Vigezo ni vitatu, Udadi ya mashabiki na muitikio wao viwanjani, Ushiriki mashindano ya CAF vilabu na hatua zinazofikiwa na team husika, history and Legacy.
Ili mambo yakae vizuri ni lazima utafutwe uwiano mzuri wa hizo sifa kwa kila club. ASEC na RIVERS zipo vizuri zikilinganishwa na ENYIMBA lakini kibiashara bado sio machaguo mazuri (hawawezi kulipa) kutokana idadi yao ya mashabiki na muamuko wao kuja viwanjani wanapolinganishwa na Enyimba.
Ukiutafuta uwiano wa hizo sifa kwa Enyimba kidogo unapatikana. Nikimaanisha ndani ya miaka hii mitano huku CAF wanashiriki na wanafika hatua zinazoonekana japo si sawa na hao wengine uliowataja, Wana mashabiki wengi hivyo watazalisha pesa, lakini pia wana Legacy kubwa inayowafanya wajulikane kwa wengi kuliko hao uliowataja hivyo ni rahisi kuvuta attention ya wafuatiliaji.....nk.
Haya sio mashindano ya kuchezesha uwanja ukiwa mweupe.Kwa ukanda wetu huu, kama sio Simba Sc basi Yanga ingefaa kutokana na kukidhi hivyo vigezo, tatizo ni kwenye hicho kigezo cha ushiriki wa mashindano ya CAF vilabu, ni wazi kuwa Simba Sc yupo mbele ya Yanga (kama hautaendekeza ushabiki) sasa kwakua vingine vyote Simba na Yanga wanalingana, hicho ndio kikafanya Simba Sc iwe hapo.
Tujaadili kwa hoja bila kuendekeza USHABIKI, leta hoja nyingine.