwenyewe, Chama Chake na mbaya zaidi wananchi waliomchagua. Wakati umefika kwa Wabunge CCM kuja mbele na kukemea matusi ya Serukamba! Kama hawatafanya hivyo basi wananchi hatutofautisha wao na Mpumbavu Serukamba.
MKuu kweli aisee umekasirika kweli kweli.....kiburi hiki kinaletwa na mfumo waliojiwekea kuwa wakiwa bungeni ni kuwapinga tu Chadema....ndio sera yao....na mama spika kazi yake kawekwa pale kuzima kila hoja inayotoka kwa wapinzani.....
 
Inategemeana na mazingira, kama unaongea point halafu mtu anakuja na pumba badala ya mchele kwa nini asimbulie tusi japo kidogo? Under similar circumstances we would just be like him..! Its only a fool who condemn, blame and complain..!
There's no way you can justify this, absolutely, NO WAY! Bungeni? Huku ukifahamu fika kwamba kuna watu all over the country wanasikiliza na wengine kuangalia LIVE? Unjustifiable aisee!
 
MATUSI TENA?? NAULIZA KUNA AIBU YA MATUSI TENA BUNGENI DODOMA KWELI???????

...... Kwa mtaji wa matusi mazito kiasi hiki tena siku moja tu tangu Mhe Spika kutoa onyo kwa taasisi hiyo ya kikatiba; sasa ni wazi zaidi kwamba hakika KUNA TATIZO KUBWA MNO KWA WAWAKILISHI WETU hawa.

Ama kweli pengo la Mh Samuel Sitta, mzee wa standards and speed, sasa ni dhahiri zaidi kuliko hapo jana. Hakika hadi hivi sasa wananchi tunapata picha mbaya sana tena sana toka bungeni Dodoma kinyume kabisa na matarajio jamii yetu zima na hasa watoto wa taifa hili.

Ila fundisho tunalopata ni pamoja na kufanya mageuzi yafuatayo kipindi kijacho, katika mchakato wa kupitisha mtu kugombea kiti cha ubunge, ili kunusuru taifa na fedheha kama hizi:

1. Kufanya thorough background check kwa mwombaji kwa kufuata taratibu za wazi;

2. Kupandisha zaidi VIWANGO VYA ELIMU vinavyohitajika kukidhi kwanza ili kuwa mbunge;

3. Mafunzo kwa wabunge kuhusu ubunge, majukumu yaliomo, na matarajio ya umma;

4. Siku za usoni Spika sharti awe na misingi ya taaluma ya sheria ili kukirejeshea nafasi hii ya kitaaluma heshima yake stahiki;

5. Kosa lolote la kinidhamu bungeni lifike mahala litafune 1/4 pato la mbunge walau
kwa kipindi cha siku 90 tangu kosa kutendeka (kwa utaratibu huu kutajitokeza uhiari wa kuonyesha nidhamu bungeni).


Nimeshangazwa sana na Serukamba,, amesema COME ON FU*K YOU...

Nilikuwa sijaangalia bunge 2013 na leo imetokea kwa bahati mbaya but sirudii tena kuangalia bunge. Mbaya zaidi kavaa suti na ni jana tu Spika alisema atawakamatisha polisi. Wapi tunaenda jamani mbunge mwenye zaidi ya miaka 7 bungeni kusema F*CK YOU bungeni
 
Kasema f.a.k.y.u da!c walisema ukitukana wanaita polisi ngoja tuone ccm bana

walidhani hilo rungu litaanza kuikumba CDM kwanza badala yake limewajia na spika kashindwa kutekeleza uamuzi wake wa jana
 
Hebu wataalam kizungu watusaidie kuliweka kwenye kiswahili sie wa shule za kata. Taratibu zinazingatiwa
"Unaliwa uroda" mkuu,nimetumia tafsida hapo!!!
Duh!!ingekuwa ni kamanda wa chadema leo dunia ingesimama!!!!
 
Hapa Spika Makinda anatakiwa kusimamia kauli yake na lazima aone amedharauliwa vya kutosha coz' it doesn't make any sense, within 24 hours, jambo ambalo amelitolea tamko, linatokea tena! Kama Makinda alimaanisha, basi hana budi kuonesha makucha yake sasa ili ifahamike haikuwa ni kauli kwa ajili ya watu wa upande fulani au ilikuwa ni "tishia nyau!" tu!!
 
