Mpigania uhuru wa pili
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 3,380
- 6,376
Muhammad alishushiwa quran na Allah ila cha ajabu baadhi ya waislamu wameachana na quran wamejikita kwenye biblekwani ndani ya biblia imeandikwa ni marufuku kusomwa na mtu asiye mkristo ?? halafu unatetea biblia ipi iliyo yako ?? QJV, KJV, NKJV, NIV, Douay, au maelfu ya biblia tofauti ??
Wasichana wenu wa kijahidina wameona isiwe tabu, wameamua kula Raha na muziki na kukata mauno; to hell na Hijabu zenu
View: https://x.com/nyuki_malkia/status/1760585124142309529?s=20
Elewa kwanza maana ya neno Gaidi.
Muhammad alishushiwa quran na Allah ila cha ajabu baadhi ya waislamu wameachana na quran wamejikita kwenye bible
Unaamisha magoliMungu - wa biblia
"Mimi naiumba nuru, na kulihumba giza; mimi nafanya amani, na kuumba uovu; ( Isaya 45:7 )
"Na kwa sababu hiyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo." (2 Wathesalonike 2:11)
Yeremia Nabii wa Mungu analia kwamba alidanganywa na Mungu.
"Ee BWANA, umenidanganya, nikadanganyika; wewe una nguvu kuliko mimi, nawe umeshinda; mimi ni kitu cha kudhihakiwa kila siku, kila mtu hunidhihaki." ( Yeremia 20:7 )
Unaamisha magoli
Umechoka kukariri quran umeamua kutumia biblia
Umechoka kukariri quran umehamia kwenye bibliaJe, Yesu alihitaji kufa?
Mwana wa Adamu alikuwa na "mamlaka duniani ya kusamehe dhambi" (Mk. 2:10)
na Yesu tunaambiwa alisamehe dhambi za mtu aliyepooza (Mk. 2:5),
na mwanamke mwenye chupa ya alabasta (Luka 7:48).
Basi kwa nini Yesu alipaswa kufa ili atukomboe kutoka katika dhambi?
Umechoka kukariri quran umehamia kwenye biblia
Umechoka kukariri quran umeahamia kwenye bibliaUfufuo au Uasi ?????
Mathayo 10
34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali vita.
Luka 22:36 SRUV
Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho lake akanunue.
Tutafika tu , HAPA KAZI TUUUU
Umechoka kukariri quran umeahamia kwenye biblia
Umechoka kukariri quran umeahamia kwenye biblia
Muislamu uliyeshindwa kukariri quran umehamia kwenye bibliaKifungu kingine cha maneno ya Biblia kinachonukuliwa mara nyingi kutilia nguvu imani ya kuokoka kwa damu ya Yesu ni hiki kutokana na Luka:
Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
Luka 1.67-71
Bishara hii ni ya Zakaria alipozaliwa mwanawe Yohana (Nabii Yahya).
Lakini ni wazi kuwa anasema ni Bwana Mungu ndiye aliyewaokoa watu wake kwa "kuwasimamishia pembe ya wokovu", naye ni Masihi aliyekuwa akitarajiwa na Mayahudi kuja kuwakomboa kutokana na adui zao wanaowachukia, nao ni watawala wa Kirumi.
Kuja huyo mwokozi, anasema Zakaria, ni kutimiza yale maneno waliyoyasema manabii wa zamani.
Ni kuyapotoa maana ya maneno tukifasiri utabiri huu kuwa maana yake ni kuokolewa kwa damu ya Yesu.
Umechoka kukariri quran umehamia kwenye bibliaInjili ya Marko inasema:
Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa watu wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Marko 10.42-45
Kifungu hicho nilichokinukuu ni moja katika ushahidi unaotolewa katika thiolojia (ilimu ya Ungu) ya Kikristo kuthibitisha imani ya kuwa Yesu kaja duniani auwawe na damu yake iwe ni kafara au fidia kwa dhambi za wanaadamu.
Hebu natukiangalie vyema kifungu hichi, chasema nini?
- Yesu anasema "hakuja kutumikiwa bali kutumika", licha kuabudiwa.
