CAS yapokea barua ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wapewa siku 10 kujibu

CAS yapokea barua ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wapewa siku 10 kujibu

Si mara ya kwanza Yanga kushtaki CAS au kushtakiwa CAS, hasa na wachezaji na makocha. Hukumu zote zilizotoka aliyepata aibu anajulikana
Kwa hiyo mtu akishindwa kesi 1 au 2 ndio hatashinda kesi milele?
ALHAJ ALHAJ ALHAJ
ADEN ADEN ADEN
ISMAIL ISMAIL ISMAIL
RAGE RAGE RAGE
Popote ulipo Mungu wako anakuona ujue.
 
Uto mbona mnatapatapa, wekeni mafuta kidogo ili huo mwiko usiendelee kuwasumbua.

Hivi hamjui mnavyodai mrudishiwe gharama za mechi ni kama mmekubali mechi kuahirishwa? Acheni uigizaji katika mpira!
Gharama za mechi ndio madai pekee ya yanga? Mbona unakuwa kama amnazo!
 
Uto mbona mnatapatapa, wekeni mafuta kidogo ili huo mwiko usiendelee kuwasumbua.

Hivi hamjui mnavyodai mrudishiwe gharama za mechi ni kama mmekubali mechi kuahirishwa? Acheni uigizaji katika mpira!
Hatuweki mafuta tunakuweka hivyo hivyo kavu kavu
 
CAS ; CAF inasisitiza mchezo wa mpira uchezwe kwa gharama yoyote, Kwanini mmeahirisha mchezo halali wa Ligi? Kulikuwa na hali mbaya ya hewa?

TPLB; Hapana

CAS; Kifo labda cha mchezaji, kiongozi yeyote mkubwa?

TPLB; Hapana

CAS; Tishio la ugaidi, vita na uthibitisho kutoka mamlaka husika?

TPLB; Hapana

CAS; kwanini mmeahirisha mchezo halali wa ligi?

TPLB; Makomandoo wa Yanga wamezuia 5imba wasifanye mazoezi.

CAS; (wanacheka kwa nguvu, kisha wanakaa kimya)

CAS; Kwa mujibu wa kanuni zenu, kuna kipengele kinasema timu pinzani ikizuiwa kufanya mazoezi mchezo uahirishwe?

TPLB; Kulikuwa na tishio la usalama na dalili za rushwa

CAS; Tunaomba report kutoka mamlaka husika ikionyesha kulikuwa na mashabiki wenye mabomu, visu, mapanga au tishio la ugaidi kutoka idara za intelijensia au report kutoka TAKUKURU/ Police makao makuu/ JWTZ

TPLB; hatuna, ila mabaunsa jamani wametuponza! Tunaomba mtusamehe tuna familia zinatutegemea tukijiuzulu tutakula nini? Mguto atawaletea madafu ya Unguja, Mtusamehe

CAS; (wanacheka kidogo); Ok, Karia, Kwanini umeruhusu haya?

KARIA; sikutegemea tutafika huku jamani! Najuta kuwabeba wasiobebeka! Naomba mnisamehe nina familia inanitegemea!

CAS; Na nyie kwanini muandike barua ya kugomea mchezo halali wa Ligi na kuwalazimisha na kuwapangia bodi maamuzi?

5imba; Tulizuiwa kufanya mazoezi na makomandoo.

CAS; Kwahiyo mkizuiwa kufanya mazoezi, ndiyo muwapangie bodi maamuzi ya kuchukua na kususia mchezo halali wa Ligi na kugoma kuleta timu uwanjani?

5imba; (kimya, akiangalia chini) Lakini mkuu sisi hatuhusiki kwa sababu bodi ya Ligi ndiyo waliahirisha mchezo.

CAS; Kwa hiyo bodi ya ligi ndiyo waliandika barua ya kususia mchezo?

5imba; (Kimya akiangalia chini machozi yakimlenga)

ITAENDELEA...
 
Unadai vipi urudishiwe gharama halafu hapohapo unadai pwenti 3? Akili za kimwiko mwiko hizi.
Gharama za mechi laZima zilipwe kiasi cha million 56,435,000
Kuandaa timu
Mbali na takwa la kikanuni la points 3 na magoli 3
Yanga akitumia gharama kuandaa timu Kwa ajili ya kucheza
 
Gharama za mechi laZima zilipwe kiasi cha million 56,435,000
Kuandaa timu
Mbali na takwa la kikanuni la points 3 na magoli 3
Yanga akitumia gharama kuandaa timu Kwa ajili ya kucheza
Kwa hiyo mnataka kupewa pwenti 3 bila kuwa mmeingia gharama zozote?
 
Kwa hiyo mnataka kupewa pwenti 3 bila kuwa mmeingia gharama zozote?
Sisi tulitaka bodi ya ligi watuletee mpinzani tucheze nao tumfunge hata goli 6 lakini isivyo bahati wakamficha

Yanga hatuandai timu tupate points za mezani za kikanuni tulitaka tucheze Kwa ajili ya Wanachama na mashabiki wetu
 
Sijawahi kuona unafungua kesi ya rufaa wakati hukumu ya hiyo kesi unayoifungulia rufaa haijatoka rasmi.

Yaani unafungua kesi ya rufaa kwa kuambatanisha nakala za masikilizo na majibizano ya mahakamani na siyo nakala ya hukumu.

Sawa hatujahitimu VETA ila Uto acheni kutuchezea Watanzania. Hizi Sinema Zetu zinatosha sasa.

