CAG aongea na waandishi wa habari - Aprili 8, 2021

CAG aongea na waandishi wa habari - Aprili 8, 2021

CAG. CAG soon anatumbuliwa wote hamtoamini.
 
Je? viongozi wetu wanajitafakari juu ya Ripoti hiii ambayo imefichua ubadhirifu na uozo mkubwa!

Viongozi wetu wenye dhamana je mtaamua kufumba macho lipite au mtachukua hatua?

kwakweli sisi watanzania walipa kodi tumeshituka sana juu ya ubadhirifu huu,
tunaomba wahusika wote ktk kila idara au sekta hatua za haraka zichukuliwe bila kuchelewa maana ushahidi huo hapo CAG report.

TAKUKURU msisubiri kutafuta ushahidi mwengine, repoti ya CAG ni ushahidi kamili hivyo tunaomba mchukue hatua haraka kwa kila mhusika
 
CAG Kicheere anaongea na waandishi wa habari muda huu.

Updates;
========

CAG: NILIBAINI WAKALA NNE ZA SERIKALI ZILIKUWA ZINADAIWA BILIONI 783.39

TANROADS ilikuwa na deni kubwa lenye thamani ya bilioni 770.1 kutoka kwa wakandarasi na wahandisi washauri kutokana na kuchelewa kupata fedha za kutekeleza miradi kutoka hazina, wakala wa majengo bilioni 1, RUWASA bilioni 12 na TARURA milioni 125

-Ni madeni ya wakandarasi, watoa huduma na washauri katika hizo taasisi nne

CAG: MIRADI INAYOTEKELEZWA INA TOZO YA RIBA YA BILIONI 14.9

Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali(CAG) amesema miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ina riba ya bilioni 14.9 kama adhabu ya kuchelewesha kulipa hati za madai ya wakandarasi kinyume na masharti ya mikataba

-CAG amesema malipo hayo hayana tija kwani yangeweza kuepukika kwani baadhi ya pesa ni za wafadhili ambazo zipo lakini mlolongo mrefu wa malipo kwa serikali unakwamisha

MALIASILI NA UTALII

CAG: Nilifanya ukaguzi maalum wizara ya maliasili na utalii, nilibaini bilioni 6.8 zililipwa kutoka kwenye mfuko wa tozo ya maendeleo ya utalii bila idhini ya afisa masuuli kinyume na kanuni ya fedha. Pamoja na haya nilibaini matumizi ya jumla ya bilioni 16 yalifanyika bila kuwa na hati za malipo pia yalibainika matumizi ya bilioni 11 ambayo hayakuwa na nyaraka toshelezi na milioni 89 zilizotumiwa na makumbusho ya Taifa kwa matumizi yasiyoendana na shughuli za utalii.

Kwa maoni yangu mkurugenzi wa utalii na mhasibu waliokuwa wanahusika walitumia vibaya fedha za tozo ya utalii jumla ya Tshs Bilioni 34

CAG: BODI YA WAKURUGENZI YA ATCL HAINA MJUMBE MWENYE UZOEFU NA MASUALA YA ANGA

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema hayo na pia kuongeza kuwa Shirika linadaiwa hivyo inakuwa changamoto kuruka kwenye baadhi ya maeneo

Pia Viwanja vya Ndege vimetajwa kuwa na changamoto
TAKUKURU anzeni na taarifa hii hapa ya CAG Kicheere. Huyu mtu wa matunguli kutoka Nzega alitumia madaraka vibaya katika matumizi ya tamasha la Urithi.

Msisubiri maelekezo ya Rais kumkamata Kigwangala, sheria yenu inawapa nguvu
 
Back
Top Bottom