Injili ya Marko inasema:
Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa watu wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Marko 10.42-45
Kifungu hicho nilichokinukuu ni moja katika ushahidi unaotolewa katika thiolojia (ilimu ya Ungu) ya Kikristo kuthibitisha imani ya kuwa Yesu kaja duniani auwawe na damu yake iwe ni kafara au fidia kwa dhambi za wanaadamu.
Hebu natukiangalie vyema kifungu hichi, chasema nini?
- Yesu anasema "hakuja kutumikiwa bali kutumika", licha kuabudiwa.
- Maneno yasemayo: "kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi" ni wazi kuwa ni mfano, kama usemi: "anayetaka kuwa wa kwanza, atakuwa mtumwa wa wote." Bila ya shaka hapana atakayeona kuwa Yesu alikusudia kwa neno "mtumwa" ni kiumbe wa kuuzwa na kununuliwa. Hali kadhaalika "kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi" sio maana yake lazima kuuwawa.
- Tafsiri ya Biblia The Interpreter's Bible inasema wazi juu ya kauli hiyo ya Yesu kuwa haiwezekani kuitumia kuwa ni ushahidi wa thiolojia ya Paulo ya kuokoka kwa damu.
- Kauli hii lazima ichukuliwe kama ni mfano, kama usemi wa kishairi, kama ni mshabaha.
- Wako baadhi ya wataalamu wa Kikristo ambao wanasema kauli hii ama iliongezwa na Marko au na mtu mwenginewe baadae, lakini Yesu hakusema hayo. Lakini wenye kuandika hiyo tafsiri ya Biblia wanaona kwamba maneno hayo kayasema Yesu na yana maana ya mfano kama "vile mashahidi wa Kiyahudi walivyokufa kwa kuwaokoa watu wao (II Macc. 7.37-38; IV Macc. 17.22)" Ikiwa maana yake ni hivyo wanaona wafasiri wa Interpreter's Bible yaweza kuwa kauli hiyo ni kweli ya Yesu, kama ikichukuliwa maana nyengine haiwezi kuwa ni kweli.
Ikiwa basi Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi za watu, na ikiwa kweli yeye ni Mungu, basi mambo yote hayo ni kama sarakasi tu, mchezo wa kuigiza, au kiini macho.
Kwani hakika Mungu hawezi kuwa aliona uchungu kwa yale mateso, na kufa kwake kulikuwa hakuna maana, kwani kumbe hakufa.
Mungu hufa?
Yote hayo yaonyesha kuwa ni udanganyifu mkubwa.
Na ikiwa yote hayo yalikuwa yamekwisha kadiriwa tangu mwanzo na kupangwa na kutimiza bishara za kinabii na kwa kupenda kwake Yesu, basi hao waliomtesa na wakamwua yafaa wafikiriwe na watukuzwe kama ni watu wema waliowaletea heri wanaadamu wote, na wakamsaidia Yesu kutimiza lile alilolijia.
Hao akina Yuda, na Pilato, na lile baraza la wakuu wa Kiyahudi, wote hao ndio vipenzi vya Mungu, waliotimiza mapenzi ya Mungu baraabara.
Tutafika tu , HAPA KAZI TUUUU