PreGE2025 Bwege: CHADEMA wanadai haki, ACT tunaomba haki, CHADEMA wapo sahihi, Sisi ACT wanafiki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hawa Eisitii wanawajua vizuri CCM, siasa zao zinalenga maslahi yao zaidi
View attachment 3363200

Kada wa chama cha ACT Wazalendo, Said Bungara maarufu Bwege amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiko sahihi kudai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla haujafanyika, huku akikikosoa chama chake kwa alichokisema, kinaomba mabadiliko hayo.

Bwege aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini kwa miaka 10 (2010- 2020) kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya kuhamia ACT Wazalendo, ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha East Africa mapema wiki hii.

CHADEMA wanaendelea na kampeni yao ya No Reforms No Election (hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi) wakisema kama hakutakuwa na mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi mkuu wa 2025.
Chadema hawajawai kufanya vitu kwa pupa wanajielewa sana achana na hawa chama cha machawa
 
Bwege ni mkweli mno. Kwa kiufupi amesema hivi:-
A. Chadema ndiyo chama pendwa na chenye nguvu zaidi nchini kwa sasa kuliko vyama vyote .
B. Hata bila ruzuku chadema itaendelea kustawi kwakuwa inachangiwa na kila mtanzania mpenda haki.
C. ACT wanafiki, inaomba haki badala ya kuidai haki kama wafanyavyo chadema.
D. Haifiki mwezi wa 8 Mbowe atajionesha rangi yake
Hapo D namwomba sana Mbowe asiende huko kwenye ubwabwa huko hamna la maana!
 
Akihojiwa mambo mbalimbali na kituo cha redio cha East Africa mbunge wa zamani Sulemani Bungara almaafufu Bwege amesema kwamba Chadema ndio chama makini zaidi Tanzania kwani wao wameamua kudai haki za wananchi kwa kuwa duniani kote haki haiombwi bali hudaiwa ila ACT wao wanaomba haki kwahio wanasubiri huruma za CCM kama watapewa jimbo moja au wasipewe hawana namna.

"Duniani kote tangu enzi za Adam, Ibrahim, Yesu na Mohammad haki haiombwi hudaiwa" Sijui unanielewa sijui unanielewa"alisema.

"Sisi ACT tunasema sijui usimuachie mwizi shamba,kwani si tumekuwepo tangu 2019,2020 na 2024 tuliambulia nini?sisi tunasubiri huruma tu ya CCM.

Aliongeza kusema hata kama Chadema haitashiriki,wakaweza kuishi miaka mitano bila ruzuku ikifika 2030 Chadema kitakuwa ndio chama chenye nguvu zaidi hapa Tanzania,"Na hawa jamaa ni wajanja,walijua kabisa njia wanaypita ni ngumu,wakaanzisha tonetone na watavuka bila hata ruzuku,mbona wakati vyama vinaanzishwa hakukuwa na ruzuku" alihoji.

Pia aliongeza " na tayari Kanisa na msikiti vinawaunga mkono,mtu yoyote mwenye akili atawaunga mkono,hata Mimi nawaunga mkono,sio kwamba nahama ACT hapana,ila nawaunga mkono sababu wanapigania haki yetu wote wala sina mpango wa kuhama chama"

Alipoulizwa juu ya Ukimya wa Mbowe akasema"Unajua hata yeye hakutegemea kushindwa na Lissu,imekuja ghafla tu,kwahio kukaa kimya ni sahihi ili ajue anarudijerudije au anatokakajetokaje" ila siasa inamuhitaji.

Sasa kama amewatanguliza watoto wake kama bata yeye anakuja nyuma tutajua maana kuna watoto wameenda chama fulani, kwahio tutajua kama ni bata kawatanguliza watoto au ni kuku,tutajua tutajua tu,haifiki mwezi wa nane tutajua lakini siasa inamuhitaji."

Kwa sasa Mheshimiwa Bwege anasema tutegemee kumuona jukwaani akiwanadi wagombe wa chama chake katika jimbo la Kusini kwakua yeye ni kiongozi na tayari wanachama wameanza kuchuakua fomu.

Akizungumzia afya yake Mh.Bwege amesema Kwa sasa anaishi Kigamboni ili kuwa karibu na hospitali kwani anahitaji kusafishwa figo mara tatu kwa wiki kwani figo zake zimefeli na anahitaji kubadilisha akipata,Ikumbukwe pia alishakatwa mguu mmoja kutokana na kupata kidonda kisichopona sababu ya kisukari hivyo kulazimika kukatwa mguu.

Tuendelee kumuombea.

#NRNE#
Hayo matatizo ya ugonjwa yamemfanya mtu aliyekata tamaa. Huwezi kuwa mwanachama wa ACT bado unafagilia mwenendo wa Chadema, huyo amechanganyikiwa
 
huyu mzee amechanganyikiwa, Lakini matatizo ya ugonjwa alionao ndio chanzo
 
Huyu bwana huwa namkubali si mnafiki wala masaka tonge kama zitto kabwa
 
HUYO NDO ,akina Newton wakileo ,lasaba tu mawazo yake Meli inaelea juu yamaji na haizami inatoka tz hadi china
 
Back
Top Bottom