- Maneno yasemayo: "kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi" ni wazi kuwa ni mfano, kama usemi: "anayetaka kuwa wa kwanza, atakuwa mtumwa wa wote." Bila ya shaka hapana atakayeona kuwa Yesu alikusudia kwa neno "mtumwa" ni kiumbe wa kuuzwa na kununuliwa. Hali kadhaalika "kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi" sio maana yake lazima kuuwawa.
- Tafsiri ya Biblia The Interpreter's Bible inasema wazi juu ya kauli hiyo ya Yesu kuwa haiwezekani kuitumia kuwa ni ushahidi wa thiolojia ya Paulo ya kuokoka kwa damu.
- Kauli hii lazima ichukuliwe kama ni mfano, kama usemi wa kishairi, kama ni mshabaha.
- Wako baadhi ya wataalamu wa Kikristo ambao wanasema kauli hii ama iliongezwa na Marko au na mtu mwenginewe baadae, lakini Yesu hakusema hayo. Lakini wenye kuandika hiyo tafsiri ya Biblia wanaona kwamba maneno hayo kayasema Yesu na yana maana ya mfano kama "vile mashahidi wa Kiyahudi walivyokufa kwa kuwaokoa watu wao (II Macc. 7.37-38; IV Macc. 17.22)" Ikiwa maana yake ni hivyo wanaona wafasiri wa Interpreter's Bible yaweza kuwa kauli hiyo ni kweli ya Yesu, kama ikichukuliwa maana nyengine haiwezi kuwa ni kweli.
Ikiwa basi Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi za watu, na ikiwa kweli yeye ni Mungu, basi mambo yote hayo ni kama sarakasi tu, mchezo wa kuigiza, au kiini macho.
Kwani hakika Mungu hawezi kuwa aliona uchungu kwa yale mateso, na kufa kwake kulikuwa hakuna maana, kwani kumbe hakufa.
Mungu hufa?
Yote hayo yaonyesha kuwa ni udanganyifu mkubwa.
Na ikiwa yote hayo yalikuwa yamekwisha kadiriwa tangu mwanzo na kupangwa na kutimiza bishara za kinabii na kwa kupenda kwake Yesu, basi hao waliomtesa na wakamwua yafaa wafikiriwe na watukuzwe kama ni watu wema waliowaletea heri wanaadamu wote, na wakamsaidia Yesu kutimiza lile alilolijia.
Hao akina Yuda, na Pilato, na lile baraza la wakuu wa Kiyahudi, wote hao ndio vipenzi vya Mungu, waliotimiza mapenzi ya Mungu baraabara.
Tutafika tu , HAPA KAZI TUUUU
Muislamu uliyeshindwa kukariri quran umehamia kwenye biblia
Biblia moja ya kitabu pendwa sana waislamu wameacha quran wanatumia biblia Ahsante yesuUshahidi mwingine unaodaiwa kuwa ni dalili ya uwokovu kwa damu ni huu
Siku ya pili yake (Yohana Mbatizaji) amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
Yohana 1.29
Hata tukijaalia maneno haya ya Injili ya Yohana ni kweli (kwani hayathibitishwi na Injili zote nyenginezo) basi si kama tunavyomtaja kiongozi ye yote wa kidunia hivi leo kwa kusema: "Muangalieni huyo anayetubebea mizigo yetu yote"?
Au tunapomwonya mmoja wetu: "Baba, utajiua nafsi yako kutaka kujitwika mambo ya ulimwengu mzima kwenye mabega yako hayo!"
Kuchukua dhambi si lazima iwe maana yake ni kusamehewa dhambi kwa kuuliwa Yesu; bali ni kwa kuyafuata mafunzo yake na kwenda mwendo wake ndio watu watapata uwokovu.
Ni kwa kuyatenda mapenzi ya Mwenyezi Mungu aliyemtuma mtumishi wake Yesu, kuwa ni Nabii na Mtume, kama mwenyewe mara nyingi alivyosema, ndio watu wataokoka.
Ni kwa kutenda mema na yaliyokuwa ya murwa kwa mujibu wa mapendo na sharia za Mwenyezi Mungu ndio kila mtu ataweza kujiokoa nafsi yake.
