Uchaguzi 2020 CASE STUDY - Jimbo la Hai - Walitumia teknolojia gani kupata matokeo sahihi ya kila kituo ndani ya saa 8?

Wananchi sisi ndiyo tunazingua big time uchaguzi umeharibiwa kukaa kwetu kimya kuwakatisha tamaa sana viongozi wa upinzani ambao wamesacrifice maisha yao kwa kiasi kikubwa sana
 
Huwezi kususia uchaguzi bila plann B.

Kususia uchaguzi kusingebadilisha chochote kwenye tume ya uchaguzi...
Sasa mkuu kipi tumekikimbia...
Platform ipi tunayo ya kusema kuhusu tume huru
Hakuna Tofauti kama tungesusia...
ona sasa mpaka sasa hatuamini kilicho tokea...
 

1. Kuwa shahidi ama kulipeleka jambo hili mahakamani wala hiyo siyo ishu kaka..

2. Mimi kueleza ninachofahamu kama namna ya kutoa maoni yangu wala siyo kosa na ndiyo maana na wewe ukatumia maoni yangu kama "base" ya kusema yako pia..

3. Hoja ya kutumiwa ni ya kijinga sana. Maana kama mimi kutoa maoni yangu ni "kutumiwa", wewe uliyoandika yako unaweza kuwa unatumiwa na nani eti?

4. La mwisho, kuibwa ama kutengeneza matokeo fake hakufanyiki vituoni wewe. Haya yanafanyika ndani ya ofisi za NEC maarufu kama wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo...!!

Hiki kinachofanyika kwenye vituo vya kupigia kura ni justification tu kuwa kulifanyika uchaguzi..

Inaweza ukawa hata huelewi ni kwanini katika vituo vya kupigia kura 81,000 nchi nzima, zaidi ya vituo 57,000 nchi nzima mawakala wa vyama vya upinzani hususani CHADEMA walikataliwa kufanya kazi yao kwa sababu mbalimbali...!
 
Nendeni mahakamani mkadai haki yenu.
 
Sasa mkuu kipi tumekikimbia...
Platform ipi tunayo ya kusema kuhusu tume huru
Hakuna Tofauti kama tungesusia...
ona sasa mpaka sasa hatuamini kilicho tokea...
Kwahiyo ulitaka wasusie then wachukue hatua zipi ?

Politics ni mapambano huwezi kuacha kupambana wenzako watafaidika na kususia kwako.

Currently now kila kitu kipo exposed we can have a backing even kwenye international community.

Kikubwa wananchi tunapaswa kuwapa support viongozi wa upinzani they have suffered a lot kutupigania.
 
Umeandika vizuri.

Kama umenisoma vema hapo juu nimetumia neno laiti, nikiwa na maana kwamba siwazuii viongozi wanaoona wameonewa majimboni waende mahakamani, lakini pia, ukweli lazima usemwe, kea utawala wa awamu hii sidhani kama kuna hakimu yeyote atakayethubutu kuwapa haki wapinzani ikiwa bosi wao alishatoa maelekezo kwa wakurugenzi mapema Chadema inatakiwa ife ifikapo 2020 na kilichotokea kwny uchaguzi ndio majibu yake.

Kuhusu kushiriki uchaguzi, utakuwa vipi na maelezo ya kujitosheleza au hata kupeleka ushahidi wa irregularities mahakamani kama hata huo uchaguzi hushiriki? locus standi yako itatoka wapi?! ni lazima washiriki uchaguzi, then patakapotokea baya km tulivyoona this time, ndio Chadema na wengine waende mahakamani kupinga matokeo, hivyo suala la kushiriki nalo halina mjadala.

Suala la kuandamana, hili nalo japo lipo kikatiba lakini utaweza vipi kuwalaumu wasioandamana kama unasikia kamanda wa jeshi la polisi akisema hadharani watakaoandamana watavunjwa miguu km vile kuandamana ni kosa kisheria? hapa badala ya kuwalaumu wasioandamana, ningekuona mjanja zaidi uwalaumu wale waliopewa mamlaka na sheria ya kuwalinda waandamanaji, lakini badala yake wanawatisha waandamanaji, kumbuka wao wana marungu waandamanaji hawana kitu.

