CAF Yapendekeza Hersi Said apate posho ya Milioni 136.5 kwa mwaka kama Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu vya Afrika

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limependekeza posho ya kila mwaka ya dola za Kimarekani 50,000 sawa na Shilingi Milioni 136.5 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu vya Afrika (African Club Association - ACA). Pendekezo hilo litajadiliwa kwenye Mkutano wa 46 wa Kawaida wa CAF, unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia mnamo Oktoba 22.
CAF EXCO MEETING - NAIROBI, KENYA.Imekuwa ni baraka kwangu kuhudhuria mkutano wa CAF EXCO ulio...jpg
Mwenyekiti wa ACA, Engineer Hersi Said kutoka Tanzania, amepewa jukumu la kuongoza chama hicho ambacho kinalenga kuimarisha ushirikiano na maendeleo ya vilabu vya soka barani Afrika. Hatua hii imeelezwa kuwa muhimu katika kuinua viwango vya soka la vilabu na kushirikisha wadau mbalimbali kwenye sekta hiyo.
1727703242047.png

Soma zaidi: Engineer Hersi ashinda Uenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika African Clubs Association, hongera kijana
 
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limependekeza posho ya kila mwaka ya dola za Kimarekani 50,000 sawa na Shilingi Milioni 136.5 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu vya Afrika (African Club Association - ACA). Pendekezo hilo litajadiliwa kwenye Mkutano wa 46 wa Kawaida wa CAF, unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia mnamo Oktoba 22.
Mwenyekiti wa ACA, Engineer Hersi Said kutoka Tanzania, amepewa jukumu la kuongoza chama hicho ambacho kinalenga kuimarisha ushirikiano na maendeleo ya vilabu vya soka barani Afrika. Hatua hii imeelezwa kuwa muhimu katika kuinua viwango vya soka la vilabu na kushirikisha wadau mbalimbali kwenye sekta hiyo.

Soma zaidi: Engineer Hersi ashinda Uenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika African Clubs Association, hongera kijana
Kwa Afrika hii, ngoja watu waanze kurogana! Huo mpunga, sio mchezo!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
kwani hio nafasi ni miaka mingapi inamaana kama ndo wanajadili malipo ndio kusema wenyeviti waliopita kabla ya hersi hawakuwa wakilipwa.!
 
Kwa hiyo yeye ni mwenyekiti wa vilabu vinavyoshiriki champions lg?
Motsepe mwenywe hakujua kama simba walicheza na Al Ahly Tripoli hadi kufanyia vurugu, we utajuaje ya Hersi? Subirini mshiriki CL ndio mtaona kazi yake
 
Back
Top Bottom