CAG kwa hili sijui kama yuko sahihi Mapori yaliyoko Kule mijambazi ya Rwanda na Burundi ilikuwa inasumbua sana
Magufuli akatangaza kuwa yale maeneo ni mbuga za taifa sababu kuonekana mbugani kama sio mtalii unapigwa risasi .umefuata nini mbugani
Kwa kuanzisha mbuga akawa kakomesha utekwaji magari na mabasi kwenye yale Mapori sababu majambazi wanyarwanda na warundi walijikatia mapori yale wengine wakaanzisha hadi mashule na vituo vya ujambazi .Tatizo hilolimekuweko Serikali zote Magufuli Ndie alibadilisha hiyo hali
Tatizo Serikalini coordination hamna kilichotakiwa ni wizara zote kushirikiana ku push agenda ya utalii kule ili uwanja uwe active
Lakini pia Jeshi huo uwanja ungewasaidia!!
Sasa tuchukulie mfano Serikali iseme hauna faida ufungwe wanatakaje na zile mbuga zifungwe wanyama warudishwe walikotoka na mapori yale waachiwe Majambazi wa kinyarwanda na kirundi waendelee kuteka mabasi na magari na Kuua raia?
Anyway huo ni uamuzi wa Serikali
Ila Nadhani siku ingine CAG akifanya ukaguzi ni vizuri kupata information za kutosha zaidi ya hizo za profit and loss