CAS yapokea barua ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wapewa siku 10 kujibu

CAS yapokea barua ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wapewa siku 10 kujibu

Hizo gharama mnazotumia lengo tu mpewe point 3? Mpira ni burudani wanachama wanahitaji burudani kwann msitumie uungwana tu mechi ipangwe upya na ichezwe kuliko gharama ya fedha, muda mnaotumia huko CAS?
Mpira burudani ilipaswa iwe tarehe 8. Busara ingetumika pale.
 
Wajinga wengi upande ule ukiongozwa na hersi akifuatia arafat haj na simon patrick
1000260207.jpg
 
Kupewa points 3 za kikanuni sio kucheza mechi?
Tunaandaa timu ili tucheze
Na siyo kila tukicheza tunapata alama 3 na magoli 3
Huwa tunapata magoli zaidi au pungufu
Huwa tunapata sare na kupoteza mchezo

Gharama za mchezo laZima zilipwe maana mchezo haukuchezwa sababu ya hujuma
Ni ama udai pwenti 3 za mezani au udai urudishiwe gharama zako za maandalizi ila vyote viwili haviwezi kwenda pamoja.
 
Sijasomea sheria.
Je, kwenye sakata hili Simba kosa lake ni nini hasa? Au anatakiwa ajibu nini huko mahakamani wakati aliyahirisha mchezo kisheria /kikanuni anajulikana?
 
Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imepokea rasmi rufaa iliyowasilishwa na Klabu ya Young Africans SC dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Klabu ya Simba. Rufaa hiyo inahusiana na uamuzi uliotolewa na TPLB tarehe 8 Machi 2025.

Soma: Bodi ya Ligi: Kama Yanga wameenda CAS ni kichekesho, busara itumike sio kanuni

Baada ya kupokea taarifa hiyo, CAS imewapa walalamikiwa—TFF, TPLB na Simba—siku 10 kuanzia tarehe ya kupokea taarifa hiyo ili kuandaa na kuwasilisha utetezi wao.

Kesi hiyo itasikilizwa kwa haraka chini ya kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 huku pande zote zikitarajiwa kuwasilisha vielelezo na hoja zao ndani ya muda uliopangwa.

Klabu ya Yanga itawakilishwa na timu ya Wanasheria wafuatao;

1. Alex Mgongolwa
2. Simon Patrick
3. Juma Nassoro
4. Respicius Didace
5. Kalaghe Rashid

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) pia imetaka Simba SC, TFF, TPLB nao kuwasilisha wawakilishi wao Kisheria wakati Kesi ikianza kusikilizwa rasmi.

Pia, Soma
Kwahiyo kama ni kweli imefika CAS, masna yake mambo hadharani kimataifa. Hapo mama hawezi tena kuingilia kuchezwa kwa dabi mana lungu kutoka FIFA linaweza kudondoka na kuifungia Tanzania kutokana na serikali kuingilia soka ukizingatia haters wa kijani wanaweza kupeleka vielelezo FIFA kwamba mama kaingilia soka.
 
Moto utawaka
Acha TFF, bodi ya ligi na mambumbumbu
Acha aibu iwapate
Unazingua sana, kuwa mwanaume sio unakuwa legelege, si wewe ndo ulisema Yanga tulegeze ili derby ipigwe? Sasa hivi unajifanya unashangilia hatua hii ya Yanga huko CAS.
 
Makosa makubwa ya jamii yangu ya kibongo ni kuchukulia kirahisi masuala magumu na pia kukariri, hili suala la Simba kukimbia mechi ni zito tuwaase mbumbumbu waache kujibu kishabiki, Yanga imetumia gharama kubwa kujiandaa na derby hii ngoma haiwezi kuisha kipuuzi tu na kihuni.

Yanga ni brand kubwa lazima iheshimiwe, hebu ona msemaji wake Ally Kamwe kapokewa Tabora kama mfalme halafu wahuni wachache wanakuja kuleta utani.

Ni Bora kesi iamuliwe CAS na Yanga tushindwe kuliko kubariki uhuni wa msimbazi na bodi ya ligi maana watazoea.

Na hapo Bado, tukishindwa CAS tunaenda Fifa na huko nako wakishindwa tunaenda UEFA kuomba muongozo na kuwalazimisha watutetee Fifa, lazima pachimbike ili siku ingine makolo wasijaribu kukimbia mechi.

Yanga ubishi na kudai haki yetu ni asili yetu! Makolo wakumbuke hata saa mbovu hupatia majira!!
Mkabeni kwanza ndio mpate point, hizo zingine ni tatarira tu. Morison, kagoma, fei 😁
 
Sijasomea sheria.
Je, kwenye sakata hili Simba kosa lake ni nini hasa? Au anatakiwa ajibu nini huko mahakamani wakati aliyahirisha mchezo kisheria /kikanuni anajulikana?
Labda Simba kama shahidi. Anaulizwa mfano;
CAS: Kwa nini haukwenda uwanjani?
Simba: Kwa sababu mechi ilihairishwa na TPBL.

Hapa kwa vyovyote vile mwenye kubeba dhamana kubwa katika kesi hiyo ni TBPL
 
Ni jambo lililowazi mgogoro unahusiana na wao Simba kugomea mchezo wa tarehe 8, ukumbuke Simba walitoa taarifa kwa umma kwa kuiandikia bodi barua iliyo wasilishwa bodi ya ligi.

Barua ile Yanga wali ituma CAS kama moja ya kielelezo cha Simba kugomea mchezo na kielelezo kingine cha taarifa ya Mwenyekiti wa bodi ndugu mguto ku ueleza umma kama mchezo uta kuwepo kabla ya masaa 5 baadae Bodi kuja na tamko la mchezo kutokuwepo.

Yanga ime lala mika kua Tff, bodi ya ligi na Simba walikula njama kwa pamoja ya kughairisha mchezo bila kufuata kanuni tulizo tunga wenyewe.

Barua ya Simba ili elezea kwanini hawatacheza mchezo, na Bodi watatakiwa waeleze CAS kwanini wali ughairisha mche masaa 5 baadae baada ya kusema mchezo utakuwepo.
Wakati uo Takukuru na Jeshi la polisi Tanzania awajatoa taarifa yoyote inayoweza kusababisha mchezo kusitishwa.
Ulifanyika upuuzi sana kuhairisha ule mchezo.
 
Ulifanyika upuuzi sana kuhairisha ule mchezo.
Ulifanyika upuuzi karia kuruhus gsm kudhamini timu 8 kwenye ligi moja isitoshe pia ulifanyika upuuzi mabaunsa wa yanga kuwepo uwanjani tarehe 7 simba alipoenda kufanya mazoezi na kuzuiwa na hao mabaunsa wa yanga na polisi wakiwepo kufunga njia bus la simba lisingie uwanjani
 
Back
Top Bottom