Hivyo basi, sioni utoto wowote kwny hizo sababu nilizokuwekea hapo juu, wajibu wako km raia unaejielewa nchi hii unatakiwa kuzikumbusha mamlaka zitekeleze wajibu wao bila kuingiliwa na yeyote, au kumpendelea yeyote, hapo ndipo taifa letu litasonga mbele, lakini kuwalaumu waliofungwa kamba mikono iko nyuma eti kwanini hawachukui hatua ni kuwaonea.
 
mkuu unalijua hilo jimbo mbona ni dogo sana ndani ya saa moja unaweza kulizunguka na barabara zake nyingi zina lami sio pakubwa kama unavyozani manake ukienda kidogo huku uko siha ukiludi huku kidogo uko moshi vijijini
 
Locus standi sio wote wanaelewa mkuu asa hao lumumba....
 
1. Kuwa shahidi ama kulipeleka jambo hili mahakamani wala hiyo siyo ishu kaka..

2. Mimi kueleza ninachofahamu kama namna ya kutoa maoni yangu wala siyo kosa na ndiyo maana na wewe ukatumia maoni yangu kama "base" ya kusema yako pia...
Ok.
Mimi nimekushauri tu,, wasaidie kama inawezeka kukusanya ushahidi. Kama unavyosema, nyie kwenye kituo hamjamaliza kuhesabu tayari matokeo yametoleewa. Hili tosha linaweza likawa la kulitolea ushahidi na kuwasaidia kuliko liishie Jf.

Hii nchi tunaweza kuondoa hizo dhurma so usiwe sehemu ya uonevu uliotokea. Humu kuna watu wa aina tofauti, kuna wengine ni wepesi wa kuhukumu na kujawa na jazba, maelezo yako yanaweza kuleta taflani na kuibua hisia za kuzuru mwingine. Kukaa kimya hakusaidii kabisa na kuishia jf ni vilevile.
 
Swali dogo la kujiuliza Mkuu ni " Kama Tume ya Uchaguzi haiko Huru vp Mahakama zetu?? Kumbuka Mahakama walishaambiwa Serikali ninayoiongoza mimi ndiyo mtafutaji wa fedha za kuendeshea Mahakama. Ole wenu Serikali kupitia Mawakili wake Waanguke kwenye case yeyote ile.
 
kususia tungeona kuna shida mahali....
Huwez ukasema Bar pabaya alafu kila siku unaenda... watu tutaaminije kama pabaya mpaka uache kwenda
 
Locus standi sio wote wanaelewa mkuu asa hao lumumba....
Waulize maana watapewa tu.

Simply ni neno la kilatini, meaning; "a place to stand", yaani malalamiko yako mahakamani yana "base" kwenye nini.
 
Asante sana kwa maoni yako..

1. Unaweza kurudia kunisoma tena kwani inawezekana umeskip baadhi ya mistari inayojibu baadhi ya hoja zako hizi..

2. Hata kama vituo vyote vingekuwa pale Hai mjini (Bomang'ombe) achilia mbali kuwa umbali wa 30km, haiwezekani logistics zote kuanzia vituo vya kupigia kura, katani na jimboni zikamilike ndani ya masaa 8 baada ya vituo vya kupigia kura (siyo kumalizika kwa zoezi la kupiga kura) kufungwa..!!

3. Katika mchakato mzima wa uchaguzi, ugumu wa zoezi upo kwenye kuhesabu kura kwenye kituo na kukubaliana na kutokukubaliana kwenye ishu ya kura zilizokataliwa na zenye mgogoro..

Baada ya mtu wa mwisho kupiga kura, uwezekano wa matokeo ya kituo kuwa okay huenda hata Masaa 2 hadi 5 kutegemeana na kituo..

4. Wanaolalamika watapata wapi matokeo iwapo mawakala wao kwa sababu inazozijua NEC yenyewe iliwanyima barua za utambulisho na kama walipewa basi zilikuwa zimeandikwa kwa makosa kwa makusudi ili lengo la wizi wao lifanyike kwa urahisi?

Hoja ya "rigging and fraudalent election" katika mazingira haya haiwezi kujengwa kwa kutumia matokeo ya kura za uchaguzi bali mchakato mzima ulikuwa batili...!!
 
kususia tungeona kuna shida mahali....
Huwez ukasema Bar pabaya alafu kila siku unaenda... watu tutaaminije kama pabaya mpaka uache kwenda
Vp kihusu ule uchaguzi wa Serikali za Mitaa?? Mlichukua hatua yeyote au mlishangilia??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…