Burkina Faso: Cptn. Ibrahima Traore apunguza mishahara ya wanasiasa

Hazikupata maendeleo zikiwa za kidemokrasia. Hakuna nchi ya kidemokrasia inaweza kupata maendeleo.
 
Hazikupata maendeleo zikiwa za kidemokrasia. Hakuna nchi ya kidemokrasia inaweza kupata maendeleo.
South Africa na nchi zingine za ulaya. Maendeleo yao ni endelevu tafauti na nchi za kidicator. Mfano putini akifa tu na uchumi wa urusi unayumba mana mwenye sauti ni mmoja. Faida ya demokrasia hata muweke kichaa kiwa rais bado hataathiri uchumi maana siyo last decision maker
 
Nchi ikishakuwa na watu kama Sankara au JPM huwa huko mbele watu hawaishi kupiga kelele kutaka mtu kama huyo. Na lazima atatokea mtu kama huyo. Hata wana wa Israeli walikuwa wanalia na kuomboleza aje Daudi mwingine.
 
Sometimes not all the time.
Tumechoshwa na hili liCCM, bora liondoshwe hata kijeshi.
Benjamin Franklin once said: "Those who would give up essential Liberty, to purchase a little temporary Safety, deserve neither Liberty nor Safety."
 
Hehe afrika kusini tokea waachiwe hao weusi na demokrasia za mzungu si ndo na nchi ikaanza kuharibika,, SA wangeanza watu weusi na hizi demokrasia za mzugu kwa sasa wangekua tu kama mataifa mengine ya huko kusini
 
South Afrika iliendelea wakati wa makaburu wabaguzi wa rangi. Leo kwenye demokrasia hata umeme hawana, hata yale mazuri wameyaharibu. Nchi za Ulaya ziliendelea zamani kabla ya demokrasia. Kilichopo sasa ni demokrasia kuyaharibu maendeleo hayo.
 
Acha masikhara basi

Long live Traore
 
West watamtegenezea Rebels...watampinduA.

Africa pagumu nyinyi..😭😭
Tumuombee
 
Hehe afrika kusini tokea waachiwe hao weusi na demokrasia za mzungu si ndo na nchi ikaanza kuharibika,, SA wangeanza watu weusi na hizi demokrasia za mzugu kwa sasa wangekua tu kama mataifa mengine ya huko kusini
Kumbuka south afrka iko kati nch za g8 na ni ya pili afrika kwa uchumi. Hata majuzi tu uchaguzi wao umeenda kidekrasi hakuna wizi wowote tofauti na jpm ambaye alipora uchaguzi wote kwa kutumia wakurugenzi Na sasa tuna bunge la ajabu ambalo haliwezi hata kumwambia samia fanya hiki acha hiki
 
Hazikupata maendeleo zikiwa za kidemokrasia. Hakuna nchi ya kidemokrasia inaweza kupata maendeleo.
Marekani haijawahi kuwa ya kidikteta na ina maendeleo. Uingereza ilianzisha First Reform Act mwaka 1832. India imekuwa ya kidemokrasia miaka mitatu baada ya uhuru, ilinganishe na Pakistan inayoongozwa na majenerali muda mwingi. Na walipata uhuru kwa pamoja.
 
Ukiona hivyo, jua raia wameshachoshwa na demokrasia za kilaghai.
Tunaweza kuondoa demokrasia za ulaghai bila kutamani utawala wa kijeshi.

Tatizo Watanzania wengi wanapenda kupelekwa pelekwa kama ng'ombe.

Ndiyo maana wanapenda utawala wa kijeshi.

Na hawa watawala wetu washawajulia, ndiyo maana kina Magufuli na Samia hawaishi kuvaa kombati kujionesha na wao wanajeshi.

Na siku hizi wanateua wanajeshi kwenye nafasi za kisiasa.

Wakati tulishatenganisha jeshi na siasa.
 
Marekani ilkuwa kama South ya Makaburu. Miaka 70 baada ya uhuru ndiyo utumwa wa tu weusi ulikomeshwa. Katika miaka hiyo yote walikuwa wanachinja Wahindi wa Marekani na kuwapora ardhi. Wanawake hawakuruhusiwa kupiga kura hadi miaka ya 1920's. Watu weusi hawakuruhusiwa kupiga kura hadi miaka ya 1960's. Huwezi kusema nchi hiyo ni ya kidemokrasia, kusema ya kibepari ni sawa. Leo demokrasia ya Marekani imekomaa lakini ndiyo inadidimiza nchi. Leo nchi yao haiwezi hata kujenga high speed railways sababu ya kubishana na urasimu unaoletwa na demokrasia. Hata uhalifu unawasumbua kudhibiti.

Marekani ilikuwa kama SA au Ujerumani ya wanazi tu. Huwezi kusema nchi hizo zilikuwa za kidemokrasia. Uingereza imeendelea sababu ya uporaji tu, leo na demokrasia yao ipo karibu kufirisika. Fuatilia miji inavyotangaza kufirisika. Na India na ukubwa wake ifananishe na China si Pakistani.
 
Tuiondoe roho ya kwanini, kijana kafanya vizuri, silaha ananunua hapewi Bure. Kuna washirika wasio na mashart magumu kama wamagaribi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…