Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limependekeza posho ya kila mwaka ya dola za Kimarekani 50,000 sawa na Shilingi Milioni 136.5 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu vya Afrika (African Club Association - ACA). Pendekezo hilo litajadiliwa kwenye Mkutano wa 46 wa Kawaida wa CAF, unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia mnamo Oktoba 22.
Mwenyekiti wa ACA, Engineer Hersi Said kutoka Tanzania, amepewa jukumu la kuongoza chama hicho ambacho kinalenga kuimarisha ushirikiano na maendeleo ya vilabu vya soka barani Afrika. Hatua hii imeelezwa kuwa muhimu katika kuinua viwango vya soka la vilabu na kushirikisha wadau mbalimbali kwenye sekta hiyo.
Soma zaidi: Engineer Hersi ashinda Uenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika African Clubs Association, hongera kijana
Soma zaidi: Engineer Hersi ashinda Uenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika African Clubs Association, hongera kijana