Case study Havard University: Ni kwanini kuna wasomi wachache kutoka mataifa ya kiarabu kwenye vyuo bora duniani?

Nimekuletea list hapo juu au hujaisoma??
Unapoitaja Palestina wapo wapalestina wenye vyeo QATAR,KUWAIT NA BAHRAIN AMA UNATAKA NIKULETEE??
 
Msaudi hata mmoja amewahi kushinda Noble Prize ?
Kwahiyo kushinda noble prize ndio kuwa na elimu kubwa??
Noble prize zipo za aina nyingi kuna peace noble prize,science noble prize,artsfacts noble prize n.k n.k we unazungumzia noble prize ya aina gani???
Maana mwaka jana kuna MuIran kashinda peace noble prize.
 
Waarabu hata UDOM wakuhesabu sana
Mimi nimesoma UDOM ila nimeachwa mbali na ambao hawajasoma UDOM, je ukisoma UDOM inamaanisha wewe ni msomi zaidi?

Watu wanasoma Cambridge huko na vyuo vingine, mtu anamaliza anapata kazi dunia nzima, ama kama anajiajiri anajielewa na hakiriri mambo kama vyuo vyetu.
 
Ishu sio kuisaidia India ishu ni influence ya mtu U.N na katika serikali za first world countries. Watetezi wa palestina wapo katika ulimwengu wa roho lakini sio kwenye dunia. Marekani na ulaya ni nchi ambayo ukiamua kukaza matako unatoboa lakini ukifocus kwenye kumbatona na kubeua pilau utabaki kulalamika. Wayahudi wanaitetea Israel kwa sababu wapo kwenye system. Viongozi na wanataaluma katika mataifa makubwa duniani wengi wao ni wayahudi. Hicho chuo tu cha Harvard kilipochukua upande wa palestina wayahudi waligoma kukisaidia kifedha. Ninajaribu kuwaelimisha ndugu zangu kuna mambo mengi ya dunia watu hawajui kwa sababu hawasafiri.
 
Hawa jamaa wana chuki binafsi na jamii ya kiarabu.
Mie huwa nafuatilia sana mienendo ya siasa za middle east na nina ndugu wapo huko wana vitengo vizuri tu.
Mmoja anafanya kazi kampuni ya utengenezaji magari ya umeme UAE na hiko kiwanda kimeanzishwa na waarabu wenyewe.
Hawa wanachoshindwa kuelewa waarabu wa sasa sio wale wa zamani,waarabu washaona athari wanazopata za mataifa yao kuburutwa kisa kukosa wasomi wabobezi sasa hivi wamezinduka wana recruit maprofessa wakubwa toka China kuwaambukiza ujuzi aisee nyanja ya sayansi na teknolojia.
Embu aende akafuatilie Doha AI summit huyu jamaa kesha arudi hapa.
Ila hawa jamaa ni vile hawapendi kujisumbua ila asahv kusoma wanasoma na wana mifumo yao ya uendeshaji nchi sio lazima ifanane na ya wamagharibi kama hawa wanavyotaka.
 
Nimekuletea list hapo juu au hujaisoma??
Unapoitaja Palestina wapo wapalestina wenye vyeo QATAR,KUWAIT NA BAHRAIN AMA UNATAKA NIKULETEE??
QATAR, KUWAIT NA BAHRAIN zina influence gani katika maamuzi ya dunia ? zipo G8 au NATO ? Inaeleka haujui dunia inaendeshwaje. Kuna m´nchi ambazo zinapanga maamuzi makubwa ya dunia yanafanywaje na kuna nchi zinakaa kimya na hazijui nini kinaendelea. Unajua mpaka leo Marekani ina kambi Saudi Arabia ? Na utajiri wote huo wanashindwa nini kumfukuza mmarekani ? pia wana kambi Qatar, Bahrain, Kuwait, na U.A.E . Shule muhimu kuliko pesa . Hiyo list ipo wapi naomba uniletee ?
 
