PreGE2025 Bwege: CHADEMA wanadai haki, ACT tunaomba haki, CHADEMA wapo sahihi, Sisi ACT wanafiki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Kada wa chama cha ACT Wazalendo, Said Bungara maarufu Bwege amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiko sahihi kudai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla haujafanyika, huku akikikosoa chama chake kwa alichokisema, kinaomba mabadiliko hayo.

Bwege aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini kwa miaka 10 (2010- 2020) kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya kuhamia ACT Wazalendo, ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha East Africa mapema wiki hii.

CHADEMA wanaendelea na kampeni yao ya No Reforms No Election (hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi) wakisema kama hakutakuwa na mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi mkuu wa 2025.
 
Ameongea ukweli mtupu, kuna watu wanawafundisha cdm uoga eti kama hawatashiriki uchaguzi chama kitakufa. Yaani kama vile kiko hai kwa ajili ya kupata ruzuku.
Chama hakiwezi kufa,hao ni wale machauma ndio kauli zao
 
Amejaribu kushauriana na Chama chake ? Na wanachotaka wao ni tofauti na wanachotaka wengine ? (Vipaumbele)?

Sababu hawa so called wapinzani wote naona wanapoteza ammunition zao kwa kupigana na kukanyagana wenyewe kwa wenyewe
Kushauriana kuhusu nini?Alishawashauri viongozi juu ya wao kutoshiriki uchaguzi ila wakawa na mawazo tofauti,kwahio akawa hana namna
 
mambo yamebadilika sana, yaani hatuangazii utendaji tena sisi ni mwendo wa mitano tena, pia hatujisumbui kuchuja kipi kinafaa sisi, ni kutiki tu, Mungu atusamehe mara ngapi?
 
Kushauriana kuhusu nini?Alishawashauri viongozi juu ya wao kutoshiriki uchaguzi ila wakawa na mawazo tofauti,kwahio akawa hana namna
Kwahio kama kuna mawazo tofauti na ulionao unasubiri nini kutoka huko ulipo ili kuungana na wenye mawazo kama wewe ?

Better still kwanini usipigie chapuo Mgombea binafsi ili hata ukiwa na mawazo yako ya pekee uweze kwenda nayo bila kushurutishwa na Herd Mentality...

After all Vyama vya Siasa ni Muunganiko wa watu wenye Fikra na Itikadi sawa ili kuunganisha Sauti zao ziweze kusikika vema kuliko mmoja mmoja
 
Hili swali lako anayepaswa kujibu ni Bwege mwenyewe,kuhusu mgombe binafsi nadhani unajua kwamba kuna kesi mtu alishinda mahakama ya Afrika mashariki na Tanzania ikaamuriwa itekeleze kama sikosei,sijui imefikia wapi
 
Mtikila alishinda Mahakamani kwamba ni kweli inavunja Katiba Bunge likaja kubadilisha sheria retrospectively.., ila ndio hivyo hata hivi Vyama zaidi ya Mtikila hakuna anayepigia kelele hii issue; Kuna kipindi ilibidi Mtikila ajiunge na CHADEMA ili tu aweze kugombea Ubunge ila ndio hivyo ndoa yao baada ya kukosa Ubunge ikawa chungu (akaja na Kauli kuna CHADEMA chumbani na Sebuleni); Kumbuka kwa kipindi kirefu sana Mtikila alikuwa ananyimwa hati ya kwamba ni Chama cha Siasa kwa kukosa representatives Visiwani....

Anyway point yangu kuu kama upo kwenye Chama inabidi kuendana na msimamo wa Chama chenu au kujitoa zaidi ya hapo ni kuleta Chaos ambayo haijengi zaidi ya kunufaisha Chama Tawala...
 
Sawa
 
file_00000000a19c61f7a8a31c72919aef6b.png
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiko sahihi kudai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla haujafanyika, huku akikikosoa chama chake kwa alichokisema, kinaomba mabadiliko hayo
Hawa Eisitii wanawajua vizuri CCM, siasa zao zinalenga maslahi yao zaidi
 
Back
Top Bottom