CAF wametumia vigezo gani kupata timu katika mashindano ya Africa Football league (AFL)

Usimba na uyanga ni tatizo sana. Yaani ukiingia damuni mtu hata akili anaziweka kando.
 
Mleta uzi hana mashaka na Simba bali ameomba ufafanuzi kuhusiana na Enyimba.
 
Tupe timu hapa ambazo ww unadhani zilistahili kuwepo.
 
Wewe Yanga unatakiwa uingie huko kwa kigezo kipi.?

Ni vyema ungejikita hapa ili utushawishi kutukuelewe kuwa Simba Sc kapendelewa.
Kwa hiyo nyie mnawazidi Raja casablanca
Hilo ni bonanza tu
 
Wewe Yanga unatakiwa uingie huko kwa kigezo kipi.?

Ni vyema ungejikita hapa ili utushawishi kutukuelewe kuwa Simba Sc kapendelewa.
Kwa hiyo nyie mnawazidi Raja casablanca
Hilo ni bonanza tu
 
Kwa hiyo nyie mnawazidi Raja casablanca
Hilo ni bonanza tu
Kwa ukanda huo amechukuliwa WYDAD, ningekuona ufikiri vizuri kama ungeleta hoja ya kwanini kwa ukanda ule kachukuliwa Wydad mbele ya Raja, kitu abacho ni wazi kuwa Wydad kamzidi parefu sana Raja.


Team zimechaguliwa kwa ukanda, na kwa ukanda wa Africa Mashariki imeonekana Simba, kule magharibi ikaonekana ENYIMBA, Kusini ikaja MAMELOD Nk.


Kama ni hoja ya kupinga, inatakuwa upinge kwa kupendekeza "kanda fulani ilitakiwa team fulani kwa vigezo fulani" sio kwa hizo hoja zako.
 
Kwanini Enyimba na sio Asec Mimosa ama Rivers united?
 
Kwanini Enyimba na sio Asec Mimosa ama Rivers united?
Vigezo ni vitatu, Udadi ya mashabiki na muitikio wao viwanjani, Ushiriki mashindano ya CAF vilabu na hatua zinazofikiwa na team husika, history and Legacy.


Ili mambo yakae vizuri ni lazima utafutwe uwiano mzuri wa hizo sifa kwa kila club. ASEC na RIVERS zipo vizuri zikilinganishwa na ENYIMBA lakini kibiashara bado sio machaguo mazuri (hawawezi kulipa) kutokana idadi yao ya mashabiki na muamuko wao kuja viwanjani wanapolinganishwa na Enyimba.


Ukiutafuta uwiano wa hizo sifa kwa Enyimba kidogo unapatikana. Nikimaanisha ndani ya miaka hii mitano huku CAF wanashiriki na wanafika hatua zinazoonekana japo si sawa na hao wengine uliowataja, Wana mashabiki wengi hivyo watazalisha pesa, lakini pia wana Legacy kubwa inayowafanya wajulikane kwa wengi kuliko hao uliowataja hivyo ni rahisi kuvuta attention ya wafuatiliaji.....nk.


Haya sio mashindano ya kuchezesha uwanja ukiwa mweupe.Kwa ukanda wetu huu, kama sio Simba Sc basi Yanga ingefaa kutokana na kukidhi hivyo vigezo, tatizo ni kwenye hicho kigezo cha ushiriki wa mashindano ya CAF vilabu, ni wazi kuwa Simba Sc yupo mbele ya Yanga (kama hautaendekeza ushabiki) sasa kwakua vingine vyote Simba na Yanga wanalingana, hicho ndio kikafanya Simba Sc iwe hapo.


Tujaadili kwa hoja bila kuendekeza USHABIKI, leta hoja nyingine.
 
Bora umeweka vigezo vitatu humu wengi wamechukulia kama mashindano ya vipanga vya CAF. Kumbe kuna ishu zingine zitakazovutia kibiashara na sio ubora pekee.
 
Bora umeweka vigezo vitatu humu wengi wamechukulia kama mashindano ya vipanga vya CAF. Kumbe kuna ishu zingine zitakazovutia kibiashara na sio ubora pekee.
Ukilijadili hili swala kwa kutanguliza ushabiki, halifiki mwisho. Ni lazima utembee na vigezo vyote vitatu bila kuacha hata kimoja.

