Butiku: Viongozi watambue wanaongoza watu siyo kuku au mbuzi

Unachokisema ni kweli. Lakini huyu maza hawezi wafukuza hawa washirika wa msoga
 
Sijaelewa, Butiku anamuunga mkono Bashiru, pia Mzee Warioba anamuunga mkono Bashiru, ndio kusema Bashiru ana hao wazee na genge lake wako nae..

Ila wanasiasa sio watu kabisa, juzi kati hapa wakati wa Jiwe, huyo Bashiru alikuwa ni Mungu mtu yaani, alikuwa anajua watu wanauliwa, wanapotea, wanafilisiwa mali zao, wanateswa vibaya na kikosi kazi maalum, hakuna uhuru wa mawazo au kuongea ila Bashiru alikuwa kimyaaaa, aliona mambo sawa kabisa, nchi ilifikia sehemu ya hatari sana, kupotezwa ilikuwa dakika tu, ila Bashiru alikuwa haoni, sbb ya upigaji, anakula asali na kulalia asali..

Bashiru leo katoka kwenye inner circle ya asali, kaanza kupiga kelele bila aibu kumkashifu Mama Samia, yaani mm ningekuwa ndio Mh. Rais Samia, namfuta ubunge wa kuteuliwa haraka na arudi chuoni akafundishe ashike adabu..

Bashiru sio mtu, hafadhiliki, mnafiki sana.
 
Kwan top leader wa sasa hawakuyaona hayo unayoyasema na kama waliyaona kwann walikaa kimya pia tena walikuwa part of dola sembuse Bashiru alikuwa katibu wa chama

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Kama alikuwa vile ina maana akibadilika na kuwa mtu mzuri ni kosa. !! Inasemwa hata shetani akizeeka anakuwa Malaika !!
 
Ndio maana amejitokeza hadharani na kuyasema mapungufu aliyoyaona !! Tena amejitokeza hadharani bado akiwa humo humo kwenye kaya !! We learn through mistakes ! Ndivyo tulivyoumbwa !! Wote walikuwemo ndani ya kaya na mpaka sasa wote bado wapo ndani ya kaya !! Sio vibaya baadhi yao wakaanza kuyaona madhaifu yaliyokuwepo na bado yanaendelea kuwepo kama wanaona hivyo !! Hakuna mkamilifu ndivyo tulivyoumbwa !! Kakurwa integrity yake ipo palepale!!
 
kwa mifano na vielelezo ukatili, uuaji, ubambikiaji na ufungaji watu wa bashiru ally
An accomplice of Magufuli ......a person who helps another commit a crime. As long as alihudumu katika nafasi nyeti katika utawala wa kikatili wa magufuli, then naye anahusika kutenda hayo uliyoorodhesha! (au kwenye utawala wa magufuli hayakutokea?). He should have resigned to protest what was going on
 
Wooote waliomo ndani ya kaya ndio wale wale waliokuwemo kipindi cha mwendazake sio Bashiru pekee !!
 
Ni kweli kabisa !! Tunasubiri atoe ufafanuzi kwanini alinyamazia yale majambo !!
Ukiwa mtu wa Mungu, mkweli, muadilifu...unamwambia kuwa rafiki naomba kujiudhuru maana sitaki kuwa sehemu ya haya! (lakini njaa zetu hakuna wa kuacha Ukatibu Kiongozi, kama mbaya mbaya!) πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Uko sahihi kwa asilimia 100. Bashiru ni mnafiki hata kama ameongea ukweli. Lakini yeye ndio muasisi wa watu kuzuiwa kutoa maoni yao. Chini ya utawala wa kina Bashiru wetu ndio walikuwa wakitekwa, na chaguzi za nchi hii kunajisiwa.
Porojo michademi huwa hambebeki kila kitu kusingizia tu watu
 
Wwnyw chuki na bashiru hata akifanyaje wao hawatakakaa waridhike .wanajifanya wakamilifu ukiwaomba wakuonyeshe ukamilifu wao huwezi kuuona hata kidogo
 
Ukiwa mtu wa Mungu, mkweli, muadilifu...unamwambia kuwa rafiki naomba kujiudhuru maana sitaki kuwa sehemu ya haya! (lakini njaa zetu hakuna wa kuacha Ukatibu Kiongozi, kama mbaya mbaya!) πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
Ni shida Kwakweli
 
Wana mchango gani zaidi ya maigizo?
Butiku nA warioba hawajahi kukubali moyoni kuwa nje ya ruling system,, ndo maana tangu awamu ya nne wao wako against serikali,, waliopoa kidogo enzi za JPM maana yule hakuwa na cha msalie mtume,, WANGEPOTEAπŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…