CAS yapokea barua ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wapewa siku 10 kujibu

CAS yapokea barua ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wapewa siku 10 kujibu

Mnaacha kujadili masuala muhimu ya nchi mmekaa kujadili mambo ya kipumbavu ..Ndio maana kutwa kuombaomba watu misaada ..hamtaki kujishughulisha na mambo ya maana...Na haya ndio serikali inapenda
 
Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imepokea rasmi rufaa iliyowasilishwa na Klabu ya Young Africans SC dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Klabu ya Simba. Rufaa hiyo inahusiana na uamuzi uliotolewa na TPLB tarehe 8 Machi 2025.

Soma: Bodi ya Ligi: Kama Yanga wameenda CAS ni kichekesho, busara itumike sio kanuni

Baada ya kupokea taarifa hiyo, CAS imewapa walalamikiwa—TFF, TPLB na Simba—siku 10 kuanzia tarehe ya kupokea taarifa hiyo ili kuandaa na kuwasilisha utetezi wao.

Kesi hiyo itasikilizwa kwa haraka chini ya kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 huku pande zote zikitarajiwa kuwasilisha vielelezo na hoja zao ndani ya muda uliopangwa.

Klabu ya Yanga itawakilishwa na timu ya Wanasheria wafuatao;

1. Alex Mgongolwa
2. Simon Patrick
3. Juma Nassoro
4. Respicius Didace
5. Kalaghe Rashid

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) pia imetaka Simba SC, TFF, TPLB nao kuwasilisha wawakilishi wao Kisheria wakati Kesi ikianza kusikilizwa rasmi.

Pia, Soma
Simba hawatajibu! Wanataka kushushwa daraja,ili yanga iendelee na maisha yake
 
Umesoma kilichowekwa? Kisome kimantiki halafu tuijadili.
Redio kakujibu vizuri mashtaka ya yanga yanajulikana ata kama ayajawekwa hapo,,na ni mashtaka dhidi ya bodi, tff na Simba, hivyo kama unalo la kujadili jadili mashtaka husika!
 
Labda hiki ndiyo Kikwete alichosema kikitokea kikavurugavuruga mambo, maamuzi magumu itabidi yafanyike. Embu tusubiri tuone.

Possible outcome:
1. Tanzania kufungiwa kushiriki mashindano ya kimataifa
2. Tanzania kunyang'anywa uenyeji wa AFCON
3. Miradi ya viwanja vipya kutelekezwa
4. Tunarudi square one kisoka
5. Tunapata mgombea mwingine
 
Sijawahi kuona unafungua kesi ya rufaa wakati hukumu ya hiyo kesi unayoifungulia rufaa haijatoka rasmi.

Yaani unafungua kesi ya rufaa kwa kuambatanisha nakala za masikilizo na majibizano ya mahakamani na siyo nakala ya hukumu.

Sawa hatujahitimu VETA ila Uto acheni kutuchezea Watanzania. Hizi Sinema Zetu zinatosha sasa.

Active Cookie wekeni hii taarifa iliyoletwa kama TETESI hadi itakapothibitishwa rasmi na wahusika. Tulinde hadhi ya JF.
 
Simba, TFF na Bodi wakiona inafaa wataweka wazi nini kinacho pelekea wao kuitwa kwenye shauri ilo.

Mbumbumbu Leo mtaropokwa maneno ya kutosha

Redio kakujibu vizuri mashtaka ya yanga yanajulikana ata kama ayajawekwa hapo,,na ni mashtaka dhidi ya bodi, tff na Simba, hivyo kama unalo la kujadili jadili mashtaka husika!
Uto mbona mnatapatapa, wekeni mafuta kidogo ili huo mwiko usiendelee kuwasumbua.

Hivi hamjui mnavyodai mrudishiwe gharama za mechi ni kama mmekubali mechi kuahirishwa? Acheni uigizaji katika mpira!
 
Sijawahi kuona unafungua kesi ya rufaa wakati hukumu ya hiyo kesi unayoifungulia rufaa haijatoka rasmi.

Yaani unafungua kesi ya rufaa kwa kuambatanisha nakala za masikilizo na majibizano ya mahakamani na siyo nakala ya hukumu.

Sawa hatujahitimu VETA ila Uto acheni kutuchezea Watanzania. Hizi Sinema Zetu zinatosha sasa.

Active Cookie wekeni hii taarifa iliyoletwa kama TETESI hadi itakapothibitishwa rasmi na wahusika. Tulinde hadhi ya JF.
Acha bhange.
 
Back
Top Bottom