PreGE2025 Bwege: CHADEMA wanadai haki, ACT tunaomba haki, CHADEMA wapo sahihi, Sisi ACT wanafiki

PreGE2025 Bwege: CHADEMA wanadai haki, ACT tunaomba haki, CHADEMA wapo sahihi, Sisi ACT wanafiki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Akizungumzia afya yake Mh.Bwege amesema Kwa sasa anaishi Kigamboni ili kuwa karibu na hospitali kwani anahitaji kusafishwa figo mara tatu kwa wiki kwani figo zake zimefeli na anahitaji kubadilisha akipata,Ikumbukwe pia alishakatwa mguu mmoja kutokana na kupata kidonda kisichopona sababu ya kisukari hivyo kulazimika kukatwa mguu.
Pole sana mzee Bwege, kuna wana CCM wapumbavu tu wale ndio wangekatwa figo akapewa huyu Mzee kuliko wale wanaCCM na Polisiccm wanaoteka watu kila siku na kujinadi hadharani
 
Akihojiwa mambo mbalimbali na kituo cha redio cha East Africa mbunge wa zamani Sulemani Bungara almaafufu Bwege amesema kwamba Chadema ndio chama makini zaidi Tanzania kwani wao wameamua kudai haki za wananchi kwa kuwa duniani kote haki haiombwi bali hudaiwa ila ACT wao wanaomba haki kwahio wanasubiri huruma za CCM kama watapewa jimbo moja au wasipewe hawana namna.

"Duniani kote tangu enzi za Adam, Ibrahim, Yesu na Mohammad haki haiombwi hudaiwa" Sijui unanielewa sijui unanielewa"alisema.

"Sisi ACT tunasema sijui usimuachie mwizi shamba,kwani si tumekuwepo tangu 2019,2020 na 2024 tuliambulia nini?sisi tunasubiri huruma tu ya CCM.

Aliongeza kusema hata kama Chadema haitashiriki,wakaweza kuishi miaka mitano bila ruzuku ikifika 2030 Chadema kitakuwa ndio chama chenye nguvu zaidi hapa Tanzania,"Na hawa jamaa ni wajanja,walijua kabisa njia wanaypita ni ngumu,wakaanzisha tonetone na watavuka bila hata ruzuku,mbona wakati vyama vinaanzishwa hakukuwa na ruzuku" alihoji.

Pia aliongeza " na tayari Kanisa na msikiti vinawaunga mkono,mtu yoyote mwenye akili atawaunga mkono,hata Mimi nawaunga mkono,sio kwamba nahama ACT hapana,ila nawaunga mkono sababu wanapigania haki yetu wote wala sina mpango wa kuhama chama"

Alipoulizwa juu ya Ukimya wa Mbowe akasema"Unajua hata yeye hakutegemea kushindwa na Lissu,imekuja ghafla tu,kwahio kukaa kimya ni sahihi ili ajue anarudijerudije au anatokakajetokaje" ila siasa inamuhitaji.

Sasa kama amewatanguliza watoto wake kama bata yeye anakuja nyuma tutajua maana kuna watoto wameenda chama fulani, kwahio tutajua kama ni bata kawatanguliza watoto au ni kuku,tutajua tutajua tu,haifiki mwezi wa nane tutajua lakini siasa inamuhitaji."

Kwa sasa Mheshimiwa Bwege anasema tutegemee kumuona jukwaani akiwanadi wagombe wa chama chake katika jimbo la Kusini kwakua yeye ni kiongozi na tayari wanachama wameanza kuchuakua fomu.

Akizungumzia afya yake Mh.Bwege amesema Kwa sasa anaishi Kigamboni ili kuwa karibu na hospitali kwani anahitaji kusafishwa figo mara tatu kwa wiki kwani figo zake zimefeli na anahitaji kubadilisha akipata,Ikumbukwe pia alishakatwa mguu mmoja kutokana na kupata kidonda kisichopona sababu ya kisukari hivyo kulazimika kukatwa mguu.

Tuendelee kumuombea.

#NRNE#
Akihojiwa mambo mbalimbali na kituo cha redio cha East Africa mbunge wa zamani Sulemani Bungara almaafufu Bwege amesema kwamba Chadema ndio chama makini zaidi Tanzania kwani wao wameamua kudai haki za wananchi kwa kuwa duniani kote haki haiombwi bali hudaiwa ila ACT wao wanaomba haki kwahio wanasubiri huruma za CCM kama watapewa jimbo moja au wasipewe hawana namna.📌📌📌🔨💪🏿✌🏿✌🏿✌🏿✌🏿
 
Bwege yuko sahihi sana, yeye alikuwa ni mbunge ambaye wananchi wake wengi mno walipata mateso makubwa zaidi ya kutekwa kuuawa huko mikoa ya kusini. Kwa hiyo namuelewa sana anapotaka haki idaiwe siyo iombwe!
Na anasema alishauri wasiingie kwenye uchaguzi ila ndio hivyo,inabidi akubaliane tu
 
Ameongea ukweli mtupu, kuna watu wanawafundisha cdm uoga eti kama hawatashiriki uchaguzi chama kitakufa. Yaani kama vile kiko hai kwa ajili ya kupata ruzuku.
 
Amejaribu kushauriana na Chama chake ? Na wanachotaka wao ni tofauti na wanachotaka wengine ? (Vipaumbele)?

Sababu hawa so called wapinzani wote naona wanapoteza ammunition zao kwa kupigana na kukanyagana wenyewe kwa wenyewe
 
Back
Top Bottom