Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,255
- 1,565
Toka Chama cha Mapinduzi kuundwa mwaka 1977 kimepita baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union na Afro - Shiraz, CCM imekuwa Imara, Bora na yenye mshikamano kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka ngazi ya Taifa kuliko kipindi chochote cha uhai wa CCM.
Kabla Mama Samia Suluhu Hassan hajakabidhiwa kijiti cha kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, iliaminika ikuwa CCM ni chama ambacho kinabebwa na mfumo , iliaminika kuwa CCM ni chama ambacho hakipendwi na Vijana, kwa lugha nyepesi ilionekana ni Chama cha Wazee.
Mama Samia Suluhu Hassan amefanikiwa kwa asilimia 100 kurudisha imani kwa Vijana kuwa CCM ndio chama bora, chama rafiki, chama chenye kubeba maono ya Watanzania, CCM ya sasa chini ya Mama Samia Suluhu Hassan Hassani si kile chama kilichokuwa kinategemea nguvu ya dola.
Watanzania kwa sasa wanashuhudia CCM yenye siasa za kiungwana, hakuna tena yale matamko ya kibabe, majivuno na ya kutishana kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM au kutoka kwa Katibu Itikadi na Uenezi, CCM ya sasa ni ile inayoendesha siasa zake kistaarabu saana.
Mama Samia Suluhu Hassan ameweza kutenganisha vizuri kati ya mamlaka ya Serikali na Chama, CCM imeweza kuisimamia Serikali vizuri hasa katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo, ni CCM iliyo chini ya Mama Samia Suluhu Hassan ambayo imeweza kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini, imehakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule ameanza shule, imeweza kumtua Mwanamke ndoo kichwani kwa kuhakikisha maji safi na salama yanafika kila kijiji, imehakikisha umeme umefika kata zote Tanzania, imehakikisha kila Kata kunakuwa na Kituo cha Afya, kila Kijiji kunakuwa na Zahanati yenye vifaa na madawa, CCM kwa kuisimamia Serikali vizuri imeweza kumalizia miradi iliyokuwa imekwama kwa miaka mingi ikiwa ni pamopja na umaliziaji wa maboma ya vyumba vya madarasa na Zahanati.
Hongera sana Mama Samia Suluhu Hassan, Hongera sana Daniel Chongolo kwa kuitengeneza CCM IMARA inayopendwa na Watu wote.