Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Mwana harakati na Mjasiriamali carol Ndosi kupitia kipindi cha Joto Kali la Asubuhi TV-E ameweka wazi kukerwa kwake na kitendo cha Rais Samia kila anapopata nafasi kuongea na Watanzania basi lazima aseme kuwa yeye ni Rais mwanamke na yeye ni mwanamke. Amesema kuwa amekuwa akirudia mara kwa mara kila apatapo nafasi kuwa yeye ni mwanamke wakati kila mtanzania anajua kuwa yeye ni mwanamke.
Carol Ndosi anasema kuwa Rais Samia yeye ni Rais hapaswi kuendelea kujificha nyuma ya kimvuli cha uanamke kwani hilo si jambo zuri na haipendezi kwa Rais kuwa na hofu ya uanamke wake bali anatakiwa ajue watu wanamuamini kama Rais si kama mwanamke.
Amesema pengine Rais Samia anapitia mambo mengi kwenye chama chake au kwa watu wanaomzunguka kwa sababu ya uanamke wake lakini yeye kama Rais hatakiwi kuitumia kama ngao kwani yeye ni Rais na watu wanajua ni mwanamke hatakiwi kuwakumbusha watu, haipendezi.
Chanzo: TV-E/E-FM