Active Cookie wekeni hii taarifa iliyoletwa kama TETESI hadi itakapothibitishwa rasmi na wahusika. Tulinde hadhi ya JF.
Nakukumbusha, Yanga wali iandikia Bodi kuwa wanastahili point tatu kama kanuni zinavyo elekeza kwakua Simba ili gomea mchezo.
Bodi ikawajibu kwa barua kua kulingana na kifungu cha kanuni iyo awastahili point 3 kwakua kulikua na ukosefu wa usalama na tuhuma za rushwa na vilevile Simba wali kiuka utaratibu wa kuto toa taarifa kwa Yanga, mamlaka za uwanja na metch commissioner kama watakwenda kufanya mazoezi uwanjani na watakwenda muda gani ili maandalizi ya uwanja yafanyike kabla ya mazoezi yao .
kama kanuni za CAF/ FIFA zinavyo sema.
Hitimisho la barua ile ni kuwa Yanga hawata pata point tatu na magoli matatu.

Walichofanya Yanga ni kuweka maelezo yao waki onyesha kanuni/ vifungu vya CAF/ FIFA vinavyo stahili kufuatwa ili wapewe haki yao kwenye iyo barua ya Yanga.

kuna sehemu wame weka ivyo vifungu kama utaisima vizuri.

Yanga imelalamika juu ya Tff, Simba na Bodi kuwa wamekula njama kwa kutofuata ivyo vifungu vilivyopo kwenye kanuni za ligi yetu ambavyo pia vipo kwenye kanuni za CAF na FIFA na wao Bodi kuvifumbia Macho na kuja na sababu za kikanuni zisizo FIT ku ghairisha mchezo.

Tukumbuke Mamlaka za Nchi zinazo husika na kushughulikia Rushwa(Takukuru ) na Mamlaka za ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao hazikua na taarifa yoyote itakayo pelekea mchezo ku ghairishwa.
 
Sisi tulitaka bodi ya ligi watuletee mpinzani tucheze nao tumfunge hata goli 6 lakini isivyo bahati wakamficha

Yanga hatuandai timu tupate points za mezani za kikanuni tulitaka tucheze Kwa ajili ya Wanachama na mashabiki wetu

Wewe ni mbumbumbu uliyekomaa tuondolee ujinga wako hapa!
Jibuni hoja. Hamjui kudai kurudishiwa gharama za mechi ni kukubaliana na maamuzi ya mechi kuahirishwa ili ichezwe siku nyingine. Kwa maana hiyo, madai ya pwenti 3 yanafia hapo hapo na mnakuwa mmeyaua nyie wenyewe.
 
Nakukumbusha, Yanga wali iandikia Bodi kuwa wanastahili point tatu kama kanuni zinavyo elekeza kwakua Simba ili gomea mchezo.
Bodi ikawajibu kwa barua kua kulingana na kifungu cha kanuni iyo awastahili point 3 kwakua kulikua na ukosefu wa usalama na tuhuma za rushwa na vilevile Simba wali kiuka utaratibu wa kuto toa taarifa kwa Yanga, mamlaka za uwanja na metch commissioner kama watakwenda kufanya mazoezi uwanjani na watakwenda muda gani ili maandalizi ya uwanja yafanyike kabla ya mazoezi yao .
kama kanuni za CAF/ FIFA zinavyo sema.
Hitimisho la barua ile ni kuwa Yanga hawata pata point tatu na magoli matatu.

Walichofanya Yanga ni kuweka maelezo yao waki onyesha kanuni/ vifungu vya CAF/ FIFA vinavyo stahili kufuatwa ili wapewe haki yao kwenye iyo barua ya Yanga.

kuna sehemu wame weka ivyo vifungu kama utaisima vizuri.

Yanga imelalamika juu ya Tff, Simba na Bodi kuwa wamekula njama kwa kutofuata ivyo vifungu vilivyopo kwenye kanuni za ligi yetu ambavyo pia vipo kwenye kanuni za CAF na FIFA na wao Bodi kuvifumbia Macho na kuja na sababu za kikanuni zisizo FIT ku ghairisha mchezo.

Tukumbuke Mamlaka za Nchi zinazo husika na kushughulikia Rushwa(Takukuru ) na Mamlaka za ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao hazikua na taarifa yoyote itakayo pelekea mchezo ku ghairishwa.
Kisa cha kuniandikia gazeti lote hilo ni nini?
 
Jibuni hoja. Hamjui kudai kurudishiwa gharama za mechi ni kukubaliana na maamuzi ya mechi kuahirishwa ili ichezwe siku nyingine. Kwa maana hiyo, madai ya pwenti 3 yanafia hapo hapo na mnakuwa mmeyaua nyie wenyewe.
Kupewa points 3 za kikanuni sio kucheza mechi?
Tunaandaa timu ili tucheze
Na siyo kila tukicheza tunapata alama 3 na magoli 3
Huwa tunapata magoli zaidi au pungufu
Huwa tunapata sare na kupoteza mchezo

Gharama za mchezo laZima zilipwe maana mchezo haukuchezwa sababu ya hujuma
 
Moto utawaka
Acha TFF, bodi ya ligi na mambumbumbu
Acha aibu iwapate
Nikwambie kitu na ukitunze sana; Maamuzi ya CAS yatakuwa kati ya haya mawili na yote sio rafiki kwa Yanga;
a) Kwakuwa mechi haijachezwa, basi ichezwe kwenye "neutral ground".

b) Kwakuwa Yanga ndio walikuwa wenyeji na walishindwa kuwahakikishia usalama wageni (Simba), basi Yanga inanyang'anywa pointi tatu na magoli mawili na watalipia gharama za kesi!!!

Nimekaa hapa Msimbazi nasubiria majibu!
 
😅😀😃We Sina hata cha kukujibu nimeona labda Leo April 1 ndo siku yako maalum upo unasherehekea
Kwa ujinga kama huu Rais Samia ana kazi kubwa
 
Back
Top Bottom