Ni matumizi au mazoea mabaya ya lugha za watu, au ana bwana anayejivunia??!
 
MKuu kweli aisee umekasirika kweli kweli.....kiburi hiki kinaletwa na mfumo waliojiwekea kuwa wakiwa bungeni ni kuwapinga tu Chadema....ndio sera yao....na mama spika kazi yake kawekwa pale kuzima kila hoja inayotoka kwa wapinzani.....

Yo Yo,

Hivi vitu vinatia hasira sana! Nakubaliana na wewe kuwa mama Spika amewekwa pale kumaliza hoja za upinzani na kuharibu image ya upinzani kwa wananchi. Kitu ambacho hawa viongozi wenye muono mdogo "myopic" wanachoshindwa kuelewa ni kuwa historia itawahukumu. Zaidi ya yote, Tanzania ni zaidi ya chama chochote cha siasa. Ni lazima wajifunze kuweka maslahi ya taifa mbele. Kuna sababu watoto wadogo leo wengi wanajua kulikuwa na Rais anayeitwa Nyerere, lakini hawajui kitu chochote kuhusu Mwinyi.
 
Mkuu NasDaz, ukitaka kuamini, Chukua wale watoto wa primary, uwapeleke bungeni Dodoma, kama kawaida bi kiroboto, atakutambulisha na kusema, waliopo kwenye Spika galary ni wageni wetoto watoto wa shule ya msingi..Bunge Dar, ni jirani zetu, wamekuja kwa MAFUNZO na wameletwa na NasDaz.

Kisha mtasimama, baada ya dakika kumi, watoto wataanza kulia na kutoa... watoto wote watakimbia na kuanza kukupiga,

Mkuu, Ilitoke watoto wapo Bungeni-mafunzoni- walimuona Wassira akijibu hoja- alijibu kwa ukali sana, mpaka watoto wakaogopa...
 
Last edited by a moderator:
MATUSI TENA?? NAULIZA KUNA AIBU YA MATUSI TENA BUNGENI DODOMA KWELI???????

...... Kwa mtaji wa matusi mazito kiasi hiki tena siku moja tu tangu Mhe Spika kutoa onyo kwa taasisi hiyo ya kikatiba; sasa ni wazi zaidi kwamba hakika KUNA TATIZO KUBWA MNO KWA WAWAKILISHI WETU hawa.

Ama kweli pengo la Mh Samuel Sitta, mzee wa standards and speed, sasa ni dhahiri zaidi kuliko hapo jana. Hakika hadi hivi sasa wananchi tunapata picha mbaya sana tena sana toka bungeni Dodoma kinyume kabisa na matarajio jamii yetu zima na hasa watoto wa taifa hili.

Ila fundisho tunalopata ni pamoja na kufanya mageuzi yafuatayo kipindi kijacho, katika mchakato wa kupitisha mtu kugombea kiti cha ubunge, ili kunusuru taifa na fedheha kama hizi:

1. Kufanya thorough background check kwa mwombaji kwa kufuata taratibu za wazi;

2. Kupandisha zaidi VIWANGO VYA ELIMU vinavyohitajika kukidhi kwanza ili kuwa mbunge;

3. Mafunzo kwa wabunge kuhusu ubunge, majukumu yaliomo, na matarajio ya umma;

4. Siku za usoni Spika sharti awe na misingi ya taaluma ya sheria ili kukirejeshea nafasi hii ya kitaaluma heshima yake stahiki;

5. Kosa lolote la kinidhamu bungeni lifike mahala litafune 1/4 pato la mbunge walau
kwa kipindi cha siku 90 tangu kosa kutendeka (kwa utaratibu huu kutajitokeza uhiari wa kuonyesha nidhamu bungeni).

Hata ufanye yote hayo haisaidii kitu aisee. Wabunge wa CCM wanajisikia sana, wanaona kama wako juu ya kila kitu na hizo dharau ndio zinasababishwa wawatukane wenzao matusi ya nguoni kwa kuwa wanajua hawatafanywa kitu chochote
 
Back
Top Bottom