CAF Confederation Cup yafutwa. Msimu ujao kutakuwa na mashindano mawili tu

Nafikiri hii sasa imekuja kuua soka na sio kuleta ushindani.
 
Kwa mpira wa bongo jinsi watu walivyo wapuuzi soon wataanza kuidharau champions league mana wale wakubwa wote simba na Yanga watakuwa wanacheza AFL

Ila sio mbaya ili hata akina Azam nao waonje utamu wa champions league 😂
 
Kutakua na makundi??
 
Kumbe umesema kunaweza kusiwe na cafccl bado huna hukakika ila Kama yanav watashiriki lzm afike fainali
 
Duh una uhakika mzee au utapeli tu
 
Sasa kama issue ni point na hao simba et al hawashiriki CAFCL inakuaje miaka ya mbeleni watabaki vipi na hizi timu zinazoongeza point zitaishia wapi?
 
Kumbe umesema kunaweza kusiwe na cafccl bado huna hukakika ila Kama yanav watashiriki lzm afike fainali
Hakuna mashindano yanaitwa cafccl. Cafccl ndio maanake nini? Mkuu muda ni mwalimu mzuri. Hayo mashindano ya Cafcc tokea mwezi wa kwanza raisi wa CAF alisema anaweza kuyafuta kutokana na kuwepo na mashindano matatu hakuna pesa za kutosha kuyaendesha na pia ratiba inabana. Ila kwasasa ni rasmi yamefutwa hayo mashindano.
 
Yanga itaingia kwa Mgongo wa Simba, sababu kuu ni Kupata Mashabiki ambao ni base kubwa kwa Simba.
 
kwahio kuna uwezekano timu moja ipo CAF na same time ipo ACL, na same time anatakiwa kucheza NBC,mapinduzi, azam federation ...

Mkuu hujamalizia kuusoma uzi wote?

Mwishoni kabisa, jamaa kaandika kama ifuatavyo...

Ikumbukwe msimu ujao kunaweza kukawa na mashindano mawili pekee AFL na CAFCL) na haipaswi timu kushiriki mashindano yote mawili.
 
Hongera Sana mkuu Kwa ufafanuzi murua Sana Heko. [emoji119]

Naona kuna watu bado hawajaelewa timu zikavoshiriki AFL... Ingawa umefafanua vizuri kua n zile zilizo Rank ya juu CAF Kupitia Shirikisho la soka la ukanda husika...

Pia umeeleza vizuri sasa rasmi AFL ndo kutakua kunakutanisha vigogo wa soka Afrika maana ni only top ranking team Katika Miaka Mitano ya michuano ya CAF ila sijajua na huko AFL kutakua kunatoa pointi au vipi...?

Sasa rasmi CAF champions League itakua inashirikisha team zile zilizokua kombe la Shirikisho hivo kombe la Shirikisho automatically litakua halipo....

Japo naona wangeliacha kama ulaya walivo na michuano mitatu yaani UEFA, EUROPA Na CONFERENCE....
Na Sisi tungekua na AFL, Champions League na Confederation cup...

Ila sio mbaya tusubiri msimu mpya najua utakua wa Moto Sana....
 
Mkuu hujamalizia kuusoma uzi wote?

Mwishoni kabisa, jamaa kaandika kama ifuatavyo...
ilikua imenichanganya kidogo maaana ukisema CAFCL kidogo kuna uzito ila apa inachukuliwa kama shirikisho tu
 
Yanga itaingia kwa Mgongo wa Simba, sababu kuu ni Kupata Mashabiki ambao ni base kubwa kwa Simba.
Yanga itaingia kwa mgongo wake wenyewe kwasababu point 16 alizipata kwa kufika fainali cafcc na point 15 amezipata kwa kufika robo fainali cafcl ikamfanya awe na point za kutosha kushiriki AFL akiwa na jumla ya point 31.
Swala la mashabiki sio kigezo kikubwa kwasababu Mamelodi tu kule pamoja na ubora wao lakini inafahamika mashabiki hawana. Japo ukweli Yanga ina mashabiki wengi sana tofauti na unavyowaza wewe.
 
Raisi wa CAF alisema tatizo ni gharama za kuendesha mashindano
 
MFano yanga na simba wana vigezo vya kushiriki AFL na ndio top 2 ya ligi kuu maana yake uko CAF ataenda Azam alieshika nafasi ya tatu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…