Sifa, bila ya shaka, itamrejea yule mwenye kuonyesha njia, na kwa hakika hivyo ndio amekuwa ni mwokozi wa watu. Mafunzo na maisha yake Yesu ndio muhimu yenye maana, na ndio hayo amejia duniani.
Ama mateso yaliyompata ni matukizi yaliyomzukia katika ile kazi yake, wala yeye hakuyapenda; au asingekimbia na kujificha na kumwomba Mungu amwondolee kikombe cha mateso na mauti. Yatufalia basi kuyatupa kando yaliyo muhimu na yenye maana, na tukan'gan'ganilia yaliyozuka tu?
TUTAFIKA ; HAPA KAZI TUUUUU
Umechoka kukariri quran umeahamia kwenye biblia
Biblia moja ya kitabu pendwa sana waislamu wameacha quran wanatumia biblia Ahsante yesu
Biblia moja ya kitabu pendwa sana waislamu wameacha quran wanatumia biblia Ahsante yesuMbona umechanganyikiwa unawataja waislamu wote na ilhali umeniambia mimi tu huko mwanzo , pata dawa hii upunguze mchanganyiko akilini
Hapa kuna nukuu zaidi zinazokanusha fundisho la utatu na uwongo wa kumkubali Yesu kuwa amekufa kwa dhambi zako ili upate uzima wa milele:
1- Matendo 20:34-36 BHN - “Katika mambo yote niliyofanya, niliwaonyesha kwamba kwa kazi ya namna hii imewapasa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe aliyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea. '"
2- Mathayo 5:9-11 "Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni wao."
3- Mathayo 5:8-10 "Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa Mungu."
4- Mathayo 5:5-7 "Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa."
5- Mathayo 5:6-8 "Heri wenye rehema, maana hao watahurumiwa."
6- Mathayo 5:7-9 "Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu."
7- Mathayo 5:3-5 "Heri wenye huzuni maana hao watafarijiwa."
8- Mathayo 5:4-6 "Heri wenye upole maana hao watairithi nchi."
Biblia moja ya kitabu pendwa sana waislamu wameacha quran wanatumia biblia Ahsante yesuKifungu hichi kifwatacho kutokana na Injili ndicho kinachoonekana chenye ushahidi mkubwa wa imani ya kuokoka kwa damu:
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Yohana 3.16-17
Hapa yafaa tutambue kuwa hii Injili ya Yohana ni khitilafu kabisa na zile nyengine tatu. Hii iliandikwa mwishoni kabisa baada ya zile.
Tangu awali haikukusudiwa hii kuwa ni maelezo ya kweli kueleza maisha ya Yesu kama yalivyokuwa, bali ilikusudiwa kuwa ni maoni ya huyo mwandikaji, naye amejaza humo mawazo yake mwenyewe.
Ni dhahiri kuwa Injili ya Yohana ilikusudiwa kuthibitisha imani ambazo alikuwa zilikwisha mvaa mwandikaji.
Wakati ilipoandikwa Injili hii Ukristo wa Paulo ulikuwa umekwisha pata nguvu na huyu mwandikaji alikuwa bila ya shaka ni mfuasi wa Ukristo wa Paulo, sio ule wa Yesu uliokuwa ukifuatwa na wanafunzi wake wa mwanzo.
Katika Injili hii ungu wa Yesu unatiliwa mkazo, na Yesu ndio anaitwa "Mwana wa pekee wa Mungu." Juu ya hivyo hii imani ya kuokoka kwa damu hata katika Injili hii haikusemwa kwa uwazi. Sana sana, itakuwa kama imegusiwa tu. Ni yule mtu ambaye akili yake tangu hapo imekwisha pikwa ndiye atafasiri maneno haya:
"Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye," kuwa maana yake ni kwa kufa kwake juu ya msalaba; au akafasiri "kila mtu amwaminiye" kuwa maana yake ni kuamini kuwa kifo chake kitakuwa ni fidia kwa dhambi za watu.
YESU KATUMWA KWA WANA WA ISRAELI TUUUUUUUUUUUBiblia moja ya kitabu pendwa sana waislamu wameacha quran wanatumia biblia Ahsante yesu