Noble prize kwanza ni Tuzo za zionist, zimejaa wauaji kibao, Kuna watu kibao dunia hii wamefanya makubwa hawana Noble prize na kuna watu wamefanya mauaji ya Halaiki wemepewa hii tuzo. Mfano

Raisi wa Maynamar ana hii tuzo baada ya kuua Malaki ya Rohynger

Wamempa hii tuzo Raisi WA Ethiopia ambaye naye anaua tigray huko

Barack Obama kapewa na Iraq, Afghanistan yake

Anwar El sadat alipewa hii tuzo Raisi ambaye alikuja Kuuliwa na Wanajeshi wake kwa usaliti.

Hata ukiangalia zamani vita vya dunia vya kwanza na pili kuna watu Kibao wamepewa Noble prize kwa mauaji yao.
 
Wewe MuAfrika una nini mpaka sasa???
Bora hata waarabu wameanza kujitutumua kupingana na western world kwa namna moja ama nyingine maana wana mataifa yenye fedha mathalan Qatar na Kuwait na wana mataifa yanayojiweza kijeshi kama Lebanon na Iran.
Ninyi Afrika matatizo yenu wenyewe yanawashinda ya M23 na balaa njaa huko Kenya,Ethiopia na Somalia.
Kwa hizi akili zenu Afrika na Tanzania zitabaki masikini mpaka kiyama.
 
Mbona unahama hama sana??
Hii dunia inaenda na geopolitical influence and interests.
Hizo G20 na G8 hazifanyi kazi sasa hivi we jamaa mbumbumbu.
Zingekua zinafanya kazi Brazil,Cuba,Spain,Belgium na mataifa mengine yasingeenda kinyume na Israel na USA pale Israel ilipovamia Gaza 2023 Octoba 8.
Qatar kupitia kituo chake cha Aljazeera aliionesha dunia kuwa mbivu ipi na mbichi ipi kuhusu mzozo wa Palestina dunia MPAKA RAIA WA USA WAKAENDA KINYUME NA USA NA ISRAEL.
Dunia ya sasa haiendeshwi kama udhaniavyo wewe jamaa.
Geopolitics zimebadilika upepo.
Ukizingua sasa hivi hatujali G8 wala G20 tunakuvuruga mpaka ukae mezani na sisi.
Mathalan Houthi rebels wa Yemeni wameifunga red sea hivyo vikao vya G20 na UN vilisaidia kuifungua red sea??
Dunia ya sasa hivi haiendi hivyo ukizingua wanakuzingua.
 
Japo Anwar Sadat aisee alikua jembe isipokua Misri ni taifa liloendekeza sana uroho wa madaraka.
 
Duniani mungu tukubali ametuumba tofauti , kuna working class ambao lazima tupate vyeti ili tuajiriwe na hapa kuna watu wa vipato vya kati na maskini na kuna wale ambao mungu amewaumba na uwezo binafsi wa kupambana hapo kuna kina gsm na kina bakhressa nadhani umepata jibu
 
QATAR, KUWAIT NA BAHRAIN zina influence gani katika maamuzi ya dunia ? zipo G8 au NATO ? Inaeleka haujui dunia inaendeshwaje. Kuna m´nchi ambazo zinapanga maamuzi makubwa ya dunia yanafanywaje na kuna nchi zinakaa kimya.
Kukiwa na hela kuna influence, why Qatar kapewa kuandaa World cup? Why mashindano karibia yote mpira, magari, tennis na mengineyo sasa yanafanyika Nchi za kiarabu?

Hela za Mafuta zimejaa mabenki ya west, hao credit suisse juzi juzi hali ilikuwa tete wanafilisika Saudi akatia mpunga kuwakomboa,

Wewe tumia chochote sasa hivi, FB, Twitter, Tiktok, Sikiliza mziki youtube, kanunue iphone ama Tecno kuna possibility kubwa umewaingizia hao jamaa hela.
 
