Maajabu hayaishi. Kuna biashara gani nzuri hivyo gerezani Ukonga? Hivi, akifungwa mmoja, kwa nini mfungwe wote watatu, si bora wabaki wawili nje watafute chakula cha watoto? Hawa kina Mama nadhani ni wake za watu, wana watoto wao, na wajukuu, kwa nini wawasikitishe wenza wao?Hawa wamekamatwa leo Katika viunga vya Mahakama ya Kisutu walipofika kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti wa Chama chao , aliyeshitakiwa kwa kesi za uongo ili kumkomoa kutokana na kupigania haki nchini Tanzania, ikiwemo Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Kesi iko mikononi mwa serkali, imepangiwa tarehe, ushahidi utatolewa, mahakama itaamua, haraka ya nini? Na kama issue ni Tune Huru, kwani itazinduliwa wiki hii Kidutu au mwezi ujao Gereza la Ukonga? Si ni mambo ya bungeni, na inachukua muda? Mabango ya Kisutu ni ya nini?
Viongozi wa Dini, Mufti, Maaskofu, Wachungaji, wote, tuiombee Nji yetu kuna shetani anatamba sana sasa hivi hewani. Hasa KKKT Maaskofu wana jukumu zito kwa sababu CHADEMA officially ni chama chao tangu zamani, tunaomba mfunge novena shetani ashindwe.