Halafu akilinda maslahi ya Zanzibar atalaumiwa kama JPM kwa "ukanda/ukabila."
Dear Chadema, jitahidini kufahamu vipaumbele vya Watanzania kisha muwe kipazasauti cha vipaumbele hivyo. Kadhalika, jibidiisheni kusoma upepo wa kisiasa ulivyo. Mama Samia anapendwa na Watanzania, pengine kutokana na kuwa Rais wa kwanza mwanamke. Lakini pia anaongea lugha ya kistaarabu. Sasa mkicheza ovyo karata zenu, mtaishia kuonekana mnam-bully.
Mwisho, mjibidiishe kuwa proactive. Anzisheni mijadala itakayowafanya Watanzania wafanye tafakuri badala ya sasa ambapo mnaendeshwa kwa matukio. Mnasubiri Mama Samia atamke hili au lile mpate cha kuongea.
Povu ruksa [emoji4]