Jiulize kwa nini major events za duniani hata jana anthony joshua kapigana riyadh saudi arabia kaacha kupigana kwao uingereza au marekani kaenda uarabuni ndio utajua nani mwenye vyeti na nani mwenye akili
 
Nimekuletea list hapo juu au hujaisoma??
Unapoitaja Palestina wapo wapalestina wenye vyeo QATAR,KUWAIT NA BAHRAIN AMA UNATAKA NIKULETEE??

Asante sana nipo ujerumani ninasoma huku nafanya kazi katika kiwanda cha continental ninangia ofisini mara mbili kwa wiki. Na mwaka jana nilipokea tuzi ya mfanyakazi bora wa mwaka. Ninasomea Industrial Engineering and Management nategemea kumaliza research yangu mwakani 2025. Nikimaliza nitafanya PhD, wajerumani wananiheshimu sana kwa kazi ninayoifanya. Nikimaliza nina mpango wa kurudi nyumbani nifungue kiwanda. Usiseme Afrika itabaki masikini mpaka kiama jipige kifuani sema "mimi nitabaki masikini mpaka kiama". Kuna kitu kinaitwa focus mimi ninafocus kwenye kazi yangu kwa asilimia mia moja. Nilifika huku mwaka jana mwezi wa tatu lakini sasa ninaongea kijerumani vizuri. Kuna watu wana miaka kumi huku lakini wanang'ang'ania lugha zao na wanalalamika kuwa wanakosa kazi nzuri. Haijalishi wewe ni dini, kabila au tabaka gani huku ukikomaa unatoboa. Nina maboss ambao wanatumia Cocaine, Ketamine, Marijuana na wengine ni mashoga na wasagaji . Mimi siviafiki hivyo vitu lakini kwenye kazi nakubali kuwa ni wachapakazi japokuwa nje ya kazi siwezi kuwa na urafiki nao. Afrika ni sawa na wapalestina tuna malengo ya muda mfupi hatuna malengo ya muda mrefu. Ukifuatilia mpango wa Israel wayahudi hawakuamka asubuhi na kuamua iwe hivyo. Wali-infiltrate serikali za mataiffa makubwa.
 
Hela haiwezi kununua ushawishi rafiki yangu ushawishi unanunuliwa na uwekezaji wa muda. Na uwekezaji mzuri wa muda ni mahusiano na elimu kitu ambacho Qatar hana. Unadhani wahindi au waarabu ndio waliosaidia Mo asiuliwe alipotekwa ? Mashindano ya mpira, magari, tennis yatasaidiaje katika ukombozi wa palestina ? FB, Twitter, Tiktok na youtube zitasaidia vipi kuwafanya Marekani na mataifa makubwa yasiisaidie Israel ? Naomba unijibu.
 
Wewe unaangalia short term, wenzako wanaangalia mbali, na Matokeo yanaonekana. Zamani ukiongelea support ya Israel Ulaya na Marekani tunaongelea almost 100% support, hawaulizi ila sasa hivi wanapata hio support? Imebaki wazee tu, Vijana wengi ambao wamezaliwa miaka 30-40 iliopita hawasuport Israel bila kujali rangi zao.

Unaweza ukasoma hii poll

Nchi kama Japan na Korea ambazo kikawaida zinasuport west ila support imeshuka vibaya mno kwa Israel.

Ukiangalia hizo nchi za South America zote ni pro palestine siku hizi, Tumeona Brazil na Colombia walivyopigana kuwatetea Palestina.

So hii ni trend inakua, taratibu pro palestine wanakngezeka, Ulaya sasa hivi wapo vulnerable, haya mataifa ya America Kusini na Asia yakiwa makubwa kiuchumi kupitia Ulaya Ofcourse nayo yatakua na say na kuweka vikwazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…