Simba na Yanga wamelingana kwa kila kitu (mashabiki & Legacy ) ila wamekuja kutenganishwa na ushiriki na hatua waliofika kila mmoja kwenye mashindano ya CAFCL ndano ya hii mitano.


Sasa hapo ukitaka Yanga iwekwe kwakuwa watajaza watu pia basi ujue hata kule South Kizer na Orlando zitaomba pia, pale Sudani Hilal na Merreikh wataleta mgogoro, pale Morocco Raja nae atataka, Egypty Zamalek atataka, Algeria Belouzidad watataka yaani itakuwa ni mzozo.


Sasa kama hayo mafanikio ya Simba Sc huko CAFCL ikilinganishwa na Yanga ndio yanayowapa haki mashabiki wa Simba Sc kijiita vipanga mbele ya Yanga Sc, sina cha kuchangia.
 

Sijui Simba kaingiaje kwenye huu mjadala, swala lilikuwa ni Enyimba na kwa maelezo yako ni kwamba kwa mafanikio ya miaka mitano Enyimba hampati Rivers na Asec Mimosa ila tu sababu ya kigezo cha mashabiki ndio kimewaondoa Asec na Rivers. Enyimba ameingia kwenye mashindano sio kwa rank ya 5 years bali ni kwa vibe la mashabiki na ndio maana nikasema sio mashindano ya vipanga pekee yao.
 
Ungezingatia heading na mada ya muanzisha uzi wala usingeuliza Simba Sc imeingiaje hapa, hoja sio ENYIMBA, hilo la Enyimba limeletwa na nyinyi wachangiaji.

Hoja ni vigezo vilivyotumika kuchagua team AFL, sasa kama unadhani Simba Sc haihusiki kwenye hizo team, hilo sio tatizo langu.
 
Nanukuu "Ningependa kujua vigezo vilivyotumiwa na Caf kuanzisha haya mashindano kwa sababu kama wamechukua timu bora kila ukanda Kwa hivi sasa Rivers ni bora kuliko Enyimba"
 
Kujizungushazungusha tu lakini hapo ndiyo hasa wanalenga.[emoji23]
Ukweli usemwe Yanga wanaumia sana sana sana.
Kuona Simba inaangaliwa na Dunia nzima kwenye Super Cup.

Kibaya zaidi tarehe 20 inafungua mechi na Bingwa wa Afrika.
Kibaya zaidi mechi mechi inachezwa Tanzania.
Kibaya zaidi Simba inajitangaza duniani kote.

Kibaya zaidi wadhamini wa mpira wa miguu na viongozi wa mpira wa Dunia nzima wapo Tanzania na wataangalia game ya Simba.

Kibaya zadi kwa hizi wiki mbili Yanga haitajwi kabisa na Vyombo vya habari wakiwemo wacha-mbuzi wao Uchwala.

Hapo ndio mjue kuwa Simba ni Damu yenu Nyekundu, ipo katika kila mwili wa mtu.
 
Nanukuu "Ningependa kujua vigezo vilivyotumiwa na Caf kuanzisha haya mashindano kwa sababu kama wamechukua timu bora kila ukanda Kwa hivi sasa Rivers ni bora kuliko Enyimba"
Kawaulize hao CAF, au hujui Website Yao.
Wacha kusumbua watu humu wakati unajua jinsi ya kuwauliza CAF.
 
Ningependa kujua vigezo vilivyotumiwa na Caf kuanzisha haya mashindano kwa sababu kama wamechukua timu bora kila ukanda Kwa hivi sasa Rivers ni bora kuliko Enyimba
Walitumia CAF Ranking kwa msimu wa 2022/2023.

Kwa kila confederation.

COSAFA Sundowns na Petro
UNAF Al Ahly, Wydad na Esperance
West Africa kwenye category ilikuwa Horoya, Lobi Stars, Enyimba, Cotton Sports na Asec Mimosas kwenye raking na vigezo vingine vya Club licensing Enyimba akaqualify.

Central Mazembe na CECAFA Simba alikidhi vigezo vya Club licensing vingi kulinganisha na zingine plus Caf Ranking
 
Yanga ambayo kwa miaka 25 haijawahi kushiriki tu japo makundi champions league au kuna yanga nyingine
Club zisizokuwa na malengo, yaani miaka 25 unapelea timu uwanjani - kuingia makundi ya mabingwa Africa hola ? kweli.

Miaka 25 ni umri wa mtu tena mwenye mji wake kabisa sheikh...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…